kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kwa heshima na taadhima mimi binafsi naheshimu mawazo mbadala ya kuliendea jambo kulitatua ili kuliondosha, kuliboresha au kupata ahueni.
Tangu wimbi la demokrasia ya vyama vingi litue Afrika ikiwemo Tanzania tumeshuhudia uanzishwaji wa vyama vingi ambavyo vinasema kuwa kuna njia rahisi sana ya kufanikisha mambo yetu Afrika na Tanzania kuliko njia hizi zinazotumiwa na vyama tawala vya sasa.
Tanzania bado, lakini Zambia, Uganga, Burundi, Rwanda, Malawi, Kenya, DRC, Ethiopia, Sudani Kusini, Misri, Libya, na mataifa mengine vyama vya upinzani vilifanikiwa kuviondoa vyama tawala na wao kuingia madarakani, LAKINI hata vyama hivyo vipya vya upinzani havikuonyesha na havionyeshi utofauti kwenye maisha ya wananchi wao kuliko maisha yalivyokuwa wakati utawala wa vyama vya zamani. Maendeleo na maisha ya waafrika yanafanana tu bila kujali ni chama za zamani au kipya kinaongoza nchi.
Maswali yangu ni haya hapa:
1. Ni nini hasa kinasababisha Afrika yote ifanane kimaendeleo?
2. Kama vyama vyenu vikipata nafasi ya kushika dola mtafanyaje kuzuia sababu hizi zinazosababisha nchi zote za bara lote la Afrika chini ya uongozi wa vyama vya siasa vikongwe na vile vipya vya upinzani zifanane kimaendeleo?
3. Wapi mtapata soko zuri la mazao (korosho, pamba, mbao), madini, na wanyama wetu tofauti na sasa?
4. Mtafanya nini ili tanzania kuwe na huduma za kutosha za umeme, maji, chakula, afya, elimu, usafirishaji, ulinzi na usalama na ajira kwa vijana?
5. Vyama vya upinzani ni ajira sawa na ajira nyingine? Hii ni baada ya kuona viongozi wa upinzani, wabunge na waanzilishi wa vyama hivi wakilimiki mahoteli, majumba, magari ya kifahari, miradi, mastudio, mashamba, kusomesha watoto wao shule za gharama, shule, nk binafsi badala ya kutumia hela hizo kujenga na kuimarisha vyama vyao au hata pesa hizo kwenda kusaidia wananchi wenye shida kama ya maji, ada, umeme, nyumba, usafiri, afya, nk.
Naomba tafadhali kwa unyenyekevu tu mjibu maswali haya ili tuone thamani halisi ya vyama vya upinzani ili wanaoviunga mkono hivi vyama waione thamani na hasara ya kuviunga mkono. Maana wananchi hawa ndiyo wanaovipigia na kulinda kura za wagombea wa vyama. Wanapenda kujua maisha yao yatatofautianaje na ya sasa au vyama vya upinzani vya mataifa mengine vilivyofanikiwa kushika dola vinakosea wapi?
Je, ruzuku, mahoteli, majumba, magari na mali za viongozi/wabunge wanazozipata baada ya kuungwa mkono na kupigiwa kura na kuchaguliwa zinawanufaishaje watu hawa? Au wanatumika tu kutafutia watu ulaji na maisha kwa familia zao?