Kuna sababu mbalimbali zinazochangia maambukizi ya VVU kuwa makubwa katika mikoa ya Njombe na Iringa. Sababu hizo ni kama ifuatavyo
1. Idadi kubwa ya wafanyakazi wa kazi za ndani Wasichana wengi wamekuwa wakitoka katika hiyo mikoa kuja kufanya kazi za ndani na hawa wamekuwa wahanga wa ngono kutoka kwa mabosi wao. Wengi wamekuwa wakiambukizwa HIV na kisha kurudi kwao ambako wamechangia kuambukiza watu wengine
2. Kuoa wajane. Hii ni mila ya kawaida miongoni mwa hawa watu ambao wamekuwa wakirithi wake wa ndugu zao.
3.Ukaribu na nchi za kusini husani Afrika Kusini. Ukiona serotype ya HIV inayoathiri watu wa mikoa hiyo ni tofauti na aina za maeneo mengine isipokuwa nchi za Afrika Kusini. Inaaminika serotype hiyo imetoka huko na kuathiri watu wa mikoa hiyo. Aina hiyo ya virusi iko katili kidogo kuliko virusi wengine. Subtype C iko Afrika Kusini na maeneo ya Afrika Mashariki ni A na D .
4. Pia mikoa hiyo kuwa katika maeneo ya mpakani, kuwa na centre na route nzuri za biashara kumechangia maambukizi kuwa juu. Nchi kama Uganda walifanikiwa kupunguza maambukizi kutokana na kuongeza matumizi ya kondom na kupunguza mapenzi miongoni mwa wasichana wadogo.