Vyama vya Siasa ndio wawakilishi na watetezi wa wanyonge. Fikirieni suala la makazi nafuu mijini

Vyama vya Siasa ndio wawakilishi na watetezi wa wanyonge. Fikirieni suala la makazi nafuu mijini

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Vyama vya Siasa ndiyo wawakilishi wa wananchi, ndiyo sauti ya wengi. Katika sera zenu wengi wameongelea Afya ya Jamii, maji, umeme, elimu, kilimo, biashara, nk.

Wananchi ambao ni wapiga kura wenu, hasa wanaokaa mijini wengi ni wenye kipato chini ya Tsh 500,000 kwa mwezi. Wengi wako kwenye ujira wa 300,000 au chini ya hapo kwa mwezi. Wengine ni waajiriwa wenye ujuzi ambao ujuzi wao unaendeleza jamii. Lakini watu hawa uwezo wa kuishi kwenye makazi yenye hadhi mijini ni changamoto.

Kama mtaweza kufikiria ujenzi wa nyumba self contained au flats za chumba kimoja, viwili na vitatu, zipangangishwe kwa kodi ya 100,000, 150,000 mpaka 200,000 kwa mwezi. Ili kwasaidia wenye kipato cha chini kuwa na makazi yenye hadhi.

Kigezo cha kuapata nyumba hizi kiwe wenye mishahara chini ya 500,000 kwa mwezi. Sisi wa hali ya chini tumechoka kuishi kwenye chumba na sebule na kutumia vyoo vya passport size. Hata tukienda Mloganzila tuwe na mazoea ya kutumia miundo mbinu kama vyoo na mabafu.
 
Hili litawezekana kwa kuanzisha mufuko ya hifadhi ya majimbo.

Pesa hizi za mifuko ndizo zinaziwezesha ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Na mifuko ya hufadhi ya jamii itaonyesha tija endapo kutakuwa na mkakati wa makusudu wa kuongeza au kurasikisha ajira.

Na ajira zitapatikana endapi tutaweza kuongeza thamani za bidhaa au mazao yetu.

Na tutaweza kuongeza thamani ya bidhaa zetu kwa kutafuta masoko ya nje na kubuni au kununua mashine zinazoendana na teknolijia ya sasa.
 
Mbona nyumba za bei hizo zipo, unataka serikali kama ya uingereza imiliki nyumba zote za kupangisha.
 
Hili litawezekana kwa kuanzisha mufuko ya hifadhi ya majimbo.

Pesa hizi za mifuko ndizo zinaziwezesha ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Na mifuko ya hufadhi ya jamii itaonyesha tija endapo kutakuwa na mkakati wa makusudu wa kuongeza au kurasikisha ajira.

Na ajira zitapatikana endapi tutaweza kuongeza thamani za bidhaa au mazao yetu.
Na tutaweza kuongeza thamani ya bidhaa zetu kwa kutafuta masoko ya nje na kubuni au kununua mashine zinazoendana na teknolijia ya sasa
Mwanzo utakuwa mgumu lakini kukiwa na mipangilio mizuri kuwa wasiolipa wanatolewa na wengine wanaohitaji wapaewa nyumba. Watu watawajibika na makusanyo yanaweza kuongeza nyumba nyingine.
 
Back
Top Bottom