Vyakula ambavyo haviruhusiwi kutumiwa na binadamu

Vyakula ambavyo haviruhusiwi kutumiwa na binadamu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Wapendwa tupitie sehemu ya maandiko kuhusu vyakula visivyofaa kutumiwa na mwanadamu!
Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia. Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia,
,**Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.
1.Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.
2.Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato;
*Ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.

*Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.

*Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.

*Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu, na mwewe, na kozi kwa aina zake, na kila kunguru kwa aina zake;

*Na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake, na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa, na mumbi, na mwari, na mderi, na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo.

*Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake.

*Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu.
* Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi.

*Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.
*Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zao na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi.
Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni.
(Mambo ya Walawi 11:01-31)
Karibuni kwa michsngo au maoni
 
Jamani hv zile zilizopo salanda ni kuku kweli..?
Mi nahisi itakua vilanyoka, bwana afya, mwewe. Lakini ukiwalita wanasema ni kuku. Kuku gani analingana na mbuzi
 
Unaweza ukanipa uhusiano wowote wa kimantiki (logical corelation) kati ya 'mnyama kutocheua' na mnyama kuwa 'najisi'? Either ki-imani, kisayansi au hata kwa logical thinking tu..;
Kwamba iliandikwa kwenye vitabu haimaanishi tusijiulize maswali au kuhoji..
 
Unaweza ukanipa uhusiano wowote wa kimantiki (logical corelation) kati ya 'mnyama kutocheua' na mnyama kuwa 'najisi'? Either ki-imani, kisayansi au hata kwa logical thinking tu..;
Kwamba iliandikwa kwenye vitabu haimaanishi tusijiulize maswali au kuhoji..
Kisayansi samaki wasio na magamba ni kundi la walao uchafu!
 
Nguruwe na Ngamia wasiliwe.....
Nguruwe analiwa kama dawa.ukikutana na MTU yeyote mwenye majini mwambie ale kitimoto yatafunga virago yenyewe.Wachaga wanakula sana kitimoto ndio maana hufanikiwa kibiashara biashara zao hazilogeki hata wafungue maeneo ya wafuga majini.Majini ukisoma Biblia yalikuwa kwa mgerasi yesu akayaamuru yawaingie nguruwe kwa kuwa alijua nguruwe ni kiboko cha majini na wanajua namna ya kuyashughulikia.Nguruwe wakabeba Yale majini wakaenda kuyamwaga baharini.Kula kitimoto kama unataka uogopwe na majini ni tiba
 
Hizo zilipwenda tangu mussa na harouñ hata kama kweli sheria hiyo ilikuwepo enzi hizi za umati wa mtume muhammad (saw,) hazifanyi kazi
 
Watoto wa mama mdogo mbona wao wanakula ngamia ila watoto wa mama mkubwa wakila kitimoto wanaambiwa haramu?? Nadhani haramu ndio tamu siku zote
 
Wachina wanakula kitu.Manyema wanakula watu,panya,punda na nyoka mbele kwa mbele.Hizo zimepitwa na wakati ni enzi za Biblia na Israel !
 
Kwahyo kisayansi kuna madhara ukiwala!?...Hilo ni agano la kale lilishatenguliwa sasa hivi hata kunguni ukiweza we kula tu!..kikutokacho ndio najisi!
Hakuje kutengua torati
 
Unaweza ukanipa uhusiano wowote wa kimantiki (logical corelation) kati ya 'mnyama kutocheua' na mnyama kuwa 'najisi'? Either ki-imani, kisayansi au hata kwa logical thinking tu..;
Kwamba iliandikwa kwenye vitabu haimaanishi tusijiulize maswali au kuhoji..
ipi wazi sana angalia wote hao ni wachafu...kama sikosei nyama ya nguruwe na samaki wa matopeni wanaminyoo zaidi ya 6000
 
kitimoto.jpg


Hii ni spesho kwa Wateule wa Bwana, wasiofungwa na dhamira na sheria bali wakidodondozwa unono na Neema zitokazo kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom