Vyombo vya Dola viendelea kuwachukulia hatua wanaovaa mavazi ya kijeshi

Vyombo vya Dola viendelea kuwachukulia hatua wanaovaa mavazi ya kijeshi

bongo dili

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
12,350
Reaction score
25,180
Wewe sio Askari kwanini uvae mavazi yasiyokuhusu? Mbona hamvai sare za wafungwa, madaktari, mapadre, nk? Kwanini ya jeshi wakati we si Askari? Kila mtu huvaa vazi kulingana na aina ya kazi yake.

Wengine huyatumia vibaya kwenye uhalifu mavazi hayo. Pitia huu ushuhuda binafsi;

Mimi anko wangu (RIP) aliuwawa na majambazi waliovaa sare za kijeshi akiwa bar, wakavamiwa, wakaambiwa wote walale chini. Akiwa tayari kilaji akainuka na kuwaambia, "Tutambuane wenzangu", akidhani ni wana kikosi wenzake. Hakuomba hata maji akapigwa risasi, tena na jambazi la kike na kufia hapo hapo, wakapora na katokomea.

Huwa hakuna mhalifu smart, walikuja kamatwa wote. Jambazi la kike alipohojiwa kwanini umeua askari akajibu, "Sikujua kama ni askari"! Hapo ndio imetoka hiyo, uhai haurudi tena, huyo jambazi katuachia tunalea yatima leo. Atajuana na Mungu wake kama alihukumiwa au alitoka jela, hatukufatilia tena imepita miaka 13 sasa tangu tukio hilo, RIP uncle.

Kwahiyo JWTZ wapo sahihi, mabasi yalitekwa na watu waliovaa sare za jeshi.
 
Yeah ni vyema kuepusha shari na vyombo vya dola.
 
Si kwamba wavaai hawajui ni kosa kuvaa nguo za jeshi,thus wakigongana na wanajeshi au askari utoka nduki kwa sababu wanajua ni kosa.
Yeyeto mvaaji we mwambie mbele Kuna askari kama hatokata kona.
 
Eti jeshi la magereza nalo waliwahi kuleteana za kuleta na madereva na makondakta wa daladala jijini dar wakidai yunifomu zao zinafanana na zao. Ikawa wanaleta ubabe kukataza rangi zao za ugoro zisiigwe na raia
 
hizi bakabaka tunavaa huku Mbande na Mvuti, ila mwisho Pugu, mjini hatuendi nazo
baka baka na suti ipi yenye bei.. 😅😅
images (1).jpeg
images.jpeg
 
Bakabaka zinavaliwa mbna,halafu za kinyama hatari ni kucheza na location tu
 
Back
Top Bottom