Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,566
Uchaguzi umegeuka kuwa wa kumtafuta bingwa wa kujaza fomu kiufasaha na si kumtafuta mwakilishi wa wananchi!Lakini wapinzani wanaenguliwa kwa kukosea kujaza form, hivyo dawa ni kutokukosea! Chama kiwajibike kuwasaidia wagombea wake badala ya kila kuachiwa akajaze anavyojua yeye.
Please tusipotezeane muda bana, mbona mgumu kuelewa wewe! Mbona Ngwajima aliyeandika Jina lake ni Askofu hajaenguliwa? Wako wagombea wengi tu wa CCM wamebandika picha za kipemara, ubatizo na harusi kwenye fomu mbona hawajaenguliwa???Pointi yangu kuu hapa ni chama kuwasaidia wagombea wake kwenye mambo haya.
Hili linaweza kuepusha hata wale wanao nunuliwa na kukosea kujaza form kwa makusudi.
Nyinyi ni shida!! Mtabaki hivyo hivyo mnafundishwa cha kufanya lakini mapovu tuuu!!Kwa vyo vyote
1. Ujazaji wa fomu hauwachagulii wapiga kura wawakilishi wanaowahitajika .
2. Maana ya uchaguzi ni fursa ya hiari ya kura yako kuamua unayempima kuwa anafaa.
2. Aliyeteuliwa ni uwakilishi wa aliyemteua si uchaguzi wa wapiga kura.
4. Nakubaliana na wewe kuwa CCM walijitayarisha kuhumu uchaguzi kwa kuwaengua washindani. Wenye akili wanajua hawangefua dafu kwa wapiga kura.
KUNAPOKOSEKANA DHAMIRA YA KUTENDA HAKI, CCM HUTANGAZA HUJUMA ZAO KUWA WANAPENDWA NA WAPIGA KURA NA KUWA NI HAKI YAO. WANAPOBAKI MADARAKANI KWA NGUVU YA DOLA WANASHINDWA KWENYE MIPANGO NA MIKAKATI INAYOTARAJIWA NA WANANCHI.
Tatizo hawa ndugu zangu ni wabishi kweli. CCM inamfumo mzuri sana wa kitaasisi, lakini hawa ndugu hata ukiwaambia jengeni ofisi za maana ili muachane na habari za kufanyia vikao mlimani city na mahotelini hawataki kabisa kusikia.Umewapa somo zuri sana lakini wanasaccos na timu yao hawatakuelewa bali wataleta mqpovu tu.
Ni kweli, ideally mambo yanapaswa kuwa hivyo, lakini kwenye mazingira halisi hali ndio iko hivi kama tuliyonayo, sasa kwanini chama makini kifanye uzembe na kumpa mtesi wake nafasi ya kukiadhibu?Kwa vyo vyote
1. Ujazaji wa fomu hauwachagulii wapiga kura wawakilishi wanaowahitajika .
2. Maana ya uchaguzi ni fursa ya hiari ya kura yako kuamua unayempima kuwa anafaa.
2. Aliyeteuliwa ni uwakilishi wa aliyemteua si uchaguzi wa wapiga kura.
4. Nakubaliana na wewe kuwa CCM walijitayarisha kuhumu uchaguzi kwa kuwaengua washindani. Wenye akili wanajua hawangefua dafu kwa wapiga kura.
KUNAPOKOSEKANA DHAMIRA YA KUTENDA HAKI, CCM HUTANGAZA HUJUMA ZAO KUWA WANAPENDWA NA WAPIGA KURA NA KUWA NI HAKI YAO. WANAPOBAKI MADARAKANI KWA NGUVU YA DOLA WANASHINDWA KWENYE MIPANGO NA MIKAKATI INAYOTARAJIWA NA WANANCHI.
Hii mbinu itatumika tena 2025, lakini pia kuna mbinu mpya zitaibuka. Wapinzani wajijenge kitaasisi zaidi na wawe na intelijensia ya kuyang'amua haya mapema.Unaposema wapinzani wajifunze kwenye hili unakosea kwani kuna uhakika gani kama uchaguzi mwingine watakuja na mbinu hii tena ya kuweka complications kwenye form?
nadhani ifike mahali upinzani ujifunze kuwa andaa wagombea wake ili kutokuja kuviziana kwenye ushindi wa mezani na kuishia kulalamikia mpingamizi kutupiliwa mbaliTume ni ccm utake usitake, kosa umesema ni tecnical la mgombea wa njombe na kawekewa pingamizi sasa nec inasubiri nini kumtoa?
Usiwajaze watu uongo ili kujenga hoja ya kuhalalisha njama na maovu yanayofanywa na CCM! Maelekezo yaliyopo kwenye zile form yanajitosheleza na yanaeleweka kabisa wala haitaji Semina wala uzoefu! Nani hajuwi kama vimeshafanywa visvyoeleweka??
Acheni kujichanganya mseme CCM ilisambaza wanasheria Nchi nzima!, Mara mseme walitoa semina! Mara walipelekwa wilayani! Wananchi sio wajinga wanelewa wazi kuwa kuna mitego inawekwa kwenye hizo form ili mgombea akijaza tu, hachomoki kwenye pingamizi au anaenguliwa kwa madai ya kukosea kujaza form!
Kuna mapingamizi mengine yametengenezwa na watu wasio wagombea lakini kwa maelekezo na ushirikiano na wanaoshughulikia hizo form alafu mtu unatoka hadharani kutamka eti hawakupewa semina na kusimamiwa! Hivi kuna vyama vinavyofanya shughuli zao kwa umakini kama wapinzani hususani CHADEMA??
Kama ujazaji wa hizo form ni lazima kusomea sheria , basi hata hao waliopita bila kupingwa hawana vigezo!
Sasa unafikiri kwa nn polepole amepeleka wanasheria zenji kwa ajili ya kuwajazia form wagombea wao ? Maana yake form hizo zimeaandaliwa kwa ajili ya wapinzani wakosee hata huyo mwanasheria peke yake hawezi maana si mitego ya kiufundi ni ya makusudi lakini kwa nini iwe hivyo? Kigezo cha kukosea herufi si cha kumuengua ni kurkebisha tu vipo vigezo vya muhimu
Mfumo wa kuengua wagombea ni wa serikali iliyo madarakani. Tutaupigia keller mpaka wajione walivyo wapumbavu. Naamini hata kwenye sanduku la kura kukataa mfumo huu kandamizi kutawekwa alama.Ni kweli, ideally mambo yanapaswa kuwa hivyo, lakini kwenye mazingira halisi hali ndio iko hivi kama tuliyonayo, sasa kwanini chama makini kifanye uzembe na kumpa mtesi wake nafasi ya kukiadhibu?
Lakini pia kuna wagombea wa upinzani wanatumia mwanya huo kuchukua pesa upande wa pili na kujaza form vibaya ili waenguliwe.