Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Najua ni ujinga na upuuzi kwa NEC kuwaengua wagombea wa vyama vya upinzani kwa makosa madogo madogo katika ujazaji wa form.
Lakini pamoja na hilo, vyama vyote vya upinzani vinalo la kujifunza hapa. Unaweza kujiuliza, mbona wagombea wengi wa CCM form zao hazina matatizo? Iko hivi;
- Baada tu ya kanuni za uchaguzi kutangazwa, CCM walitoa semina kwa viongozi wao wote (makatibu wakuu hadi ngazi za chini) juu ya kanuni hizo. Sote tuliliona hili likifanyika.
- Uteuzi wa wagombea ulipo kamilika, wagombea wote waliitwa wilayani na form zao. Wakaelekezwa waende kuzijaza sehemu ya wadhamini pekee, kisha wakapewa tarehe ya kurudi tena hapo wilayani ili kukamilisha ujazaji.
- Tarehe ya kurudi ilipofika, form, wote walirejea na viambatanishi vyote muhimu kama vile picha ya paspoti n.k
- Viongozi wa chama walizikagua fomu zote, kisha zoezi la ujazaji likaanza. Ilikua wanajaza kipengele kimoja baada ya kingine wote kwa pamoja chini ya maelekezo na usimamizi wa viongozi.
- Baada ya zoezi kukamilika, form zikakaguliwa tena, kisha zote zikarudishwa ofisi ya msimamizi wa uchaguzi ndani ya siku moja.
Jinsi CCM walivyofanya zoezi hili muhimu inakuonesha tofauti kubwa kati yao na vyama vingine. Wamelifanya kama taasisi imara yenye uongozi imara mpaka ngazi za chini. Hakukua na nafasi ya mgombea kufanya makosa ya kijinga (either kwa makusudi au bahati mbaya), au kujichelewesha kupeleka form.
Anyway, hivyo ndivyo zoezi lilivyo endeshwa hapa wilayani kwetu, natumaini utaratibu ulikua huohuo nchi nzima.
Ni lazima vyama vya upinzani vijifunze kwenye hili, la sivyo wataendelea kulia kila uchaguzi.