Kuhusu ARV pia ninaona wagonjwa wa homa ya ini wanapewa, wanasema kwa sababu nao wana virus HCV or HBV, sasa wakamwambia mgonjwa asubiri virus (viral load iwe zaidi ya 1000 , ila jamaa akanifuata akaniambia hilo swala mwaka jana ila kwa kipindi hicho viral load walivyompima ilikuwa 935, nikampa ushauri wa chakula cha kumpa mgonjwa, ila mwanzoni sikujua kama watatekeleza basi wakaenda kumpa mgonjwa, na mgonjwa alitumia kwa takribani kama miezi minne na baadaye mwezi november wakaenda kupima hapo Muh...... hospitali ili waone sasa wameshafikia kiwango walichokisubiri ili wampe ARV, wakakuta viral load imeshuka mpaka 224 , na madaktari wakamwambia endelea kutumia njia unayotumia, na wakamwambia aje kupima tena baada ya miezi mitatu waangalie kitakachotokea, cha kusikitisha mgonjwa alipoona mambo yameonyesha matokeo mazuri anaanza kuvunja masharti ya lishe/chakula nilichomshauri.
Ndio hali ilivyo hata kwa watu waliowengi hawamalizi dozi matokeo yake matatizo yanakuwa makubwa baadaye.
Ushauri wangu, unapoanza dozi, basi umalize dozi isiachie njiani kwa kuona inafanya kazi na ukadharau ugonjwa.