Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 4,240
- 10,561
Habari wana jamiiforums, poleni na majukumu ya hapa na pale 🤝, Hili bandiko sijagusa Maisha ya mtu/watu. Lakini Kwa njia hii, vyeti vya wanachuo vitoe picha kamili na sahihi kuhusu sababu za muda mrefu wa masomo yao, hii itasaidia kuepusha mkanganyiko kuhusu uwezo wao wa kitaaluma na changamoto walizokutana nazo nje ya darasa. ( kuna wahitimu wengine wamepitia misukosuko migumu sana ya kiuchumi wakati wa masomo yao, lakini bado watajumuishwa na wale walioludia ludia masomo kwa sababu ya uwezo wao mdogo wa akili)
• Wahitimu wengi wameshindwa kuajiriwa sehemu mbali mbali kutokana na Afya ya vyeti vyao, mfano mhitimu cheti kinaonesha alianza masomo mwaka 2018 na kumaliza masomo yake mwaka 2024, tukija kwa upande wa mwajiri hapa moja kwa moja atahisi huyu muombaji alikuwa anauwezo mdogo darasani na ndo maana alikaa mda mrefu chuoni kwa sababu ya kuludia ludia masomo( sup za kutosha), hivyo hata kama kulikuwa na nafasi ya kuajiriwa lazima atakosa bila kuwa na sababu za msingi kwa sababu upande wa pili unakuwa haujaangaliwa.
• Utaratibu huu wa cheti cha mhitimu kuonyesha sababu za kukaa mda mrefu chuoni ni muhimu sana ili kutoa uwazi na haki kwa wanachuo wote.

1. Cheti cha Kuhitimu, Kama mwanafunzi alifeli Cheti kioneshe wazi kuwa mwanafunzi alirudia mwaka kutokana na kushindwa mitihani kwa kipindi cha mda miaka kadhaa. Na kuwe na kauli kama "Alirudia mwaka kutokana na kushindwa kufikia viwango vya ufaulu."
2. Cheti cha kuhitimu, Kama mwanafunzi ali-postpone Cheti kioneshe wazi kuwa mwanafunzi aliahirisha masomo kwa sababu maalum, kama vile matatizo ya kifamilia au kiuchumi. Na kuwe na kauli kama" Ali-postpone masomo kutokana na matatizo ya kimaisha."
3. Karatasi ya Matokeo, Karatasi ya matokeo( transcript) iwe na kipengele maalum kinachoelezea sababu za mwanafunzi kurudia mwaka au kuahirisha masomo. Kwa mfano, inaweza kuwa na sehemu ya maelezo ya ziada kama vile:"Mwanafunzi alirudia mwaka wa masomo kutokana na kushindwa mitihani ya mwisho wa mwaka.
AU
""Mwanafunzi ali-postpone mwaka wa masomo kutokana na matatizo ya kimaisha/kiuchumi.
4. Taratibu za Uthibitisho, Kuhakikisha kuwa sababu za kurudia mwaka au kuahirisha masomo zimehakikiwa na zimeidhinishwa na vyombo husika kama bodi ya masomo au uongozi wa chuo. Uthibitisho wa sababu hizi uweze kwa kutumia nyaraka rasmi kama vile ripoti za matibabu, barua za kisheria, au ripoti za kijamii ambazo zitawekwa kwenye rekodi za mwanafunzi.
5. Mfumo wa Kielektroniki, Kuwe na mfumo wa kielektroniki unaoruhusu wanafunzi kuona historia yao ya masomo na sababu zilizoandikwa kuhusu mabadiliko yoyote katika ratiba yao ya masomo. Mfumo huu uweze pia kuruhusu wanafunzi kutuma nyaraka za kuthibitisha sababu zao za kuahirisha au kurudia mwaka moja kwa moja.
6.Kuandaa mafunzo kwa wahadhiri, watunza kumbukumbu, na maafisa wengine wa chuo kuhusu jinsi ya kushughulikia na kuweka kumbukumbu hizi kwa njia sahihi na kwa uwazi. Kwa njia hizi, vyeti vya wanachuo vitatoa picha kamili na sahihi kuhusu sababu za muda mrefu wa masomo yao, na kuepusha mkanganyiko kuhusu uwezo wao wa kitaaluma na changamoto walizokutana nazo nje ya darasa.