VX-V8 (Toyota) milioni 250 mpya, MRI 1 Milioni 600 (mpya)

VX-V8 (Toyota) milioni 250 mpya, MRI 1 Milioni 600 (mpya)

Hauko serious mkuu,kwahiyo hizo gari ndio zikafanye kazi ya kuwahudumia wananchi wa vijijni,unazijua vizuri barabara za vijijini lakini...?
Kwani hakuna watu wenye hayo magari vijijini na wanasurvive?
Halafu huduma gani wanatoa vijijini hao
Wanaotoa huduma ni mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kata, waalimu,bwana kilimo, madaktari nk ambao hata hayo magari hawana.
 
Akili kubwa ya wp gari za serekali hazilipiwi kodi ya kuingiza .....
na wanaponunua nyingi hupewa discount....
nyinyi watu mbona mpo nyuma sana
Sasa kwanini wasinunue MRI-1 nyingi instead ili wapewe discount
Kwani MRI-1 zinalipiwa kodi?
 
Kipindi cha mwalimu zilitumika landrover 109, baadaye zikaja pajero, landrover 110. Sina uhakika kama wapo tayari kurudi kutumia landrover 109 ili wabane matumizi.
Tena hali ya barabara ilikuwa mbaya mara 100 kuliko hivi sasa lakini viongozi wa kipindi cha Mwalimu walipiga kazi kwelikweli
Walitembelea mashamba ya mkonge, kahawa, korosho, tumbaku, Pamba na kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa vitendo
Waliweka kando ubinafsi.

Hawa viongozi wa sasa wakishavimbiwa tozo wanatuuliza kama wakulima tunaijua V8
 
Back
Top Bottom