Vyakula vipi umekula pindi umepigika vilivyo?

Vyakula vipi umekula pindi umepigika vilivyo?

Maji ya mchele huwa yananukia,na nyumba wakiyopika mchele harufu huwepo,angeshindwaje kujua kua haya ni maji ya mchele,mkuu...?
Mkuu, njaa isikie tu. Ikikukolea, hata chakula ambacho ulikuwa ukiisikia harufu yake unahisi kutapika, ukikutana nacho, unaweza usiisikie ile harufu iliyokuwa ikikukera, badala yake ikawa inanukia harufu ya chakula ukipendacho.
 
๐”๐ ๐š๐ฅ๐ข ๐ฆ๐ค๐ฎ๐›๐ฐ๐š,๐ง๐š ๐ฎ๐ ๐š๐ฅ๐ข ๐ฆ๐๐จ๐ ๐จ ๐ง๐๐ข๐จ ๐ฆ๐›๐จ๐ ๐š
 
Nilishawahi kula ugali na tomato ila ilikuwa ni kwasababu nilichelewa kutafuta chakula na nilikuwa mkoani( mbeya). Lile baridi lilijua kunifunza adabu ule usiku.

Maana sehemu nilipokuwa kutoka hadi kwenda town kulipochangamka ilikuwa mtihani na Mbeya unajua balaa lake usiku baridi kali la mwezi wa sita.

Hotpot ilikuwa na ugali wa mchana, aiseee niliruka nao na tomato ile njaa ilikuwa inauma hadi kwenye mifupa.
Nishakula ugali na sukari dadeki, kuna kipindi miaka hiyo andazi mmoja tunagwana wawili halafu kimyaaa hakuna kulalamika like nothing happened ....Mungu ashukuriwe Kwa kweli wanaJF
 
Kuna Siku tumeenda kufanya kazi Fulani ya Site

Hakukuwa na maduka jirani Wala mama ntilie

Hivyo alipita Mama mmoja anatoka shambani, alikuwa amebeba mizizi Fulani hivi(Inaitwa Ming'oko) kule mikoa ya Kusini.

Ndiyo mara ya kwanza nikala hiyo Ming'oko kuepusha njaa
 
Back
Top Bottom