Uchaguzi 2020 Vyama pinzani badilikeni, uchaguzi ni matangazo wekeni picha za Wagombea wenu mitaani

Uchaguzi 2020 Vyama pinzani badilikeni, uchaguzi ni matangazo wekeni picha za Wagombea wenu mitaani

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini Vyama Pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani.

Hali hii inawafanya wananchi wengi kuona kama vile vyama pinzani haviko serious na havijajipanga kwa uchaguzi.

Achaneni na hiyo hoja kuwa eti mnazuiliwa kuweka mabango na mamlaka za jiji, wananchi wanajua huo ni uzushi hizi sehemu za mijini watu ni wasomi hawadanganyiki kirahisi namna hiyo.

Toeni fungu, tengenezeni mabango ya kampeni. Uchaguzi bila matangazo ni kujiandaa kushindwa na si kushinda.
 
Hata Mbeya ni hivyo hivyo lakini kuna haja gani kama wanafahamika mfano Sugu kwa Mbeya.
 
Wapiga kura wako majumbani wanausubiria tu hiyo tarehe 28/10 wakafanye jambo lao. Hayo mabango, ndege, flyovers, nk. Vyote hivyo havipigi kura.
Kama unafikiri mambo ni rahisi namna hiyo basi unajidanganya mkuu.
 
Nimekumbuka bango la Lowassa Ubungo mawasiliano.. bango la Lowassa Kariakoo sokoni...

Siku bango la Lowassa linafungwa sokoni Kariakoo ilikuwa shangwe Kariakoo yote mpaka unashangaa nini kimetokea.. Nikajibiwa bango la Rais linafungwa sokoni.
 
Kama TV, magazeti,Radio na online tv zimezuiwa kutokumtangaza mgombea wa upinzani na wananchi bado wanahudhuria na kupata taatifa zote kuhusu kampeni, sio kma hayo mabango ya ccm Nchi nzima Kama yatasaidia. Watu wa Sasa sio wa miaka ya 1970s' watu wanajitambua wanajua kinachoendelea wewe washauri ccm waongeze mpk mashuleni mahospitali.
 
Kuna vyama haviko serious na uchaguzi. Kuna majimbo hata hatujui nani anagombea na wagombea wapo. Vyama vijitahidi kutupasha Habari ukiangalia idadi ya wanaohudhuria mikutano na idadi ya watu waisohudhuria unaona inahitajika mbinu ya kuwafikia wapiga kura zaidi ya mikutano.

Yabandikwe mabango walau Watu waone, kwa wababozi wa masoko wataelewa kidogo naongelea nini.
 
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye Kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini vyama pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani...

Wanachaniwa kila siku
 
Mabongo ndo vitu gani mambo yakizamani sana hayo, sisi wananchi tunataka hela za tetemeko , simmeona leo Bukoba muhutu kakosa watu pamoja nakujaza mabango mji mzima.
Hapa ndio bukoba alipokosa watu
FB_IMG_1600184483246.jpg
FB_IMG_1600184473143.jpg


Wekeni matangazo acheni kudanganyana na ubishi usio na tija huku wenzenu wakizidi kuwafikia zaidi wananchi we unakuta watu hata mgombea udiwani wa kata yao hawamjui sa unategemea nini hapo?
 
Tunasubiri kwenye sanduku la kura. Mwendo ni mafiga 3, Rais, Mbunge na diwani. Mabango tumewaachia wanaofikiri mabango yanapiga kura😎😎😎
 
Mdada Akiwa mzuri haitaji make up wala kuvaa vizuri kiivyo ila akipita tu kila mtu atasema hii pisi kali. Kibaya chajitembeza mkuu
 
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini vyama pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani...
Maajabu ya dunia.

Maccm kutaka wapinzani waweke mabango ya wagombea.
 
Mdada Akiwa mzuri haitaji make up wala kuvaa vizuri kiivyo ila akipita tu kila mtu atasema hii pisi kali. Kibaya chajitembeza mkuu
Sitaki kabisa kuamini kuwa hujui maana ya matangazo na umuhimu wake kimkakati iwe kibiashara ama kampeni Kama hivi.
 
kuanzia tarehe 15 october 2020 mabango ya chadema yatatoka ili wananchi wasisahau sura ya kuiwekea tiki
 
Hapa ndio bukoba alipokosa watuView attachment 1570881View attachment 1570883

Wekeni matangazo acheni kudanganyana na ubishi usio na tija huku wenzenu wakizidi kuwafikia zaidi wananchi we unakuta watu hata mgombea udiwani wa kata yao hawamjui sa unategemea nini hapo?


The numbers of the peoples which occurred on the ccm Rally its few to comparing with the real residents which find in Bukoba Municipal.
 
Back
Top Bottom