GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
1. Mkate na maji. Hapo ni kipindi nikiwa Chuoni. Wenzangu walikuwa wakinipitia room kwangu tukale mghahawani, nilikuwa nikiwaambia nipo "busy". Wakishaondoka tu, nafunga mlango, nachukua mkate wangu "kabatini" na kikombe cha maji na kuanza kuubugia kwa haraka nisije nikakutwa. Kwanza, mkate wenyewe nilikuwa naula kwa bajeti ili usiishe kabla ya muda nilioupangia.
2. Katika harakati za utafutaji nikiwa mikoani, kuna kipindi mambo ya kifedha yaliniendea kombo. Kuna wakati nilikuwa nikinywa kikombe cha uji wa sh 300/= (wa kununua kwa mama lishe) mara moja kwa siku, saa moja Jioni hadi kesho yake tena saa moja Jioni ndiyo nije kuunywa mwingine, na kuna wakati nilishinda njaa na kulala njaa bila kula chochote, na kuna wakati nilijipikia uji mkavu - haukuwa na sukari wala limao, ni maji na unga tu, na mambo yakasonga mbele.
Hayo ni kwa uchache tu, lakini matukio ni mengi. Ndiyo maana wakasema"ukiliona dume la nyani limenenepa ujue limekwepa mishale mingi"