Kwani hakuna watu wenye hayo magari vijijini na wanasurvive?
Halafu huduma gani wanatoa vijijini hao
Wanaotoa huduma ni mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kata, waalimu,bwana kilimo, madaktari nk ambao hata hayo magari hawana.
Kipindi cha mwalimu zilitumika landrover 109, baadaye zikaja pajero, landrover 110. Sina uhakika kama wapo tayari kurudi kutumia landrover 109 ili wabane matumizi.
Tena hali ya barabara ilikuwa mbaya mara 100 kuliko hivi sasa lakini viongozi wa kipindi cha Mwalimu walipiga kazi kwelikweli
Walitembelea mashamba ya mkonge, kahawa, korosho, tumbaku, Pamba na kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa vitendo
Waliweka kando ubinafsi.
Hawa viongozi wa sasa wakishavimbiwa tozo wanatuuliza kama wakulima tunaijua V8