Hili nalo litapita
Member
- May 6, 2024
- 7
- 3
UTANGULIZI:
Navipongeza vyombo vyote vya Habari ambavyo vinaendelea kuwa wabunifu katika kurusha matangazo/maudhui mbalimbali ili kuhabarisha jamii kwa kujumuisha mtindo wa tafsiri kwa ALAMA ili iwe rahisi kueleweka kwa watu wasio sikia vizuri au wasiosikia kabisa.
Hatua hii ni nzuri lakini bado ina changamoto kwani sio rahisi kuelewa kwa ufasaha na sio wote ambao hawasikii vizuri ni wenye kujua lugha ya ALAMA kwa sababu wapo wanaopoteza usikivu wakiwa wakubwa na ambao tayari wanajua kusoma maandishi kama kawaida.
Pia mtindo wa kuwekea video, picha maneno(CAPTION) ambao ndio umekuwa maarufu sana kwa sasa kwenye vyombo vya Habari hasa Televisheni, Televisheni za Mitandaoni, Video (Clips) huku ukifuatiwa na maelezo ya sauti kwa kina kuhusu picha, video husika unawaacha hawa watu bila kuelewa nini kimezungumzwa kwa kina.
Ili kutoacha hili kundi nyuma katika kuhabarisha, vyombo vya Habari vyote vinavyorusha maudhui/Habari hasa TELEVISHENI, TV za Mitandaoni nendeni mbali zaidi kwenye ubunifu, tumieni Teknolojia ya Kubadili sauti na kuwa maneno ambayo yatakuwa yanaonekana moja kwa moja mbele ya kioo cha Televisheni pindi mtangazaji anapotangaza/kusoma Habari.
Hii Teknolojia sio ngeni, imekuwepo kwa muda mrefu ikitumiwa na makundi mbalimbali kama Watafiti ambao wanataka kurahisisha kubadili sauti kuwa maneno, Wanahabari ambao wanafanya mahojiano mbalimbali na kurekodi sauti halafu baadae wakitaka kuweka katika maandishi wanarahisisha zoezi hilo kwa kutumia Teknolojia hii. Hata kwenye Filamu mbalimbali tumeona zikiwa zenye tafsiri ya kuonesha maneno pindi wacheza filamu wanapozungumza, hii imetuwezesha kuelewa filamu hata zikiwa katika lugha nyingine kwa kutafsiriwa kwa mtindo wa lugha nyingine kwa Teknolojia hii.
Televisheni zinazorusha taarifa za Habari kwa muda mahususi na zile za mitandaoni zinazotengeneza maudhui na kuyarusha ni rahisi kutumia hii tekenolojia hata kama watashindwa kutumia yenye kubadili sauti moja kwa moja, kwani wakati wanaandaa taarifa ya Habari wataweza kuibadili sauti na kuwa maneno kwa kurekodi kabla ya kuirusha hewani kama inavyofanyika kwenye filamu.
JINSI WATU WASIO SIKIA WATAKAVYOFAIDIKA NA URUSHWAJI WA HABARI/MAUDHUI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KUBADILI SAUTI KUWA MANENO
Kupata habari kwa usahihi:
Watu wasio sikia na wanaoweza kusoma, wataweza kupata taarifa kwa usahihi kwa kusoma maandishi yatakayokuwa yanaonekana mbele ya kioo cha Televisheni na kuweza kuelewa kinachondelea ulimwenguni kupitia Habari husika.
Kuelimika:
Vipindi mbalimbali hurushwa na Televisheni vyenye lengo la kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali kama usalama barabarani, utambuzi wa maambukizi ya magonjwa na namna ya kujikinga, haki za kijamii kwa makundi mablimbali, elimu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, elimu kuhusu ujasiria mali, elimu kuhusu kilimo na mengineyo. Kwa kutumia Teknolojia hii ya kubadili sauti kuwa maneno itawezesha watu wasio sikia kuelewa vizuri elimu husika inayotolewa kwenye Televisheni na kuwajengea uwezo mzuri wa kuelewa.
Kusaidia kutambua haki zao:
Hili kundi likiweza kuelimika kwa kuhabarishwa kupitia hii teknolojia wataweza kuzitambua na kuzidai haki zao, tofauti na ambapo hawazijui kutokana na kutoelewa kuwa hizi ni haki zao sababu ya kutosikia vizuri.
Kuwa ni watu wenye kujiamini:
Uelewe wa taarifa au mambo sahihi humjengea mtu kujiamini juu yake pia akiwa kwenye jamii, kitendo cha hili kundi kuelewa taarifa wanazopata litawajengea hali ya kujiamni na kuwafanya ni wenye kufanya maamuzi sahihi na kutoogopa kutokana na wasiwasi endapo wangekuwa hawana uelewa wa taarifa au jambo fulani.
Kuhamasika kushiriki mambo ya kijamii:
Watu wasio sikia wataweza kuhamasika kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii kutokana na kupata taarifa sahihi zinazowajengea uwezo na hamasa ya kutaka kujua zaidi mambo mengi katika jamii, hivyo kuwafanya washiriki kikamilifu hasa katika kutoa maoni yao. Pia katika suala la kutambua sera nzuri nyakati za chaguzi ambapo vipindi na matangazo mengi ya kampeni huwa yanarushwa katika Luninga litawahamasisha kushiriki katika kuchagua viongozi wao wanaowataka kulingana na sera badala ya kuangalia sura.
Kuwasaidia kuepuka na msongo wa mawazo:
Kundi hili likipokea taarifa zisizo sahihi zinawajengea hali isiyo nzuri ambayo inaweza kupelekea kuwa na msongo wa mawazo, endapo wakipata ukweli juu ya taarifa hizo kama ni sahihi au sio sahihi kupitia vyombo vya habari katika matangazo au vipindi vya kuelimisha, fikra zao zitabadilika na kuwaepusha na msongo wa mawazo ambao wanaweza kuupata kutokana na taarifa potofu. Pia itawasaidia kujikinga na tatizo la Afya ya akili ambalo lingetokana na msongo wa mawazo.
Kuwaepusha na unyanyasaji wa kijinsia:
Unyanyasaji wa kijinsia umekuwa ni janga katika jamii ambalo linakumba makundi mbalimbali huku makundi ya walemavu na Watoto wakiwa wahanga. Kuwa na taarifa sahihi na uelewa wa mambo kwa walemavu wasio sikia kupitia kupata taarifa sahihi na kuzielewa kutoka kwa vyombo vya habari vya televisheni kutawawezesha kuepuka na vitendo vya unyanyasaji kwani wataweza kuchukua hatua kwa kuripoti au kushirikiana na watu wengine katika kudhibiti vitendo hivyo.
Kuburudika:
Vyombo vya habari vinatoa burudani kwa watu wote, ikiwa ni pamoja na wale wenye ulemavu wa kusikia, kupitia vipindi vyenye maudhui ya filamu, maigizo, vichekesho vyenye kubadilishwa sauti kuwa maneno, maudhui yataeleweka vizuri kwa watu wasio sikia na hatimaye kupata burudani sawa na watu wanaosikia. Burudani itaimarisha afya zao kwa kuwapunguzia msongo wa mawazo, kuwafanya wawe wabunifu kutokana na elimu kupitia burudani wanayoilewa.
WITO KWA SERIKALI KUPITIA WIZARA YA HABARI NA TEKNOLOJIA YA HABARI:
Serikali iviwezeshe vyombo vya Habari hasa Televisheni za Umma (kwa kuanzia) ili waweze kupata hii Teknolojia na kuanza kuitumia ili kuziba gebu hili katika jamii, na hatimaye kuchochea ushiriki katika maendeleo kwa wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo kundi hili la wasio sikia

KIELELEZO: TBC wakiendesha kipindi kikitafsiriwa kwa ALAMA kuwawezesha wasio sikia kuelewa(angalia mshale kwenye picha)
CHANZO: TBC online YouTube Channel
CHANZO: TBC online YouTube Channel
Hatua hii ni nzuri lakini bado ina changamoto kwani sio rahisi kuelewa kwa ufasaha na sio wote ambao hawasikii vizuri ni wenye kujua lugha ya ALAMA kwa sababu wapo wanaopoteza usikivu wakiwa wakubwa na ambao tayari wanajua kusoma maandishi kama kawaida.
Pia mtindo wa kuwekea video, picha maneno(CAPTION) ambao ndio umekuwa maarufu sana kwa sasa kwenye vyombo vya Habari hasa Televisheni, Televisheni za Mitandaoni, Video (Clips) huku ukifuatiwa na maelezo ya sauti kwa kina kuhusu picha, video husika unawaacha hawa watu bila kuelewa nini kimezungumzwa kwa kina.
Ili kutoacha hili kundi nyuma katika kuhabarisha, vyombo vya Habari vyote vinavyorusha maudhui/Habari hasa TELEVISHENI, TV za Mitandaoni nendeni mbali zaidi kwenye ubunifu, tumieni Teknolojia ya Kubadili sauti na kuwa maneno ambayo yatakuwa yanaonekana moja kwa moja mbele ya kioo cha Televisheni pindi mtangazaji anapotangaza/kusoma Habari.
KIELELEZO: Rais wa Bank ya Dunia, Ajay Banga akihutubia Mkutano, Mwaka 2023, Marrakesh, Morocco, hotuba ikiwa inaoneshwa kwa maneno moja kwa moja kwenye screen(angalia maneno meupe kwa chini)
CHANZO: World Bank YouTube Channel

Upvote
2