VX-V8 (Toyota) milioni 250 mpya, MRI 1 Milioni 600 (mpya)

Mkuu hiyo idadi ya v8 kuwa zipo 300 nchi nzima mbona kidogo sana..
Zinaweza zidi hata 1000
 
Mtu unalimpa mshahara mkubwa tu still unampa Gari na mafuta juu na Posho kede kede Mimi kwa hili hapana Kwa kweli kuna kila sababu ya izi macho ya panzi zitolewe kwa baadhi ya viongozi tu mana impact za hawa wawakilishi wetu wabunge ni ndogo sana kufafanisha na Expenditure zao wakitaka wajinununulie wenyewe.
 
Sijawahi ona mwanasiasa anakataa hizo V8..Ata mtoa mada ukipewa hiyo ngoma huwez kataa..it's a king of the road.. unakula lami, unakula vumbi, unavuka mto..
 
Wewe liongo, VX-V8 ni mil 300 (approx.).
 
Dawa ni kuondoa V8 zote zibaki kwa rais tu. Wengine wote watumie public au magari yao kama wafanyakazi wale wa kawaida. Kila mtu aone umuhimu wa public transport
 
V8 VX-R je?.ni sh ngapi
 
Kipindi cha mwalimu zilitumika landrover 109, baadaye zikaja pajero, landrover 110. Sina uhakika kama wapo tayari kurudi kutumia landrover 109 ili wabane matumizi.
 
Ni zaidi ya hizo hapo ujapiga running cost si chini ya milioni 6 kwa mwezi kulihudumia moja.Ni hospital ngapi,shule ngapi,vyuo vingapi,miradi mingapi ya umwagiliaji hapo.Hao ni watumishi Kama wengine wapandao daladala pia wote hao wanauwezo binafsi wa kununua private car.Pia si watendaji kazi ufanywa na wapanda daladala.Sisi waafrika tutaendelea walaumu wazungu juu ya kushindwa kwetu kuwa na mipango sahihi ya maendeleo.
Hata aliyejiita mzalendo mtetezi wa wanyonge kaangukia kulekule kula jasho la wanyonge.
 
Kipindi cha mwalimu zilitumika landrover 109, baadaye zikaja pajero, landrover 110. Sina uhakika kama wapo tayari kurudi kutumia landrover 109 ili wabane matumizi.
Wapande daladala Kama watumishi wengine
 
Hauko serious mkuu,kwahiyo hizo gari ndio zikafanye kazi ya kuwahudumia wananchi wa vijijni,unazijua vizuri barabara za vijijini lakini...?
Eti kuhudumia vijijini Nani kakwambia wanaenda vijijini
 
Kipaumbele namba Moja Cha mwanasiasa ni yeye mwenyewe Kisha familia yake.

Haijalishi Yuko upinzani au tawala.

Sasa nyingi walalahoi kwakuwa hamjielewi mtawasifia weeeee kuwapamba

Wenzenu wanawacheki jinsi mlivyo wapumbavu wa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…