Jkt nilikutana na ugali mchungu sana ule unga ulikua umeharibika baada ya kukaa muda mrefu store wakaamua kutulisha sisi kuruta wa Mungu.
Siku za kwanza ulikua unatushinda sasa kambini ilikua kuna eneo limetengwa la kufugia nguruwe yale mabaki ya ugali yaliyotushinda wakawa wanapelekewa nguruwe lakini hata nguruwe nao walikataa kula
Mazoezi yalivyozidi kuwa makali ilibidi tule ule ugali mchungu bila kulazimishwa maana usipopiga msosi hutoboi, licha ya kuwa nguruwe walikataa ule ugali ila sisi tuliula na tulimaliza stock