Vurugu zaibuka msiba wa watoto matajiri wa Arusha, mwandishi wa Ayo TV anyang'anywa camera

Vurugu zaibuka msiba wa watoto matajiri wa Arusha, mwandishi wa Ayo TV anyang'anywa camera

Nimeshapiga wengi sana. Siku moja nilizua vurugu kwenye club maarufu inaitwa PICNIC...kwa nje nilikwidana na jamaa akaja na ndugu yake. Nikaamua kuanza kurusha makonde. Niliwapasua vibaya wachaga wale wanaojinasibisha na wamasai. Hamna kitu vijana wa arusha maneno mtupu!
Weee dubyasha funga domo lako

Ntakutoa lokuu weee. Sasa ivi

Let mambo yako ya kishwani hapa.

Tuna majozi tumepoteza masela ujue.

Kunguni wewe
 
Nimeshapiga wengi sana. Siku moja nilizua vurugu kwenye club maarufu inaitwa PICNIC...kwa nje nilikwidana na jamaa akaja na ndugu yake. Nikaamua kuanza kurusha makonde. Niliwapasua vibaya wachaga wale wanaojinasibisha na wamasai. Hamna kitu vijana wa arusha maneno mtupu!
Ulipiga wengi wapi wewe acha mbwembwe.
Hadi mke ulishachukuliwa na ukabaki kama zoba wa banana zorro😂😂😂
Screenshot_20220731-223515.png
 
Aliitwa na nani? Watu wako kwenye machungu jitu linakuja kurecord? Si akarecord mwenge? Angenaswa na vibao
😁Haya bana mrembo kwakuwa umesema wewe wacha nisikupinge, lakini nikukumbushe ,misiba ya Magufuli , Nyerere ,Mkapa nk hakukuitwa mtu ila huwa wandishi wanaenda, hata Mimi kwenye ukoo wetu Kila Mara akifa mtu mkubwa huwa tuna record

Nadhani hapo ingetumika tu busara hao vijana wangefuta Kama Kuna picha za msiba na wamuambie mwandishi amekosea

Kwa sisi wasukuma taratibu zetu, hao vijana wangepaswa kutandikwa viboko hapo hapo msibani
 
sasa huyo mwamba nae watu wako msibani anaenda na makamera yake,kama ripoti ya ajali si aende polisi au siku hizi utaratibu umebadilika.
Mtoa mada anataka kumtetea ndg mwandishi kwa sababu ni jamaa yake although ninachoendelea kujiuliza ni hiki, Godfrey alipewa (labda) mtonyo kuwa kuna story , naye bila kushtuka akakurupuka pasi kuacha kamera kwanza akajue what's going on.

Although siyo kila msiba ni wa kukimbilia kisa mwandishi HAPANA tuwe na adabu kwenye misiba ya watu iwe masikini au tajiri mtoa tips na bahasha!.
 
.

Katika hali isiyo ya kawaida vurugu zimeibuka katika msiba wa watoto wawili wa matajiri jijini Arusha ambao walikuwa ni wachumba waliofariki ajalini jana ambapo zimepelekea mwandishi wa habari kutoka AyoTV kunyang’anywa camera.


Mbali na kunyang’anywa camera mwandishi huyo alinyang’anywa kadi (memory card)na kisha kuvunjwa na ndugu wa karibu akiwemo mdogo wa marehemu,Brighton Temu maarufu kama “Bonge “.

Vurugu hizo zimefuatia mara baada ya mwandishi huyo,Gedfrey Thomas kutinga msiba
ni kwa marehemu, eneo la KwaMrefu majira ya saa 10:30 leo jioni kufuatilia tukio la kifo cha mtoto wa Tajiri Denso.

Taarifa zimeeleza kwamba mara baada ya mwandishi huyo kutinga msibani hapo akiwa ameshikilia camera yake mkononi ndipo kundi la vijana waliojitambulisha ndugu wa karibu akiwemo mtoto wa mfanyabiashara anayemiliki mgahawa wa Uzunguni City Park ,Kevin Masuwa alimvamia na kutishia kumpiga mwandishi huyo.

Taarifa kutoka msibani zimeeleza kuwa kundi hilo la vijana wanaodaiwa kuwa katika hali ya ulevi ndipo lilimuamuru mwandishi huyo akabidhi camera na baada ya kuwakabidhi walichomoa kadi na kisha kuivunja na kisha wakamrejeshea camera yake.

Hatahivyo,taarifa zimedai kuwa mara baada ya vurugu hizo ndipo baba wa marehemu tajiri....maaarufu kama “Denso “ndipo alipomfuata mwandishi huyo na kumuuliza gharama za kadi hiyo ili amlipe lakini mwandishi huyo alikataa na kudai anahitaji kadi pekee.

Akihojiwa na waandishi wa habari Mwandishi huyo kwanza alilaani tukio hilo na kudai anawatambua vijana waliomfanyia fujo na kumyang’anya vifaa vyake vya kazi.

Mwandishi huyo alisema kwamba yeye alifika msibani hapo kufuatilia tukio la ajali lililopekea mauti ya kijana huyo kama Mwandishi na ghafla alipoingia ndani ya eneo la tukio alishangaa kuvamiwa na kundi la vijana mbalimbali.

“Mimi baada ya kufika msibani niliingia moja kwa moja eneo la tukio nikiwa nasogea ndani ghafla walitokea vijana ninaowatambua kwa sura wakaniamuru niwakabidhi camera nilipotaka kukataa walitishia kunipiga ndipo nikawakabidhi wakachomoa kadi na kisha kuivunja “alisema Mwandishi huyo

Hatahivyo,alisisitiza kuwa kitendo kilichofanyika sio cha uungwana na anajiandaa kutoa taarifa mbele ya jeshi la polisi mkoani Arusha.


WATOTO wawili wa Matajiri wakubwa katika jiji la Arusha,wanaodaiwa kuwa ni wachumba , Estomi Temu na mpenzi wake Nice Mawala(24)Mkazi wa Njiro walifariki dunia jana kwa ajali mbaya eneo la kwa Mrefu katika jiji la Arusha .

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ,ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 7 usiku katika eneo hilo wakati gari la kifahari walilokuwa wakitumia lilikuwa kwenye mwendo kasi.

Katika tukio hilo linalodaiwa walitoka Klabu ,Nice alipasuka kifua na kuvunjika mkono wa kulia huku Estomi akiumia kwa ndani na kuvuja damu masikioni puani na mdomoni.

Watu mbalimbali wameendelea kufurika katika msiba huo ambao umeibua gumzo ambapo idadi kubwa ya magari ya kifahari imeibua gumzo kufuatia kupangana kuanzia nyumbani mpaka barabarani katika kituo cha KwaMrefu baada ya kukosekana eneo la maegesho.


Mwisho.
Kuna kanuni za kiuandishi zilivunjwa ndio maana hayo yametokea kwa mwandishi tajwa, kwa tukio hilo Millard Ayo amekumbushwa kuacha mazoea kwenye fani yake ya habari afuate utaratibu tu.. hakuna matatizo kama hayo yatajitokeza tena.
 
Back
Top Bottom