Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.


Ahsante sana ndugu Pasco,

Nilijua wewe ni mwandishi mkongwe na Mchambuzi, pia Mtambuzi wa mambo ya kisiasa. Kwa hiyo nilitegemea utanijibu kisayansi zaidi na kwa uchambuzi wa kutosha kuonesha tu si kwamba CCM itashinda 2015 bali itatawala milele kama ulivyosema kwenye ile post yako ya nyuma.

Unayoyasema ni kama yale yale ambayo mgombea wako EL aliwahi kuwambia wanataaluma wa SUA mwaka1996, kuwa CCM itatawala milele.... Sina hakika kama naye takuwa bado na mtazamo ule ule ukizingitia jitihada zake zinazidi kuzama gizani...

Kwa hiyo, naomba kama hutajali, utusaidie sie ambao labda tuna euphoria ya mabadiliko, kwa kutupatia uchambuzi wenye emperical evidence kwa nini CCM itashida 2015 na pia itatawala milele. Uliyoyasema kwenye post yako bado yako circumstancial kiasi kiasi kwamba yanakosa hoja za kuridhisha.

Ahsante sana!
 
Last edited by a moderator:
ulichonifurahisha tu kwenye hiyo post yako ni kunikumbusha umenyeni tu
 
ngoja tuone maamuzi yatatokaje. kuna watu huwa wanapenda kujitoa akili, wanapenda kujifanya hamnazo, lakini tunawaambiaje, safari hii mpaka watashika akili. haiwezekani watz tuchezewe na kundi dogo la watu wachache waroho mpaka wameshikwa na pepo la uroho, na ndilo linalowaondoa akili. sasa wasikilize vizuri mtapungwa hayo mapepo ya uroho, ufisadi, wizi mpaka mjitambue, maana yamewakamateni ufahamu, kila upuuzi mnaofanya mnauona kama ni jambo la kawaida.
 


Asante sana kaka Pasco,
maelezo na story nzuri sana
naona Mzee Mohamed Said keshakufundisha aina ya uandishi wake,
 
Makinda si mwalimu nadhani alisomea ukarani wa mahesabu kule Mzumbe. Walimu wana uelewa mpana eti, si kama hilo kinda
 
Asante sana kaka Pasco,
maelezo na story nzuri sana
naona Mzee Mohamed Said keshakufundisha aina ya uandishi wake,
Asante , katika fasihi simulizi Mzee Mohamed Said
ni Maalim wa ukweli , tatizo lake ni moja tuu -sumu ya udini aliyofanikiwa Sana kuipandikiza, soon tutashuhudia ikimea na wakati wa mavuno ukifika patakuwa hapatoshi!.
P.
 
Mkuu watu8 kwa bahati mbaya sana (refer Speaker's cv) huyu mama hata sio mwalim kitaaluma ila tu uwezo wake wa kutafsiri sheria ni mdogo sana sana, hana tofauti kwa uwezo wa kufikiri na Livingistone Lusinde (Mbunge wa Mtera) a.k.a Mzee wa matusi au kibajaji.
 
Asante , katika fasihi simulizi Mzee Mohamed Said
ni Maalim wa ukweli , tatizo lake ni moja tuu -sumu ya udini aliyofanikiwa Sana kuipandikiza, soon tutashuhudia ikimea na wakati wa mavuno ukifika patakuwa hapatoshi!.
P.

Hilo liko wazi Mkuu, na ubovu ndio hakuna mtu wa kulikemea hilo kwani kila mtu ana interest na hilo
 
Hii thread imewavua nguo bibi Makinda na ******! Ni juu yao kuchutama au kuning'iniza machenza na machungwa!
 
tunahitaji akina tundulisu kama 20 pale bungeni japo kwa mustakabali wa taifa
 

Umenikumbusha mbali, enzi za Bino (Bichwa, Binaisa) na Second master Mzava na "eh bwan mzee" mwalimu Juma....
 

Wanabodi, hii post naitumia tuu kufanya reference ya kilichotokea jana, na the role of Tundu Lissu ili kuestablishi kama ni kweli kuna tatizo kwa wapinzani, au ni muendelezo wa ukandamizaji na uminywaji demokrasia unaofanywa na kiti, ukiongozwa na dikiteta JN?!.
Pasco.
 
Mkuu Pasco hapo namba 4, matamko na mapendekezo yamepamba moto kuleta "usawa wa jinsia" hapo 2015.
 
Hapa nafanya tuu rejea, Jumatatu nitamfutilia Tundu Lisu kwa karibu, ili kujua kama atamsumbua na Sitta kama alivyomsumbua Spika Makinda?.
Pasco
 
Hapa nafanya tuu rejea, Jumatatu nitamfutilia Tundu Lisu kwa karibu, ili kujua kama atamsumbua na Sitta kama alivyomsumbua Spika Makinda?.
Pasco

Sawa kabisa. Tunafuatilia kwa karibu
 
hapa nafanya tuu rejea, jumatatu nitamfutilia tundu lisu kwa karibu, ili kujua kama atamsumbua na sitta kama alivyomsumbua spika makinda?.
Pasco

uje na data za msingi kwani na mimi nitamfuatilia kwa makini sana huyu mbabe wa sheria.
Ukituzunguka kwa masilahi ya watu fulani nitakupnga tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…