Vyama vya upinzani havina nia ya kuikomboa Tanzania tutafute mgombea binafsi

Vyama vya upinzani havina nia ya kuikomboa Tanzania tutafute mgombea binafsi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Vyama vya upinzani havina nia ya kuikomboa Tanzania tutafute mgombea binafsi.

Nimekaa nimewaza juu ya mwenendo wa siasa za taifa letu.

Nikirejea kwa hawa wenzetu chama tawala jinsi wanavyoenenda. Ni dhahiri inaonyesha hawana muda mrefu wataachia hili taifa mikononi mwa chama kingine.

Sasa nilitegemea hawa wa vyama vya upinzani kuwa na mikakati thabiti inayoeleweka ili wapindue meza, ili 2025 wachukue nchi kiurahisi.

Sasa cha ajabu hawana mikakati yeyote ile.

Kiukweli ninaona katiba hampatii nafasi mwananchi kujikomboa bila kutegemea chama. Kungelikua na uwezekano katiba iruhusu mtu asiye na chama kugombea ili tupate watu wenye uchungu na kile wanachokitafuta.

Lakini hawa wapinzani wetu mbona kama siwaelewi.
 
Nia ipo sema CCM kuona upinzani hataki yupo radhi kuua au kufanya lolote ili yeye kubaki.

Watu wamekaa kimya sio kimya unacho jua Katiba Mpya kwanza hii ndio itakuwa pigo la CCM
 
Vyama vya upinzani havina nia ya kuikomboa Tanzania tutafute mgombea binafsi.

Nimekaa nimewaza juu ya mwenendo wa siasa za taifa letu.
Nikirejea kwa hawa wenzetu chama tawala jinsi wanavyoenenda. Ni dhahiri inaonyesha hawana muda mrefu wataachia hili taifa mikononi mwa chama kingine.
Sasa nilitegemea hawa wa vyama vya upinzani kuwa na mikakati thabiti inayoeleweka ili wapindue meza, ili 2025 wachukue nchi kiurahisi.
Sasa cha ajabu hawana mikakati yeyote ile.

Kiukweli ninaona katiba hampatii nafasi mwananchi kujikomboa bila kutegemea chama. Kungelikua na uwezekano katiba iruhusu mtu asiye na chama kugombea ili tupate watu wenye uchungu na kile wanachokitafuta.

Lakini hawa wapinzani wetu mbona kama siwaelewi.
Subiri kidogo chama cha legacy ya kizalendo kinaanzishwa hivi karibuni kitakuwa na legacy ya JPM NA NYERERE TU
 
Tanzania ni mapema sana kutafuta mgombea binafsi, mpaka kwanza tujadili funzo la JPM ambaye ni kama alikuwa mgombea binafsi kwa sababu, hakutaka chama kimdhibiti, hivyo aliishia kwenye wizi mkubwa, udikteta, uuaji.

Namuita mgombea binafsi kwa kuwa hata serikali aliita kwa jina lake binafsi kama zawadi ya pipi aliyopewa na baba yake "serikali ya magufuli"
 
Mahakama ilisharuhusu mgombea binafsi, utetezi wa serikali ilikuwa swala ilo lipo kwenye rasimu ya katiba.
Maadamu rasimu imezikwa kinachotakiwa ni kurudi mahakamani na kukazia hukumu.
Wanaopinga mgombea binafsi sio ccm peke yake bali hata vyama shindani havitaki kwa sababu wanataka kudhibiti wabunge wao
 
Back
Top Bottom