Kwa Tanzania kufikiria kuanza kula wadudu ni kujitakia tu,labda tuwekeze kwa ajili ya mifugo.
Hii ndio nchi inaongoza kuwa na mifugo wengi baada ya Ethiopia,ng'ombe,mbuzi,kondoo,kuku,nk, kinachotakiwa ni kuweka mazingira mazuri tu na Sera ili nyama ipatikane kwa bei nzuri.
Bado tuna Samaki kwenye Bahari,Maziwa na mito ambapo uvuvi wake hatuumudu hata asilimia 10,na hata kwenye pato la taifa haufikishi hata asilimia 1,matokeo yake watu wanafanya shamba la bibi.
Bado kuna wanyama kama Sungura hawajapewa promo vya kutosha ili kila nyumba ianze kufuga kama Chakula maana hawa huzaliana kwa kasi kama panya,matokeo yake tunaanza kufikiria sijui mende na funza.
Bado tuna ndege wengi sana kama kwelea kwelea ambao husababisha majanga ya njaa kwa kuvamia mashamba na kula mazao,hao ndio wangetumika kama chakula ili wapungue.
Bado tuna Kanga,bata na wengine wengi ambao wapo porini huko ambapo sheria inaweza kurekebishwa wakawa wanazalishwa na kuuzwa nyumbani watu wafuge kwa ajili ya chakula na biashara.
Tukiendelea kusikiliza stories za wazungu tutasombwa na propaganda zao halafu tutasahau hata kwamba sisi tuna utajiri wa mifugo tunaopaswa kujivunia.