Wafuasi wa vyama vikuu vya upinzani nchini CHADEMA na ACT Wazalendo Mkoani Lindi wameungana na wenzao wa CCM pamoja na wananchi katika mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Wafuasi hawa wanajua ya kuwa maendeleo hayana chama, maana Rais Samia Suluhu amefanikiwa kuwaboreshea sekta ya afya, sekta ya elimu, sekta ya kilimo pia ameboresha miundombinu katika mkoa wao. Hivyo wana kila sababu ya kumkaribisha Rais wetu mpendwa kwa furaha.
Kwa mambo yanavyoenda inaonekana Rais Samia Suluhu anaenda kuvunja record kwa kuwa Rais wa kwanza kupendwa Tanzania.