Irenga
JF-Expert Member
- Dec 14, 2015
- 3,287
- 2,560
Ni wazi Dunia imebadilika sana hasa katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia katika Karne ya 21 hii nilitegemea kuona Vyama vya Siasa vitoa Fomu kwa njia ya Mtandao ( Online ) kama vile ambavyo Wanafunzi huomba nafasi za kujiunga na Vyuo Mbalimbali lakini cha kushangaza hakuna hata Chama kimoja kimefanya hivyo badala yake Wagombea/Watia nia wanaenda kupanga foleni huku wakipoteza rasilimali muda, nguvu kazi ya Taifa kusubiria Fomu, kujaza na kurejesha Fomu.
Nilitamani kuona Vyama vya Siasa vikiandika Orodha ya Majina ya Watia nia/Wagombea angalau Waandishi wa Habari wawahabarishe Wananchi nao wapakue wasome wenyewe majumbani kwao lakini nimebahatika kuona Jimbo moja tu ndilo limeorodhesha Majina . Inasikitisha zaidi kuona Ofisini kuna Printers na Mashine za kuburuza lakini hazitumiki ipasavyo hata kama wameshindwa basi waandike majina wakachape na buruza kwenye Stationary za kujitegemea ili kuendana na thamani ya Kuuza Fomu za Wagombea ambapo hutoa 5000-100,000 TZS tuache kulibagaza Taifa kwa aibu na tubadilike.
Vyama vya Siasa vinahitaji Mabadiliko basi ni vyema wawe tayari kubadilika hata walandane na Matakwa ya Kidunia.