Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Huwezi kuongelea siasa ya nchi yetu Tanzania pasi na kuwepo vilabu vya Yanga na Simba na huo ndiyo ukweli.
Sasa ndani ya Taasisi ya Simba kuna huyo binti Babra ambaye ndiye CEO wa klabu ile hakika ndani ya muda mchache ameshagombana na kila aliyehisi ni kirusi kwenye nafasi yake!
Utulivu haupo tena ndani ya Simba kwa sababu ya roho ya chuki ya binti huyo huku akijawa na majivuno yasiyo na staha hata kwa watu walio mzidi umri.
Ieleweke utulivu ndani ya Simba na Yanga ndiyo utulivu wa siasa za nchi yetu sasa anapotokea mtu mmoja anayetaka kusababisha taharuki ndani ya vilabu vyetu akamewe mara moja!
Babra hafai kuongoza Taasisi kubwa kama Simba ama Yanga kwa sababu hana uvumilivu na ni muumini wa kukomoa.