Vyakula vipi umekula pindi umepigika vilivyo?

Vyakula vipi umekula pindi umepigika vilivyo?

Juisi ya pilipili kichaa.Kulikuwa hakuna option yoyote zaidi ya kuzisaga tuu.
 
Thanks to God sijawahi fikia hiyo level ya njaa
 
Jkt nilikutana na ugali mchungu sana ule unga ulikua umeharibika baada ya kukaa muda mrefu store wakaamua kutulisha sisi kuruta wa Mungu.

Siku za kwanza ulikua unatushinda sasa kambini ilikua kuna eneo limetengwa la kufugia nguruwe yale mabaki ya ugali yaliyotushinda wakawa wanapelekewa nguruwe lakini hata nguruwe nao walikataa kula

Mazoezi yalivyozidi kuwa makali ilibidi tule ule ugali mchungu bila kulazimishwa maana usipopiga msosi hutoboi, licha ya kuwa nguruwe walikataa ule ugali ila sisi tuliula na tulimaliza stock
 
Katika mida ile ya kutafuta, inafikia hatua unakula ili uishi yaani unakula chochote. Mimi nishakula ugali na chumvi mixer maji ya kunywa.

Wewe je ?
Mimi nilikuwa nakula maembe mabichi na chumvi,,mapapai ,machungwa machanga nk.
Hata huo unga wa sembe nilikuwa nautafuta kwa tochi.

Nawashauri kwenye nyumba zenu mpande miti ya matunda .

Ni msaada mkubwa sn ukipigika kimaisha.
 
Niliwahi kula mihogo hadi ilifika hatua nikisikia harufu yake napata kichefuchefu. Hapo budget yangu kwa siku haikutakiwa kizidi buku na ikiwezekana iwe chini ya hapo. So chakula cha kujaza tumbo cha haraka na nafuu ilikua ni mihogo.
Mida ya saa tano napata mihogo ya mia tano na kachumbali nyingiiii pale Tabata TOT darajani pale kuna mama alikua anauza ananipa mitatu kwa jero. Halafu mida ya saa mbili napata tena hivyo na maji mengi nalala.
Ile hali iliendelea hadi ikafika hatua nikisikia harufu ya mihogo napatwa kichefuchefu, imebaki historia.
 
Nilikosa unga ,nikapika pumba za kuku na nikamla na kuku
La kupika pumba za kuku ulijitakia mkuu😃

Ungemwuza kuku ukanunua unga na mchicha alau.

Au ungemchemsha huyo kuku na maji mengi ili update mchuzi mwingi. Nyama inakuwa kama ugali na mchuzi kama mboga.
 
Back
Top Bottom