Uchaguzi 2020 Vyama pinzani badilikeni, uchaguzi ni matangazo wekeni picha za Wagombea wenu mitaani

Hivi wewe kwa akili yako hapa unampigia mtu kura kwa wingi wa mabango/ matangazo yake au mvuto wa sera zake?
 
Tv ipi iliyokatazwa?mbona nimeangalia ITV leo saa mbili nimeona habari za Lissu Yuko Njombe?Watanzania jamani hebu tupunguze dhambi ndogondogo
 
Kule iringa mabango yote wahuni waliotumwa na mgombea wa ccm waliyapiga rangi yote usiku.
 
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini vyama pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani...
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Huko Iringa Msigwa kupata hasara sana. Kwa kujua kuna ubanduaji picha, aliamua katumia gundi imara sana ambayo ngumu kubanduka na hata ukibandua kinatoka kipande kidogo tu na kuiacha picha nzima inaonekana vizuri. Baada ya kugundua hivyo, mahasimu wake waliamua kuzipaka rangi nyekundu picha zote toka juu ya mlima Ipogolo mpaka chini. Picha za rangi nchi 18 zaidi ya 200 kuharibiwa hivyo ni hasara ya kiasi gani.

Hayo ndiyo wanayokutana nayo wapinzani uchaguzi huu. Kama kweli unao uchungu nao na hausemi kwa unafiki. Wapigie kampeni na uwape kura yako itakayowaondoa kwenye unyonge huu.

TBC chombo cha taifa kimetoa waandishi watatu wanaotembea na wapiga kampeni wa ccm. Lakini Wapinzani wanategemea wawakilishi wa mikoani. Yanamwisho
 
Kuna vyama haviko serious na uchaguzi.
Kuna majimbo hata hatujui nani anagombea na wagombea wapo....
Hilo la kweli mkuu hata mie eneo langu huku watu hawajui wagombea wa upinzani ni akina nani?kuna jamaa alikuwa diwani wetu kupitia chama cha Cuf ila sasa amehamia ccm na anagombea tena na ndiyo huyo tu anajulikana ila wagombea wenzake wa vyama vyengine hawajulikani hata kama wapo.
 
Membe kasema vyama vinakabiliwa na ukata

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hili suala si la kulifumbia macho ama kulidharau, ukipita kwenye kona mbali mbali za jiji la Dar utakuta ni picha tu za wagombea wa CCM ndio zimetawala mji mzima lakini vyama pinzani hakuna kabisa mabango yao ya kampeni mitaani...
Sihitaji kuona picha ili kumchagua mtu. Mie nikishika karatasi tu natafuta mgombea wa Chadema naweka tiki kwenye kibox chake!!
 
The numbers of the peoples which occurred on the ccm Rally its few to comparing with the real residents which find in Bukoba Municipal.
Kwani idadi ya wanao jitokeza kupiga Kura inalingana na idadi ya watanzania wote? Idadi ya watu kwenye kampeni ya vyama pinzani ndio sawa na idadi ya watu kwenye eneo husika?
 
Nimekumbuka bango la Lowassa Ubungo mawasiliano.. bango la Lowassa Kariakoo sokoni...

Siku bango la Lowassa linafungwa sokoni Kariakoo ilikuwa shangwe Kariakoo yote mpaka unashangaa nini kimetokea.. Nikajibiwa bango la Rais linafungwa sokoni.

Ilikuwa funga kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…