Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Ahaa haaa bila shaka nilikuogesha kwenye ule mfereji uliopita kati ya uwanja na mabweni [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Yaani akili za kitoto bhana. Ilikua principle form five wakishareport tunawamsha kuwakaribisha uboyzini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!.
Umenikumbusha enzi za kuamka saa10 alfajiri kunywa uji then kwenda shamba weruweru kulima. Kipindi Cha mvua gari likikwama lazima msukume Hadi litoke. Kuna kipindi tulikoswa koswa kutumbukia mtoni na gari maana tairi za gari zilipita kwenye foundation ya daraja na halikuwa na Kingo. Yule dereva mzee masharubu siku hiyo alikuwa kapiga furu.
Kwangu Mimi Yale maisha yalifundisha na yamenifanya kuwa mtu wa kazi.
I missed mbuzi,kwaya, fongo,kuendesha ndege n.k
Popote ulipo Headmaster wa enzi hizo Mwl. Bureta nakupa heko kwa kunifanya nkapitia JKT Lyamungo indirect😆😆.
 
Nimesoma Umbwe,ugomvi na lyamungo umeanza muda,hata sisi tulivyowakuta mabraza walikuwa wanatupa story za ugomvi na lyamungo
Na hii yote ilikuwa kutokana na kuzungukwa na shule za kike ambazo tulikuwa tunamahusiano nazo (disco,michezo, debate n.k) tulikuwa tunaita "social" Kama weruweru,kibosho girls ,machame girls na Kuna nyingine siikumbuki ilikuwa mbele ya lyamungo ukitokea kindi sikoni Mara nyingi tulikuwa tunaenda kwenye joint mass.

Sasa hii ilikuwa Kama majogoo wanagombea matetea...pamoja haikuwa nzuri kwenye jamii lakini ilitujenga kuwa pamoja kuitetea shule,kuwa na mshikamano linapotokea Jambo kwa mwenzetu pia kutufanya tuishi km wanajeshi ,na pia ilipungaza unyoro nyoro km watoto wa boarding siku hz
Sijajua km machata (4uz,5JECCAS)yetu kule vyooni lyamungo na vyoo vya maputo Umbwe bado yapo
 
Kweli mkuu ile shule ni zaidi ya jeshi mpaka namaliza form 2010 nilishukuru Mungu, ilibidi nikatoe shukrani kanisani kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini waliokosea ni umbwe kuwafata lyamungo ilhali wangetulia sidhanj kama yangetokea hayo kwa jamaa. Kilichomuua jamaa ni kubaki kuendelea kuharibu mali.
Yap, alijikuta captain akaendelea kurusha mawe watu wakaanza kumkimbiza akafika uwanjani alipigwa mtama hapo ikawa kila aliyemkuta anapiga sio mwenye fyekeo, mwenye mpini, mwenye jiwe, wengine walimkanyaga dah so sad mpaka akakata kamba. Kuna mwenzake nae alikimbilia nyumbani kwa mpishi alichomolewa akaletwa pembeni ya mwenzake. Nae alikula kichapo ila wakamuonea huruma. Akapelekwa KCMC ila nadhani alipona. Na kama alipona nadhani alipata kilema cha maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uboyzini acha tu
Nimesoma Olevel Ihungo Boys Bukoba tuligoma wkt sina hela na tukawa haturuhisiwi kula, tukaenda kimya kimya uwanja wa mayunga pale bkb town, tumefika tu defender zikaanza kuzunguka uwanja. Hamna kutoka kwenda mtaani na ilkuwa usiku na asbh sikuwa nmepata breakfast na mchana nikawa nimepinga pass ndefu, ilipofika saa 6 usiku nikazimia kwa njaa rafiki yangu Edmund akanipa maandazi mawili(Mungu ambariki) roho ikarudi[emoji1787][emoji1787].
 
Hii shule mpka wanafunzi mnapanga yoye hayo uongozi uko wapi😳😳😳
 
Jamaa walitukata mikia nakumbuka tulikuwa form 5 wandiba alikuwa chizi sana...niliteseka miezi mitatu nikaona nihame shule...hivi madam Keisha bado yupo?
 
Nyie wajinga mlituogesha na kutukata mikia kwenye ule mfereji...karibu na bweni la Alhasani...namkumbuka Rad man na jamaa anaitwa Mchina alikuwa dom leader sijui wako wapi now.
 
Ahaa haaa ulishindwa mtiti. Dah yule madam alikuwa mweupe kama mzungu. Sijui alifikiria nini kuja kufundisha uboyzini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtiti ulinishinda kila siku kuogeshwa kwenye mfereji,nakumbuka mara ya mwisho tulilala porini na mshikaji wangu tulipokea taarifa nmapema kwamba form 5 usiku huo walikuwa wanakatwa mikia...na kweli jamaa walikatwa mikia asubuhi tulikuta jamaa wanalia...kule bweni la mkapa kuna jamaa alivunjwa kichwa alisukumwa kwenye ngazi....kuna mshkaji alikuwa anaitwa Bitoz form six walikuwa hawampendi kisa tu ana perfume nzuri walitaka kumuuwa.
 
Dah maisha bana ila kuna kumbukumbu nzuri na mbaya asee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…