Vyama 11 vya Siasa vyalaani kauli za Tundu Lissu

Tundu Lisu sio mwanasiasa ni mhuni aliyeingia kwenye Siasa sababu mwanasiasa huwinda kura ziongezeke kutoka Kwa walio wengi sio wachache
Lisu hata kura chache huua Kwa Domo lake chafu

Watu wengi wa chini hawana shida na muungano yeye huungana na wachache viongozi wa Zanzibar wachache wapinga muungano halafu anategemea Chadema ipate kura nyingi Bara na visiwani.

Amsikilize Warioba hapa akiongelea Kwa hoja nzito kuhusu muungano

View: https://www.youtube.com/live/zsseT8GhlEg?si=Qtf1OiHirfSMKRZz
 
acheni ngonjera zenu. hoja za lisu zijibiwe kwa hoja siyo sarakasi.
TUNDU LISU NYAGHAAMBA.
AKISEMA NCHI INATIKISIKA HAHAHAHA
 
NDO UMESHAMJIBU LISU HAPO
hahaha kazi ipo
 

 
kukataliwa ni kitu mbaya sana wajemeni tena hadharani
 
You mean separate small branches za chama tawala?
 
Kulaani Kulaani kulaaani.. Hatukubaliani hatukubaliani hatukubaliani.. Mchochezi mchochezi mchochezi.. Anatukana anatukana anatukana.. Yani ni lopolopo tupu hakuna anaejibu hoja hata mmoja. Mwenyezi Mungu kwanini umetuumba nchi hii tuongozwe na wafia tumbo. Why God WHYYYYY
 
tAKATAKA TUPU HIZO
 
Mashina ya CCM hayo, mbona habari za "tutawapoteza" toka Bukoba hawakukemea.
 
haya si matakataka matawi ya CCM
 
Hivi vyama kwanini huwa havijitokezi kiongozi yeyote wa CCM akitoa kauli za kichochezi?
Kweli mkuu, mbona huwa hawajitokezi ccm wanapotoa kauli za kijinga?? Mfano;-
1. Asiyetaka tozo ahamie Burundi......Mwigulu.
2. Kila mbuzi hula kwa urefu wa kama a yake........Samia.
3. CCM tutatumia dola kubakia madarakani..... Bashiru akiwa Katibu mkuu wa CCM.
4. Safari hii, safari hii hatutatumia bunduki. Ni simdano tu, pyuuu!.
N.k.
5. Mkichagua chama kingine hapa hatuleti maji.....JPM.
6. Wakurugenzi unalipwa mshahara na ccm halafu umtangaze mpinzani? Inhiii!! .....JPM.
 
Tanzania tuna watu wengi sana na si lazima Warioba aongee ndiyo tujue kuna ukweli.Tuliosoma somo la Historia na Elimu ya Siasa tunamwelewa sana Tundu Lissu kwani anaongelea yale yote yaliyosahaulika na Awamu hii ya CCM.Umoja wetu utavurugwa na Viongozi wakuu wa Nchi pamoja na mapandikizi yao kwa kung'ang'ania Muungano ambao unaibeba nchi moja na kuidharau nyingine na wala si Tundu Lissu.
 
Yaani mpzka DP ya Marehemu Mtikila Mtetezi wa Tanganyika imeungana na vyana vya brief case. Hivi kama Mtikila angekuwa hai angeruhusu chama chake kitoe tamko dhidi ya jambo alilolipigania uhai wake wote?

Nikiwahi kusema humu Tanzania ina vyana vya siasa viwili tu CCM na CHADEMA basi; vingine ni
CCM B kazi yao ni moja tu kuipinga CHADEMA. Vyama ambavyo hata kuitisha mkutano Dar es salaam haviwezi eti vinaibuka kila CHADEMA inapokuwa na malumbano na CCM.

Halafu CHADEMA Ikikubaliwa na CCN kuhusu jambo fulani inalolipigania navyo vinang'ang'ania vijumuishwe katika jambo hilo hilo ingawa mwanzoni vilipinga.
Hivi kuna watanzania kabisa wanajiunga na waganga njaa hawa eti ni vyama vya siasa.
 
KUFUATIA Kauli za hivi karibuni za Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA -Tundu Lisu, Vyama 11 vya Siasa Zanzibar vimelaani vikali kauli hizo ambazo wanadai kuwa ni kauli za Kebehi na uchochezi zinazolenga kuleta ubaguzi kwa Watanzania kupitia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akitoa wasilisho la Pamoja la Viongozi wa Vyama 11 vya Siasa juu ya kauli hizo, Mwenyekiti wa Chama cha ADA TADEA Juma Ali Khatib amesema kauli zilizotolewa na Tundu Lissu ni kauli za kibaguzi ambapo wameziomba Mamlaka husika ikiwemo Msajili wa vyama vya siasa pamoja na vyombo vyengine kuangalia kwa makini hatua za kuchukua kwa kiongozi huyo na chama chake.

"Sisi Vyama 11 vya siasa hatuungi mkono kauli zako Tundu Lisu na tunazilaani, matamshi yako ya kibaguzi kwa kuonesha wazi wazi watu wa upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawana haki ya kufanya kazi upande mwingine na huu ni ubaguzi, uchochezi na kuonesha wazi wazi umefilisika kimawazo, kifikra na kisiasa na kutafuta Kiki za kisiasa,"amesema.

"Kwa msingi huu alioonesha Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ni dhahiri anawaambia wananchi kwamba yeye ni mbinafsi, mwenye uchu wa madaraka, mchonganishi, mfitinishaji na mwenye dhamira ovu kwa Muungano wetu," ameongeza.

"Tunavitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini, pamoja na msajili wa vyama vya siasa kufanya uchunguzi wa kina juu kauli anazozitoa ndugu Tundu Lissu kupitia kwenye majukwaa ya kisiasa kama ni za kwake au anatumwa na chama chake na ikithibitika Msajili wa vyama kisiasa achukuwe hatua kwa mujibu wa sheria kutokana kuwa kauli hizo zinalengo la kuligawa taifa letu," ameeleza

Vyama vilivyotoa tamko hilo ni ADA TADEA, CCK, NLD, Demokrasia Makini, NCCR- MAGEUZI, TLP, UPDP, SAU, UMD, NRA na Chama cha DP.
 
VYAMA VYOTE HIVYO NI MATAWI YA CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…