Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,626
Mkuu Dark City,
nimeripoti chaguzi 4, hivyo ya 2015 itakuwa ni uchaguzi wa tano kuuripoti. CCM siku zote inashinda sio kwa sababu inapendwa sana, bali kwa mazoea tuu!, nimeisha andika makala zangu mbalimbali kwa nini 2015 ni CCM tena. Chadema itavuna wabunge wengi zaidi huku bara, CUF itapoteza baadhi ya majimbo. Mshindi wa jumla wa urais ataendela kuwa CCM!.
Chadema inayo nafasi ya kushinda kama itakubali "to do things right", kwa sasa kupitia M4C, Chadema, inafanya kazi nzuri, yaani "is doing the right thing!". Ili chapa kipya kiweze kuking'oa "chama kubwa", "chama kongwe", na kuingia Ikulu, "doing the right thing" peke yake hakutoshi!, it got to do "things right", kitu ambacho sikioni Chadema kufanya!, as a result watu wataendeleza mazoea!.
Zile umati za watu kwenye maandamano au kwenye mikutano, sio kura!, nimeisha waambia Chadema humu kwa nini hawatashinda urais 2015 na nini cha kufanya, lakini nimeishia kutukanwa tuu "wee gamba!", mimi nasisitiza kuendelea kusema ukweli no matter what. Let them call me what they may, ila ikifika 2015 mtayaono na baada ya hapo tutaanza kuelewana vizuri!.
Siasa ni kama barabara ndefu, mbovu na ya kona kona, milima, mabonde, mashimo na makorongo!, vyama ni kama magari, wanachama ndio abiria, na viongozi wa vyama ndio madereva!. Kuelekea 2015 ndio safari yenyewe. Kwa huku bara, mchuano ni kati ya CCM, (gari kongwe, injini kongwe chovu, lakini dereva mzoefu, aliyeisha izoea hiyo barabara, miaka nenda, miaka rudi, hivyo anajua aendesheje, wapi apunguze mwendo na wapi aende kasi, wapi kuna korongo wapi kuna bonde, wapi kuna konakali na wapi kuna mlima, etc,etc!) na Chadema (gari mpya na injini bomba ina nguvu kupita gari kongwe na inakwenda mbio kuliko ule mkweche ila ina dereva mpya ambaye hajui njia!, kazi ya dereva mpya ni kutimua mbio, na kuendesha kwa kasi ili awahi kufika!, kutokana na kutojua njia, japo anakwenda kasi zaidi, kwa kuipita gari kongwe kwa mbali, mara kibao hujikuta anapotea njia, hivyo kulazimika kurudi nyuma na kuendelea na safari!.
Kwenye hii scenario, huyu dereva mpya anayo nafasi ya kushinda, sio kwa kitimua mi mbio, bali endapo atakubali au kuwasikiliza baadhi ya abiria wake wazoefu ambao wameishaipita njio hiyo mara nyingi ndani ya ule mkweche, au kutusikiliza sisi watazamaji wa mchuono huo ambao sio abiria wa gari yoyote, ila tuko homo njiani kwa muda mrefu, tunapoona dereva mpya anakosea, huwa tunampungia ishara kuwa huko siko!, au kumpa ishara ya hatari ya mbele, lakini hasikilizi!. Yeye ni mwendo kasi wa mbio tuu huku akishangiliwa na umati wa abiria wake, kuwa aendeleze "mwendo mdundo!.
Safari ya kuelekea 2015 ndio hii inaendelea, sasa hivi tuko half way!, bado hakuna dalili za dereva mpya kujifunza, hebu tusubiri, nasikia kutafanyika zoezi la kubadilishana madereva baadae mwaka huu, hebu na tusubirie timu mpya tuone, hata ikirudi timu ile ile kama itaendelkeza uendeshaji ule ule, basi ni hakika bila mashaka yote, mshindi ataendelea kuwa yule yule, dereva bingwa mwenye ule mkweche!.
Pasco.
Ahsante sana ndugu Pasco,
Nilijua wewe ni mwandishi mkongwe na Mchambuzi, pia Mtambuzi wa mambo ya kisiasa. Kwa hiyo nilitegemea utanijibu kisayansi zaidi na kwa uchambuzi wa kutosha kuonesha tu si kwamba CCM itashinda 2015 bali itatawala milele kama ulivyosema kwenye ile post yako ya nyuma.
Unayoyasema ni kama yale yale ambayo mgombea wako EL aliwahi kuwambia wanataaluma wa SUA mwaka1996, kuwa CCM itatawala milele.... Sina hakika kama naye takuwa bado na mtazamo ule ule ukizingitia jitihada zake zinazidi kuzama gizani...
Kwa hiyo, naomba kama hutajali, utusaidie sie ambao labda tuna euphoria ya mabadiliko, kwa kutupatia uchambuzi wenye emperical evidence kwa nini CCM itashida 2015 na pia itatawala milele. Uliyoyasema kwenye post yako bado yako circumstancial kiasi kiasi kwamba yanakosa hoja za kuridhisha.
Ahsante sana!
Last edited by a moderator: