Vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya zanufaisha utalii Tanzania

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Posts
65,136
Reaction score
91,917
=

SUNDAY, OCTOBER 15, 2017

Vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya zanufaisha utalii Tanzania

[http://www]

Kwa ufupi

Kwa sasa Kenya ipo katika kipindi cha vurugu za kisiasa, zikitawaliwa na maandamano tangu Mahakama ya Juu ifute uchaguzi wa Rais baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu.

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz

Hali ya kisiasa nchini Kenya imegeuka neema kwa wadau wa utalii nchini ambao wanadai kuwa idadi ya watalii wanaoingia nchini, imeongezeka kutokana na baadhi yao kuahirisha safari zao nchini Kenya kwa sababu ya hofu ya usalama.

Umoja wa wapinzani, Nasa ambao ulifungua kesi hiyo umekataa kushiriki marudio ya uchaguzi na sasa wafuasi wake wanaendesha maandamano yanayosababisha mapambano na polisi.

Jana katika maonyesho ya siku tatu ya kimataifa ya utalii yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), baadhi ya wadau wa utalii na mawakala walisema idadi ya watalii imeongezeka kwasababu wanaogopa kwenda Kenya.

“Watalii wengi wanasema hupendelea kwenda Kenya kwa sababu ya miundombinu yao ni mizuri na unafuu wa gharama za utalii. Lakini sasa wanahofia usalama wao kutokana na hali ya kisiasa iliyopo,” alisema Francis Lohay, mkuu wa fedha wa kampuni ya Bougain Villea Safari Lodge.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kitalii ya Patamu Lodge, Raymond Massae alisema kwa sasa watalii hawapendelei kwenda Kenya, hivyo ni fursa kwa wadau wa ndani lakini Serikali inapaswa kuongeza utangazaji wa vivutio vya utalii na sio kutegemea anguko la wengine.

Mkuu Geza Ulole ,
Tanzania tuna tofauti kubwa sana na Wakenya; Hili linafahamika na kila binadamu mwenye akili timamu.
Lakini kwenye kufurahia vifo vya binadamu yeyote kisa sisi tunapata faida za kiuchumi nadhani siyo uungwana hata kidogo.
Wakenya wao ndiyo wana wana-tabia hii ya kutanguliza maslahi ya kiuchumi na kufanya Propaganda binadamu wenzao wanapoumia. Tafadhali mkuu, usiwaige katika hili utajikuta umejenga chuki isiyo na kifani.

Jambo la pili ambalo bandiko ulilolileta limekiacha ni kuangalia upande wa pili wa vurugu za Kenya.
Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi sana, hivyo inamaanisha kwamba uwekezaji na masoko vinakuwa pia.
Tanzania katika kuwekeza haitaenda mbali na nje ya Afrika Mashariki na kati: Maeneo ni Kenya, Congo na Burundi.

Hivyo basi,
Ukiangalia kwa upande wa pili wa shilingi machafuko katika nchi kama Kenya yanaweza kuwa na athari nyingi sana kwa Tanzania kuliko hata hizo faida ambazo tunazipata kwenye utalii. Bidhaa zetu kama Gesi, Vinywaji vya pombe na Nafaka ndiyo vinaanza kupata soko huko Kenya sasa sidhani kama tumeangalia pande zote za shilingi kwenye hii habari.
 
Kwenye mambo ya uchumi
Hapo hakuna kuangalia jirani wala ndugu
Tuchapalike maana hii nayo fursa
Ugomvi wa panzi ...
Wamechagua Copy ya USA wacha wakione
 
Kwa hili Mkuu tuwe waungwana kidogo. Tusifurahie yanayotokea Kenya. Hali hii inaweza kuikumba Taifa letu. Badilisha lugha kidogo Mkuu. Hata kusema Utalii wazidi Kukua/Kuimarika Tz. Biko Mkuu! Kenya tunawaombea sana Mungu awaepushe na kikombe hiki!
 
Statistics za kuonyesha kutoka LCD muhimu Geza ulole
 
Kwa hili Mkuu tuwe waungwana kidogo. Tusifurahie yanayotokea Kenya. Hali hii inaweza kuikumba Taifa letu. Badilisha lugha kidogo Mkuu. Hata kusema Utalii wazidi Kukua/Kuimarika Tz. Biko Mkuu! Kenya tunawaombea sana Mungu awaepushe na kikombe hiki!

Umenena vyema mkuu.
Afrika Mashariki hasahasa Tanzania ina mengi yanayoweza kuharibiwa na hizi vurugu za Kenya.
Uchumi wa Tanzania na Kenya haijafungumana kwenye shughuli za utalii tu.
 
Mkuu Geza Ulole ,
Tanzania tuna tofauti kubwa sana na Wakenya; Hili linafahamika na kila binadamu mwenye akili timamu.
Lakini kwenye kufurahia vifo vya binadamu yeyote kisa sisi tunapata faida za kiuchumi nadhani siyo uungwana hata kidogo.
Wakenya wao ndiyo wana wana-tabia hii ya kutanguliza maslahi ya kiuchumi na kufanya Propaganda binadamu wenzao wanapoumia. Tafadhali mkuu, usiwaige katika hili utajikuta umejenga chuki isiyo na kifani.

Jambo la pili ambalo bandiko ulilolileta limekiacha ni kuangalia upande wa pili wa vurugu za Kenya.
Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi sana, hivyo inamaanisha kwamba uwekezaji na masoko vinakuwa pia.
Tanzania katika kuwekeza haitaenda mbali na nje ya Afrika Mashariki na kati: Maeneo ni Kenya, Congo na Burundi.

Hivyo basi,
Ukiangalia kwa upande wa pili wa shilingi machafuko katika nchi kama Kenya yanaweza kuwa na athari nyingi sana kwa Tanzania kuliko hata hizo faida ambazo tunazipata kwenye utalii. Bidhaa zetu kama Gesi, Vinywaji vya pombe na Nafaka ndiyo vinaanza kupata soko huko Kenya sasa sidhani kama tumeangalia pande zote za shilingi kwenye hii habari.

Huo ungwana wenu mbona huwa hamzingatii wakati mnawachinja na kuwala albino, ni taifa gani dunia yote zaidi ya Tanzania linalofahamika kwa mauaji ya hao maskini walemavu wa ngozi, tatizo huwa mna unafiki mkubwa sana. Kuna baadhi yetu tunawafahamu nyie jinsi mlivyo hadi ndani.

Kitu ambacho huwa nafurahishwa na mleta mada, yeye hudhihirisha Utanzania halisi uliojificha wa roho zenu nyeusi bila unafiki. Mara nyingi unakuta Watanzania mna hulka ya kuamkuana na kuitana wakuu lakini ndani ya roho zenu mna majungu na machungu kupitiliza. Ni kawaida Mtanzania kukuchangamkia kwa salamu nyingi na vijimaneno, lakini ukiondoka tu, anaanza kuporomosha majungu dhidi yako.

Hivyo muache kupoteza muda eti mnamrekebisha mleta mada, yeye alishafanya maamuzi ya kutoishi kinafiki kama mlivyo, huwa anadhihirisha chuki zake zote na kuziweka wazi bila kumunya maneno wala kuremba.
 
Mm... hii ni hatari muone daktari. Unaaza kuwa kama wale watu wanaotembea barabarani wakiongea pekeyao.
 
Mipovu mtatiririka lakini hali halisi haitobadilika, ndivyo mlivyo na hadi mtu aishi na nyie ndio ataweza kuwashtukia.
 
Haha, sasa baba mimi nimetoa ushauri tuu. Usiseme hatuja kuambia.
 
Lakini hata wewe ni baadhi ya Watanzania wachache ambao huwa mpo wazi na hamfichi wivu na chuki zenu, mnadhihirisha Utanzania wenu bila unafiki.
Japo nina uhakika nje ya JF huwa unajificha nyuma ya huo uwongo mnaita ustaarabu, nina uhakika huko nje huwa unakenua na kuchangamkia watu huku ukionyesha mstaarabu sana na kutumia maneno kama 'naomba' wakati unanunua na pia kuwakaribisha watu waje mle chakula nao ilhali ndani ya moyo wako haumaniishi.

Juzi nilikua sehemu na Watanzania tunakula, sasa mmoja akawa kila anayemsalimia lazima pia anamkaribisha chakula, japo wote walikua wanashukuru asante na kwenda zao. Sasa nikamuuliza hivi unamaanisha? Maana chakula chenyewe kidogo, mwenyewe halipi bill, halafu anamkaribisha kila mtu, ikitokea amkaribishe mtu asiyejua utani au asiyejua huo unafiki wenu na akaribie waanze kula itakuaje? Chakula chenyewe kidogo, bill halipi yeye na ana njaa..... Hapo najua watakula pamoja huku akijifanya kucheka, lakini ndani ya moyo wake atachukia kishenzi....hehehehe nyie bana
 
Lakini si unajuwa vitabu vyote vya dini vinasema kutoa ni upendo, na sisi watanzania tunaishi kwa huo msemo kwamba kujitolea ni upendo kwa Mungu. Nafurahi sana nikikutana na wakenya walioishi Tanzania au kujichanganya na Watanzani, maana nimegunduwa wengi wanabadilika na kuwa na upendo miyoni mwao. Wengi wanakuwa na mtazamo tofauti sana wa kimaisha pindi wanapo rudi nyumbani Kenya. Hata wewe, hapa unaweka ligi tuu, lakini naamini kabisa, mtazamo wako wa maisha umesha badilika.
 
Kutoa ukimaanisha huo ni upendo, lakini sio unafiki kisa unaishi kwa mazoea. Yaani mpo automatic 'karibu chakula', eheee mnifanyie hivyo muone kama sitakaribia, siwezi kutania nitakaa tule wakati kimoyomoyo utachukia hadi basi.
 
Karibia tuu, nakuhakikishia hicho hicho kidogo mtagawana tuu. Tena kwa utamaduni wa makabila kama ya kisukuma na kinyamwezi, kila mgeni akiigia nasongewa ugali wake mpya. Na wala sio jambo la ajabu au kishangaza. Huo ndio utanzania wetu, wewe unauita unafiki, jamani tenda wema nenda zako usingoje shukrani.
 
=

SUNDAY, OCTOBER 15, 2017

Vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya zanufaisha utalii Tanzania

[http://www]

Kwa ufupi

Kwa sasa Kenya ipo katika kipindi cha vurugu za kisiasa, zikitawaliwa na maandamano tangu Mahakama ya Juu ifute uchaguzi wa Rais baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu.

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz

Hali ya kisiasa nchini Kenya imegeuka neema kwa wadau wa utalii nchini ambao wanadai kuwa idadi ya watalii wanaoingia nchini, imeongezeka kutokana na baadhi yao kuahirisha safari zao nchini Kenya kwa sababu ya hofu ya usalama.

Kwa sasa Kenya ipo katika kipindi cha vurugu za kisiasa, zikitawaliwa na maandamano tangu Mahakama ya Juu ifute uchaguzi wa Rais baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu.

Umoja wa wapinzani, Nasa ambao ulifungua kesi hiyo umekataa kushiriki marudio ya uchaguzi na sasa wafuasi wake wanaendesha maandamano yanayosababisha mapambano na polisi.

Jana katika maonyesho ya siku tatu ya kimataifa ya utalii yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), baadhi ya wadau wa utalii na mawakala walisema idadi ya watalii imeongezeka kwasababu wanaogopa kwenda Kenya.

“Watalii wengi wanasema hupendelea kwenda Kenya kwa sababu ya miundombinu yao ni mizuri na unafuu wa gharama za utalii. Lakini sasa wanahofia usalama wao kutokana na hali ya kisiasa iliyopo,” alisema Francis Lohay, mkuu wa fedha wa kampuni ya Bougain Villea Safari Lodge.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kitalii ya Patamu Lodge, Raymond Massae alisema kwa sasa watalii hawapendelei kwenda Kenya, hivyo ni fursa kwa wadau wa ndani lakini Serikali inapaswa kuongeza utangazaji wa vivutio vya utalii na sio kutegemea anguko la wengine.

Vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya zanufaisha utalii Tanzania

Mi niko coast, mabus ya watlii yanazidi kuingia tangu sunday

wp_ss_20171019_0002.png
wp_ss_20171019_0003.png
wp_ss_20171019_0004.png
wp_ss_20171019_0005.png
 
Karibia tuu, nakuhakikishia hicho hicho kidogo mtagawana tuu. Tena kwa utamaduni wa makabila kama ya kisukuma na kinyamwezi, kila mgeni akiigia nasongewa ugali wake mpya. Na wala sio jambo la ajabu au kishangaza. Huo ndio utanzania wetu, wewe unauita unafiki, jamani tenda wema nenda zako usingoje shukrani.

Unafiki tuu mjini mtu huna hela lofa tu halafu umeitiwa ofa kisha kwa njaa zako unakaribisha kila anayekukenulia meno, hebu nikaribishe uone kama hutachukia.
 
Lakini hata wewe ni baadhi ya Watanzania wachache ambao huwa mpo wazi na hamfichi wivu na chuki zenu, mnadhihirisha Utanzania wenu bila unafiki.
Japo nina uhakika nje ya JF huwa unajificha nyuma ya huo uwongo mnaita ustaarabu, nina uhakika huko nje huwa unakenua na kuchangamkia watu huku ukionyesha mstaarabu sana na kutumia maneno kama 'naomba' wakati unanunua na pia kuwakaribisha watu waje mle chakula nao ilhali ndani ya moyo wako haumaniishi.

Juzi nilikua sehemu na Watanzania tunakula, sasa mmoja akawa kila anayemsalimia lazima pia anamkaribisha chakula, japo wote walikua wanashukuru asante na kwenda zao. Sasa nikamuuliza hivi unamaanisha? Maana chakula chenyewe kidogo, mwenyewe halipi bill, halafu anamkaribisha kila mtu, ikitokea amkaribishe mtu asiyejua utani au asiyejua huo unafiki wenu na akaribie waanze kula itakuaje? Chakula chenyewe kidogo, bill halipi yeye na ana njaa..... Hapo najua watakula pamoja huku akijifanya kucheka, lakini ndani ya moyo wake atachukia kishenzi....hehehehe nyie bana
Hapo umegonga ndipo kabisaaa! Alafu kama ume notice, siku zote hao ndo watakua watu wa kwanza kuita watu wengine majina kama roho mbaya,mnafik,wivu....
Nakwambia siku zote ukiskia mtoto anaita watoto wenzake wachoyo, muangalie ile siku atakua na kitu utagundua kumbe yeye ndo mchoyo zaidi! Hata pia watu wazima wale hupenda kuongea na na kusambaza udaku, siku zote utkuta hawawezi maliza Lisaa kabla kumwita mtu mwengine 'mdaku'.... Watanzania ni type hio hio, mtu anakuchekea unafikiri uko poa, ukishageuza mgongo jamaa anageuka shetani nyuma yako
 
Mipovu mtatiririka lakini hali halisi haitobadilika, ndivyo mlivyo na hadi mtu aishi na nyie ndio ataweza kuwashtukia.
Watu wote walioishi bongo, wanatamani kurudi, wewe mwenyewe unapapenda bongo.
 
Back
Top Bottom