LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Kama majeshi hayataki rangi zao ziigwe bora raia wakaige mabaka na mistari ya wanyama kama chui, twiga, pundamlia, fisi, chatu, kanga na tausi. Huko nako mamlaka ya uhifadhi wanyamapori nao wakichachama watu kuiga rangi za wanyama itakuaje? Anyway kama wana hakimiliki ya madoa, mabaka na mistari ya wanyama kisheria itabidi waachiwe tu. Tayari kuna nguo zenye kufanana na rangi za wanyama na raia wanazivaa na hawajui kama kuna sheria ya kukataza kufanana na wanyama. Bora wahusika wajitokeze wawaweke wazi raia wasije wakawatia hasara kwenye biashara zao