Vurugu zaibuka msiba wa watoto matajiri wa Arusha, mwandishi wa Ayo TV anyang'anywa camera

Vurugu zaibuka msiba wa watoto matajiri wa Arusha, mwandishi wa Ayo TV anyang'anywa camera

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Katika hali isiyo ya kawaida vurugu zimeibuka katika msiba wa watoto wawili wa matajiri jijini Arusha ambao walikuwa ni wachumba waliofariki ajalini jana ambapo zimepelekea mwandishi wa habari kutoka AyoTV kunyang’anywa camera.

Mbali na kunyang’anywa camera mwandishi huyo alinyang’anywa kadi (memory card)na kisha kuvunjwa na ndugu wa karibu akiwemo mdogo wa marehemu, Brighton Temu maarufu kama “Bonge “.

Vurugu hizo zimefuatia mara baada ya mwandishi huyo, Gedfrey Thomas kutinga msibani kwa marehemu, eneo la KwaMrefu majira ya saa 10:30 leo jioni kufuatilia tukio la kifo cha mtoto wa Tajiri Denso.

Taarifa zimeeleza kwamba mara baada ya mwandishi huyo kutinga msibani hapo akiwa ameshikilia camera yake mkononi ndipo kundi la vijana waliojitambulisha ndugu wa karibu akiwemo mtoto wa mfanyabiashara anayemiliki mgahawa wa Uzunguni City Park, Kevin Masuwa alimvamia na kutishia kumpiga mwandishi huyo.

Taarifa kutoka msibani zimeeleza kuwa kundi hilo la vijana wanaodaiwa kuwa katika hali ya ulevi ndipo lilimuamuru mwandishi huyo akabidhi camera na baada ya kuwakabidhi walichomoa kadi na kisha kuivunja na kisha wakamrejeshea camera yake.

Hatahivyo,taarifa zimedai kuwa mara baada ya vurugu hizo ndipo baba wa marehemu tajiri....maaarufu kama “Denso “ndipo alipomfuata mwandishi huyo na kumuuliza gharama za kadi hiyo ili amlipe lakini mwandishi huyo alikataa na kudai anahitaji kadi pekee.

Akihojiwa na waandishi wa habari Mwandishi huyo kwanza alilaani tukio hilo na kudai anawatambua vijana waliomfanyia fujo na kumyang’anya vifaa vyake vya kazi.

Mwandishi huyo alisema kwamba yeye alifika msibani hapo kufuatilia tukio la ajali lililopekea mauti ya kijana huyo kama Mwandishi na ghafla alipoingia ndani ya eneo la tukio alishangaa kuvamiwa na kundi la vijana mbalimbali.

“Mimi baada ya kufika msibani niliingia moja kwa moja eneo la tukio nikiwa nasogea ndani ghafla walitokea vijana ninaowatambua kwa sura wakaniamuru niwakabidhi camera nilipotaka kukataa walitishia kunipiga ndipo nikawakabidhi wakachomoa kadi na kisha kuivunja “alisema Mwandishi huyo

Hatahivyo,alisisitiza kuwa kitendo kilichofanyika sio cha uungwana na anajiandaa kutoa taarifa mbele ya jeshi la polisi mkoani Arusha.

WATOTO wawili wa Matajiri wakubwa katika jiji la Arusha,wanaodaiwa kuwa ni wachumba , Estomi Temu na mpenzi wake Nice Mawala(24)Mkazi wa Njiro walifariki dunia jana kwa ajali mbaya eneo la kwa Mrefu katika jiji la Arusha .

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ,ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 7 usiku katika eneo hilo wakati gari la kifahari walilokuwa wakitumia lilikuwa kwenye mwendo kasi.

Katika tukio hilo linalodaiwa walitoka Klabu. Nice alipasuka kifua na kuvunjika mkono wa kulia huku Estomi akiumia kwa ndani na kuvuja damu masikioni puani na mdomoni.

Watu mbalimbali wameendelea kufurika katika msiba huo ambao umeibua gumzo ambapo idadi kubwa ya magari ya kifahari imeibua gumzo kufuatia kupangana kuanzia nyumbani mpaka barabarani katika kituo cha KwaMrefu baada ya kukosekana eneo la maegesho.

Mwisho.

38E55C52-2D71-423A-B37C-37FDFD75276A.jpeg
5B276069-A529-4DAD-B064-FD891071224D.jpeg
 
Wachaga na vurugu ni kama ni kama makolo na umbumbumbu
Nimeshapiga wengi sana. Siku moja nilizua vurugu kwenye club maarufu inaitwa PICNIC...kwa nje nilikwidana na jamaa akaja na ndugu yake. Nikaamua kuanza kurusha makonde. Niliwapasua vibaya wachaga wale wanaojinasibisha na wamasai. Hamna kitu vijana wa arusha maneno mtupu!
 
kaka waziri naomna niambie kinachoendele hapo msibani na je taarifa ya jeshi la polisi imeshatoka kuhusu
Katika hali isiyo ya kawaida vurugu zimeibuka katika msiba wa watoto wawili wa matajiri jijini Arusha ambao walikuwa ni wachumba waliofariki ajalini jana ambapo zimepelekea mwandishi wa habari kutoka AyoTV kunyang’anywa camera...
kaka naomba niambie kinachoendelea hapo msibani na je taarifa ya polisi imeshatokah
 
Katika hali isiyo ya kawaida vurugu zimeibuka katika msiba wa watoto wawili wa matajiri jijini Arusha ambao walikuwa ni wachumba waliofariki ajalini jana ambapo zimepelekea mwandishi wa habari kutoka AyoTV kunyang’anywa camera...
Wiki chache zilizopita nilikwenda kwenye kifo kimoja cha utata pale Arumeru kuna bibi alifia kisimani nilipofika nataka anza coverage akaja ndugu mmoja wa marehemu akataka vifaa vyangu maswali mengi then wakanigomea asee watu wa Arusha wakorofi sana hususan kwenye mambo yao hawapendi publicity
 
Wiki chache zilizopita nilikwenda kwenye kifo kimoja cha utata pale Arumeru kuna bibi alifia kisimani nilipofika nataka anza coverage akaja ndugu mmoja wa marehemu akataka vifaa vyangu maswali mengi then wakanigomea asee watu wa Arusha wakorofi sana hususan kwenye mambo yao hawapendi publicity
Nawe ulifanya kitu cha kipuuzi, nani kakualika hapo? Huwezi fanya msiba ndio habari ya kutangaza unless umepata mwaliko rasmi,next time pls don't do that
 
Back
Top Bottom