econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 25,522
- 40,795
Naona kama Kuna collaboration kati ya vyombo vya habari na hawa machawa wa Abdul. Anaibuka mtu hata sio mwanachama wa CHADEMA na kudai Heche achunguzwe. Cha kushangaza, vyombo vya habari bila kutathmini na kuchunguza nafasi ya msemaji, vikaja na kichwa cha habari: Vijana wa BAVICHA Pwani wamtaka Heche achunguzwe. Wakati aliyeongea ni Mmoja.
Kwa maana nyingine mtu yoyoyte anaweza kuamka asubuhi na kuita Press na kujipa cheo ndani ya CHADEMA na kuanza kumshambulia Heche bila ushahidi.
Pia, tukumbuke Katibu Mkuu alishafunga hili Suala ya kwamba kama Kuna mtu ana tuhuma azipeleke zitafanyiwa kazi. Ila watu wamekomaa na press conference tena wakiwa eneo Moja.
Vyombo vya habari vinatakiwa vichunguze source ya habari na validity ya habari. Yani hakuna hata mwandishi aliyeweza kuhoji ukweli wa cheo cha huyo mtu?. Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Pwani anajulikana hata kwa majina. Anaitwa Richard Mbalase. Inakuwaje anaibuka mtu na kujipa cheo asichokuwa nacho na wala hakuna chombo cha habari cha kuhoji usahihi wa cheo na kinacho semwa.
Vyombo vya habari vijitathmini sana vinaua uhalali wake kisa bahasha za khaki.