Uchaguzi 2020 Vyama pinzani badilikeni, uchaguzi ni matangazo wekeni picha za Wagombea wenu mitaani

Uchaguzi 2020 Vyama pinzani badilikeni, uchaguzi ni matangazo wekeni picha za Wagombea wenu mitaani

Hivi wewe kwa akili yako hapa unampigia mtu kura kwa wingi wa mabango/ matangazo yake au mvuto wa sera zake?
 
Kama TV, magazeti,Radio na online tv zimezuiwa kutokumtangaza mgombea wa upinzani na wananchi bado wanahudhuria na kupata taatifa zote kuhusu kampeni, sio kma hayo mabango ya ccm Nchi nzima Kama yatasaidia. Watu wa Sasa sio wa miaka ya 1970s' watu wanajitambua wanajua kinachoendelea wewe washauri ccm waongeze mpk mashuleni mahospitali.
Tv ipi iliyokatazwa?mbona nimeangalia ITV leo saa mbili nimeona habari za Lissu Yuko Njombe?Watanzania jamani hebu tupunguze dhambi ndogondogo
 
Kule iringa mabango yote wahuni waliotumwa na mgombea wa ccm waliyapiga rangi yote usiku.
 
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini vyama pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani...
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Huko Iringa Msigwa kupata hasara sana. Kwa kujua kuna ubanduaji picha, aliamua katumia gundi imara sana ambayo ngumu kubanduka na hata ukibandua kinatoka kipande kidogo tu na kuiacha picha nzima inaonekana vizuri. Baada ya kugundua hivyo, mahasimu wake waliamua kuzipaka rangi nyekundu picha zote toka juu ya mlima Ipogolo mpaka chini. Picha za rangi nchi 18 zaidi ya 200 kuharibiwa hivyo ni hasara ya kiasi gani.

Hayo ndiyo wanayokutana nayo wapinzani uchaguzi huu. Kama kweli unao uchungu nao na hausemi kwa unafiki. Wapigie kampeni na uwape kura yako itakayowaondoa kwenye unyonge huu.

TBC chombo cha taifa kimetoa waandishi watatu wanaotembea na wapiga kampeni wa ccm. Lakini Wapinzani wanategemea wawakilishi wa mikoani. Yanamwisho
 
Kuna vyama haviko serious na uchaguzi.
Kuna majimbo hata hatujui nani anagombea na wagombea wapo....
Hilo la kweli mkuu hata mie eneo langu huku watu hawajui wagombea wa upinzani ni akina nani?kuna jamaa alikuwa diwani wetu kupitia chama cha Cuf ila sasa amehamia ccm na anagombea tena na ndiyo huyo tu anajulikana ila wagombea wenzake wa vyama vyengine hawajulikani hata kama wapo.
 
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini vyama pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani.

Hali hii inawafanya wananchi wengi kuona kama vile vyama pinzani haviko serious na havijajipanga kwa uchaguzi.

Achaneni na hiyo hoja kuwa eti mnazuiliwa kuweka mabango na mamlaka za jiji, wananchi wanajua huo ni uzushi hizi sehemu za mijini watu ni wasomi hawadanganyiki kirahisi namna hiyo.

Toeni fungu, tengenezeni mabango ya kampeni. Uchaguzi bila matangazo ni kujiandaa kushindwa na si kushinda.
Membe kasema vyama vinakabiliwa na ukata

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini vyama pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani...
Sihitaji kuona picha ili kumchagua mtu. Mie nikishika karatasi tu natafuta mgombea wa Chadema naweka tiki kwenye kibox chake!!
 
The numbers of the peoples which occurred on the ccm Rally its few to comparing with the real residents which find in Bukoba Municipal.
Kwani idadi ya wanao jitokeza kupiga Kura inalingana na idadi ya watanzania wote? Idadi ya watu kwenye kampeni ya vyama pinzani ndio sawa na idadi ya watu kwenye eneo husika?
 
Nimekumbuka bango la Lowassa Ubungo mawasiliano.. bango la Lowassa Kariakoo sokoni...

Siku bango la Lowassa linafungwa sokoni Kariakoo ilikuwa shangwe Kariakoo yote mpaka unashangaa nini kimetokea.. Nikajibiwa bango la Rais linafungwa sokoni.
images(4).jpg

Ilikuwa funga kazi
 
Back
Top Bottom