Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

 

Duh! Mag3 una wajukuu wangapi sasa?


Dah! Heshima Mkuu. Shikamoo.

Mkuu umehamia digitali kweli?

Hahahaha Mkuu Mag3 naona umezua jambo hapa, watu wanataka kufahamu hadi na idadi ya wajukuu zako.
Bila shaka huu ni uthibitisho tu kwamba JF ina kila aina ya watu ambao pengine mtu asingetarajia, na ndio maana JF inakuwa na nguvu zaidi na ubora zaidi kuliko mitandao kadhaa ya kibongo iliyopo.
 
Last edited by a moderator:
Haina shida waache wa msimamishe tundu lissu aje apige amsha amsha mtaani huku wasisahau kumuongeza na mchungaji peter msigwa hapo maana hao jamaa wakiingia mtaani miezi sita watakuwa wamepiga kazi ya maana sana m4c tutawaacha vijana wanatosha kukimbiza wabunge wote hao wa ccm!!!!!!!!!1
 
mkuu ni wachache sana ambao hawajawahi kuvuta bangi, inategemea hiyo bangi inakusaidiaje, au ilikusaidiaje au ilikupotoshaje, mimi O'level nimeikandamiza sana,
Bangi ikikukataa unateseka sana. Ngoja tusubiri orodha ya WABUNGE wavuta bangi. Bila shaka Madame Spika ataiweka hadharani ili tuwafahamu. Wabunge vijana ni wengi mno na kama wavutaji bunge letu halitatulia.
 
Bangi ikikukataa unateseka sana. Ngoja tusubiri orodha ya WABUNGE wavuta bangi. Bila shaka Madame Spika ataiweka hadharani ili tuwafahamu. Wabunge vijana ni wengi mno na kama wavutaji bunge letu halitatulia.
mkuu unadhani atakaowataja mheshimiwa madam speaker ndo wavuta bangi au yeye ndo anatumika na wavuta bangi?
inawezekana wote ni wavuta bangi ila bangi zinawasaidia tofauti kiakili......
 
Mkuu Moshe, nakuomba ulitendee haki hili jukwaa, hapo kwenye white!.
Mode please weka vile vi xxxx kwenye hilo neno!.
Pasco.
 

mkuu, Tundu kasoma A'level Galanos. Ilboru kasoma O'level. Sasa alihama kutoka Galanos kwenda Ilboru kivp?. Tuliosoma pale Galanos japo hatukumkuta ila rekodi zinaonesha amesoma HGE pale. Naona umechapia kidogo mkuu.
 

Unamawazo mgando kaka Pasco, huyo Makinda pekee ndiye brain behind the bunge bovu?
Ndugai, Lukuvi, Mwanasheria mkuu , wasira nk hawa pia ni skirt?
Au bado uko huko, hujatoka bado???
 
mkuu unadhani atakaowataja mheshimiwa madam speaker ndo wavuta bangi au yeye ndo anatumika na wavuta bangi?
inawezekana wote ni wavuta bangi ila bangi zinawasaidia tofauti kiakili......
Wenye akili nyingi darasani wakilivuta wanakuwa ni walipukaji sana. Kwa trend ilivyo Bungeni sasa, wavutaji ni wengi.
 

Mkuu,
Huoni kama maelezo yako yanajichanganya............Kwanza unamsifia Mh.Sitta, halafu hapo hapo unasema alikuwa anayumbishwa na Dr. Slaa, tena huoni soni, kama Mh. Sitta alikuwa anayumbishwa na mtu mmoja, kwa nini usione kama kulikuwa na tatizo kuliko la Mh. Makinda kuyumbishwa na watu wengi wasomi walioingia bungeni ........Sasa sijui nielewe lipi............jaribu kujenga hoja inayoeleweka.

By the way, wewe ni kabila gani?.
 
Acha kupotosha watu wewe hujui Tundu ni litobo lililowazi.Halafu mtu mwenyewe anapenda kulialia mnajidai kumsifia

View attachment 82223

Mkuu pamoja na chuki iloonesha kwa mheshimiwwa Tundu, kiswahili chako vipi? Likesha kuwa "Tobo" ni lazima liwe wazi. Huwezi sema tobo lililo wazi.
 
Mkuu Moshe Dayan hapo mwisho kweli umeghadhabika,sijawahi kuona ukifuka moshi kihivyo..hahaa..
Ukweli Unazi wa Makinda na Ndugai utatia kichefuchefu. Jaribu kupitia magazeti ya kenya uone uwajibikaji wa Bunge na taasisi zake under new constitution dispensation..Hadi wameweka wazi Wananchi watoe maoni juu ya Viwango vya mishahara vya Rais,makam, na mawaziri..Natamani kenya ile iwe tanzania..pamoja na udhaifu wao wa ukabila,but the fox are inspiring for real!
 
Last edited by a moderator:
Nilisoma na TUNDU LISSU UDSM ingawa tulikuwa faculty tofauti lakini hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui kwa ubishi na kuzungumza sana inapojitokeza migomo chuoni, yeye alikuwa mbele kupambana na utawala wa chuo na serikali.

Anachofanya TUNDU LISSU ndio tabia yake hasa kwa ambao tunamjua muda mrefu, anapobisha haijalishi yuko sahihi au la ubishi wake uko kwa kile anachokiamini.

Kama TUNDU LISSU hakubadilika akiwa mdogo sina hakika kama atabadilika ukubwani. HUYU bwana amepata misukosuko mingi sana katika maisha kutokana na misimamo mikali lakini haijasaidia kumrekebisha tabia.

Mama Spika anatakiwa kutafuta mbinu tofauti na ambazo zimekwishatumika tangu akiwa mtoto kumthibiti bila mafanikio. Akitumia kanuni za kibunge kumthibiti atamuweza kwani ni mwanasheria mwenye kipaji na akili sana wanaomjua wamewahi kumuona akijenga hoja mahakamani ni TUNDU aliyeongoza kwa mabishano ya kisheria. kafanya kazi pale Mahakama Kuu kwa muda mrefu.
 
nasikia mama ni mwasibu(accountant)na Tundu Lisu ni mwanasheria.Lisu katika tasnia ya sheria amefanya mengi sana kabla ya kuwa mbunge,ata serikali ilishawai kumtumia kwenye kesi ya city water ambayo baadaye tulishinda kwenye mahakama ya kimataifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…