Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 65,136
- 91,917
=
SUNDAY, OCTOBER 15, 2017
Vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya zanufaisha utalii Tanzania
[http://www]
Kwa ufupi
Kwa sasa Kenya ipo katika kipindi cha vurugu za kisiasa, zikitawaliwa na maandamano tangu Mahakama ya Juu ifute uchaguzi wa Rais baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu.
By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz
Hali ya kisiasa nchini Kenya imegeuka neema kwa wadau wa utalii nchini ambao wanadai kuwa idadi ya watalii wanaoingia nchini, imeongezeka kutokana na baadhi yao kuahirisha safari zao nchini Kenya kwa sababu ya hofu ya usalama.

Umoja wa wapinzani, Nasa ambao ulifungua kesi hiyo umekataa kushiriki marudio ya uchaguzi na sasa wafuasi wake wanaendesha maandamano yanayosababisha mapambano na polisi.
Jana katika maonyesho ya siku tatu ya kimataifa ya utalii yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), baadhi ya wadau wa utalii na mawakala walisema idadi ya watalii imeongezeka kwasababu wanaogopa kwenda Kenya.
“Watalii wengi wanasema hupendelea kwenda Kenya kwa sababu ya miundombinu yao ni mizuri na unafuu wa gharama za utalii. Lakini sasa wanahofia usalama wao kutokana na hali ya kisiasa iliyopo,” alisema Francis Lohay, mkuu wa fedha wa kampuni ya Bougain Villea Safari Lodge.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kitalii ya Patamu Lodge, Raymond Massae alisema kwa sasa watalii hawapendelei kwenda Kenya, hivyo ni fursa kwa wadau wa ndani lakini Serikali inapaswa kuongeza utangazaji wa vivutio vya utalii na sio kutegemea anguko la wengine.