Usiwajaze watu uongo ili kujenga hoja ya kuhalalisha njama na maovu yanayofanywa na CCM! Maelekezo yaliyopo kwenye zile form yanajitosheleza na yanaeleweka kabisa wala haitaji Semina wala uzoefu! Nani hajuwi kama vimeshafanywa visvyoeleweka??
Acheni kujichanganya mseme CCM ilisambaza wanasheria Nchi nzima!, Mara mseme walitoa semina! Mara walipelekwa wilayani! Wananchi sio wajinga wanelewa wazi kuwa kuna mitego inawekwa kwenye hizo form ili mgombea akijaza tu, hachomoki kwenye pingamizi au anaenguliwa kwa madai ya kukosea kujaza form!
Kuna mapingamizi mengine yametengenezwa na watu wasio wagombea lakini kwa maelekezo na ushirikiano na wanaoshughulikia hizo form alafu mtu unatoka hadharani kutamka eti hawakupewa semina na kusimamiwa! Hivi kuna vyama vinavyofanya shughuli zao kwa umakini kama wapinzani hususani CHADEMA??
Kama ujazaji wa hizo form ni lazima kusomea sheria , basi hata hao waliopita bila kupingwa hawana vigezo!