Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
madeni makubwa yasiyoeleweka wala yasiyolipika ni miongoni mwa hatari zinazo zengea zengea kwenye korido za miongoni mwa vyama vya siasa vikongwe na visivyo vikongwe kwenye ulingo wa kisiasa humu nchini..
hali hii ya madeni kupindukia, imepelekea kutokua kabisa na meno au sauti ya kukemea vitendo vya rushwa ndani yake na wala sio rahisi kubainisha kwamba hii fedha ni rushwa, mchango, hisani, msaada au mkopo kwaajili chama ama laa..
haijulikani taarifa zipi ni mikopo, hisani, mchango ya wanachama au misaada...
cha kushangaza zaidi,
mkopeshaji mkuu wa chama hicho ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama husika...
unakuta chama cha siasa mathalani, kila kitu anachotumia mwenyekiti ni cha mkopo tangu amechaguliwa, makamu mwenyekiti na katibu mkuu nae vile vile anaenda ofisini kwa mkopo, anaenda kwenye mikutano ya kisiasa na seminars kwa mikopo tangu amechaguliwa...
kila anakwenda madeni yanamfuata....
sasa kwa hali hiyo,
chama kinaweza kujenga hata ofisi au choo cha ofisi kweli?
kwa madeni hayo,
chama kama hicho kinaweza kukemea na kupambana na rushwa kweli?
chama kama hicho,
kinaweza kua na mawazo mapya na fikra mbadala kweli na kuleta mageuzi ya kisiasa kijamii na kiuchumi kwa wananchi kweli?
nadhani kuna vyama vya siasa nchini vilivyo kwenye hatari ya kusambaratika, kwasababu tu ya kujiendesha kwa madeni na mikopo isiyolipika na matumizi ya fedha yasiyo eleweka na yenye viashiria vya rushwa na udanganyifu kupindukia 🐒
ni muhimu sana kwa vyama vya siasa vyenye malengo, kua na vyanzo mbadala wa mapato kuliko kutegemea chanzo kimoja tu ambacho tena ni mikopo tu.
Mungu Ibariki Demokrasia za vyama Tanzania..