VX-V8 (Toyota) milioni 250 mpya, MRI 1 Milioni 600 (mpya)

Kiazi Kitamu

Senior Member
Joined
Feb 16, 2013
Posts
122
Reaction score
126
VX-V8 (Toyota) milioni 250 mpya, MRI 1 Milioni 600(mpya). Ila VX - V8 ziko kama 300 ila MRI machine hazifiki 20 nchi nzima.

Tambua hizi zinatumiwa na Viongozi wote wakuu wa nchi hii, kuanzia Baraza la Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Wakurugenzi wa Wizara zote za Serikali, Wakuu wa Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya, Majaji etc

Niko na beberu mmoja ananiambia tuna akili. Nimemuambia niongezee K-Vant kubwa nimpe majibu
 
Sio jukwaa sahihi, magari hayafanyi kampeni

α΄Έα΅‰α΅α΅‰βΏα΅ˆα΅ƒΚ³ΚΈ [emoji377]
Soma uelewe, hili ni jukwaa la siasa unataka apeleke wapi? Wanasiasa viongozi wanatakiwa wasiwe mbali kimaisha na wananchi wao.
 
Wakifariki majeneza na makaburi yao pia yanakuwa ya vx-v8 na MRI-1? Naomba unijuze.
Unatakiwa ujue kwanza alivyosema MRI-1 anamaanisha nini, sio kwamba MRI-1 ni aina ya gari anamaanisha mashine ile inayotumika hospitalini inaitwa Magnetic resonance imaging.

Mtoa mada aweke sawa kuna watu watachangia bila kuelewa
 
Hiyo bei ya MRI ni kwa used au mpya? Sidhani kama MRI mpya ina bei ndogo hivyo, unless ni brands ndogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…