Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Arusha huko kila familia bilioneaVijana wa Arusha vurugu ndio zao,
Ayo TV ni vimbelembeleTatizo ni watoto wa kitajiri. Mbona misiba ya Kiwalani simuoni huyo Millard ayo akienda kuirekodi[emoji23][emoji23][emoji23]
Wapuz sanaWanataka zile kiki za billionea wa Arusha
Mwandishi kwenye msiba wa familia anatafuta nini wakati hajaalikwa! Waandishi wajifunze kuheshimu faragha za watu binafsi, alitakiwa aombe ruhusa kabla ya kufika hapo, kisingizio cha walikuwa wamelewa ni cha kijinga na kitoto kwani wao wapo nyumbani kwao na pombe alizozifuata msibani hakuwanunulia yeye. Kuhusu kufidiwa kadi ni hisani tu kwani yeye ndiye aliyevamia nyumbani kwa watu..
Katika hali isiyo ya kawaida vurugu zimeibuka katika msiba wa watoto wawili wa matajiri jijini Arusha ambao walikuwa ni wachumba waliofariki ajalini jana ambapo zimepelekea mwandishi wa habari kutoka AyoTV kunyang’anywa camera.
Mbali na kunyang’anywa camera mwandishi huyo alinyang’anywa kadi (memory card)na kisha kuvunjwa na ndugu wa karibu akiwemo mdogo wa marehemu,Brighton Temu maarufu kama “Bonge “.
Vurugu hizo zimefuatia mara baada ya mwandishi huyo,Gedfrey Thomas kutinga msiba
ni kwa marehemu, eneo la KwaMrefu majira ya saa 10:30 leo jioni kufuatilia tukio la kifo cha mtoto wa Tajiri Denso.
Taarifa zimeeleza kwamba mara baada ya mwandishi huyo kutinga msibani hapo akiwa ameshikilia camera yake mkononi ndipo kundi la vijana waliojitambulisha ndugu wa karibu akiwemo mtoto wa mfanyabiashara anayemiliki mgahawa wa Uzunguni City Park ,Kevin Masuwa alimvamia na kutishia kumpiga mwandishi huyo.
Taarifa kutoka msibani zimeeleza kuwa kundi hilo la vijana wanaodaiwa kuwa katika hali ya ulevi ndipo lilimuamuru mwandishi huyo akabidhi camera na baada ya kuwakabidhi walichomoa kadi na kisha kuivunja na kisha wakamrejeshea camera yake.
Hatahivyo,taarifa zimedai kuwa mara baada ya vurugu hizo ndipo baba wa marehemu tajiri....maaarufu kama “Denso “ndipo alipomfuata mwandishi huyo na kumuuliza gharama za kadi hiyo ili amlipe lakini mwandishi huyo alikataa na kudai anahitaji kadi pekee.
Akihojiwa na waandishi wa habari Mwandishi huyo kwanza alilaani tukio hilo na kudai anawatambua vijana waliomfanyia fujo na kumyang’anya vifaa vyake vya kazi.
Mwandishi huyo alisema kwamba yeye alifika msibani hapo kufuatilia tukio la ajali lililopekea mauti ya kijana huyo kama Mwandishi na ghafla alipoingia ndani ya eneo la tukio alishangaa kuvamiwa na kundi la vijana mbalimbali.
“Mimi baada ya kufika msibani niliingia moja kwa moja eneo la tukio nikiwa nasogea ndani ghafla walitokea vijana ninaowatambua kwa sura wakaniamuru niwakabidhi camera nilipotaka kukataa walitishia kunipiga ndipo nikawakabidhi wakachomoa kadi na kisha kuivunja “alisema Mwandishi huyo
Hatahivyo,alisisitiza kuwa kitendo kilichofanyika sio cha uungwana na anajiandaa kutoa taarifa mbele ya jeshi la polisi mkoani Arusha.
WATOTO wawili wa Matajiri wakubwa katika jiji la Arusha,wanaodaiwa kuwa ni wachumba , Estomi Temu na mpenzi wake Nice Mawala(24)Mkazi wa Njiro walifariki dunia jana kwa ajali mbaya eneo la kwa Mrefu katika jiji la Arusha .
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ,ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 7 usiku katika eneo hilo wakati gari la kifahari walilokuwa wakitumia lilikuwa kwenye mwendo kasi.
Katika tukio hilo linalodaiwa walitoka Klabu ,Nice alipasuka kifua na kuvunjika mkono wa kulia huku Estomi akiumia kwa ndani na kuvuja damu masikioni puani na mdomoni.
Watu mbalimbali wameendelea kufurika katika msiba huo ambao umeibua gumzo ambapo idadi kubwa ya magari ya kifahari imeibua gumzo kufuatia kupangana kuanzia nyumbani mpaka barabarani katika kituo cha KwaMrefu baada ya kukosekana eneo la maegesho.
Mwisho.
Sema ulifuata pombe na misosi, covareji ya nini nyumbani kwa watu, muue bibi yako kisha ufanye cavareji, mbona misiba mingi ya uji na maharage hamuendi kufanya hizo cavareji?Wiki chache zilizopita nilikwenda kwenye kifo kimoja cha utata pale Arumeru kuna bibi alifia kisimani nilipofika nataka anza coverage akaja ndugu mmoja wa marehemu akataka vifaa vyangu maswali mengi then wakanigomea asee watu wa Arusha wakorofi sana hususan kwenye mambo yao hawapendi publicity
Mimi naona kama kuna taarifa zinafichwa,kwanza ajali haijaripotiwaWapuz sana
Viherehere sana...mtu kumiliki mgahawa bilionea [emoji1]
Washobokeaji sana hawa f kbs
Ova
Ilikuwa lini? Hebu njoo tena hata weekend hiiNimeshapiga wengi sana. Siku moja nilizua vurugu kwenye club maarufu inaitwa PICNIC...kwa nje nilikwidana na jamaa akaja na ndugu yake. Nikaamua kuanza kurusha makonde. Niliwapasua vibaya wachaga wale wanaojinasibisha na wamasai. Hamna kitu vijana wa arusha maneno mtupu!
Wanafuata pombe, kwa Ndesamburo kule Moshi wiki nzima wanashinda nyumbani kwake wakinywa na kula na vikamera vyao mikononiDah kuna watu huwa hawapendi kuweka misiba yao public...waandishi ombeni ukubali wa ndugu wa marehemu kabla ya kufika kwenye makazi ya watu na makamera yenu
🤣🤣🤣🤣Wanafuata pombe, kwa Ndesamburo kule Moshi wiki nzima wanashinda nyumbani kwake wakinywa na kula na vikamera vyao mikononi
Kuna watu wengine wanapenda faragha...msiba usiwe kama wana shoot bongo movieMimi naona kama kuna taarifa zinafichwa,kwanza ajali haijaripotiwa
na jeshi la polisi,pili familia kuteketeza memory card ya mwandishi,tatu kama kuna watu wengine wamejeruhiwa katika ajali hiyo na hawana wa kuwasemea,hapo taarifa za mwandishi huviamsha vyombo vingine kuchukua hatua.
Neno kuntu kabisa hili mkuu, life styles zinatofautiana kati ya familia moja na nyingine.Dah kuna watu huwa hawapendi kuweka misiba yao public...waandishi ombeni ukubali wa ndugu wa marehemu kabla ya kufika kwenye makazi ya watu na makamera yenu
Privacy!Dah kuna watu huwa hawapendi kuweka misiba yao public...waandishi ombeni ukubali wa ndugu wa marehemu kabla ya kufika kwenye makazi ya watu na makamera yenu
sio misiba tu, hata mambo binafsi kama mwandishi ukinifuata kuniuliz lazima nikutoe mbioDah kuna watu huwa hawapendi kuweka misiba yao public...waandishi ombeni ukubali wa ndugu wa marehemu kabla ya kufika kwenye makazi ya watu na makamera yenu