SoC02 Vyombo vya Habari na sheria nchini Tanzania tasnia ya habari kwa hapa nchini Tanzania inakuwa kwa kiwango kikubwa sana. Tofauti na zamani

SoC02 Vyombo vya Habari na sheria nchini Tanzania tasnia ya habari kwa hapa nchini Tanzania inakuwa kwa kiwango kikubwa sana. Tofauti na zamani

Stories of Change - 2022 Competition

Nadyaabuukiriwe

New Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
1
Reaction score
0
VYOMBO VYA HABARI NA SHERIA NCHINI TANZANIA
Tasnia ya habari kwa hapa nchini Tanzania inakuwa kwa kiwango kikubwa sana. Tofauti na zamani, vyanzo vya habari vikuu vilikuwa ni Televisheni, Redio na Magazeti. Ila kutokana na ukuaji wa teknolojia na utandawazi kwasasa kuna vyanzo vya habari vya mitandaoni kama vile Televisheni za mitandaoni pamoja na mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook nk.

Ibara ya kumi na nane(18) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina sema kuwa kila mtu anayo haki ya kuzungumza na kujieleza juu ya maoni yake.

Kila raia anayo haki ya kupewa tarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi.

Hii inaonyesha kuwa umuhimu wa habari kwenye jamii yetu ni mkubwa na unatija kwenye maisha ya kila siku wa binaadamu.

Nchini Tanzania kuna sheria mbalimbali zinazo ongoza tasnia ya habari kwa ujumla. Kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa kuna sheria mbalimbali zilizotungwa ambazo zinaongoza vyombo vya habri hapa nchini.

Sheria ya kwanza, ni Sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016, sheria ya uhalifu wa mitandao 2015, sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, ikiwa imefanyiwa marekebisho mwaka 2019, Sheria ya upatikanaji wa habari ya mwaka 2016, Sheria ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003 na Sheria ya habari mtandaoni ya mwaka 2020.

Lengo la kuwepo sheria hizi ni kuongoza tasnia ya vyombo vya habari katika viwango vya kifanisi zaidi. Pia kuwa kichocheo cha watu waliopo ndani ya tasnia hii, kuwa na nidhamu na kutokeuka maadili ya kazi.

Kutokana na ukuaji wa teknolojia na utandawazi kwa kasi duniani na hapa nchini, imekuwa chachu ya ukuaji wa tasnia ya habari kwa hapa Tanzania. Kwasasa habari husambaa kwa kasi na kuweza kufika maeneo mbalimbali, kupitia runinga na simu janja za mikononi almaarufu(Smart phone).

Baadhi ya vyombo vya habari hutumia maudhui yasiyo na viwango na yasiyo ridhisha katika kufikisha ujumbe.

Kutokuwepo kwa matumizi ya lugha fasaha huleta utata na mkanganyiko kwa hadhira. Vilevile kutumia lugha zaidi ya moja katika kutoa habari pia ni jambo si sahihi kufanya na ukizingatia kuwa hadhira ni ya kila mwananchi kwa aliye na elimu na asiye na elimu.

Mfano; aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Samwillu Mwafisi wakati wa kongamano la idhaa ya Kiswahili duniani aliwaasa waandishi wa habari kutekeleza jukumu lao lakuzungumza lugha fasaha ya Kiswahili ili wananchi waweze kujifunza kutoka kwenu.

Uhalali wa vyombo vya habari imekuwa ni tatizo. Vyanzo vingi vya habari vimekuwa vikifanya kazi pasipo kujulikana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) inayo sajili vyombo vya habari hapa nchini. Hii imepelekea kufungwa kwa vyanzo vingi vya habari hususani ni vile vya mitandaoni.

Maudhui yanayo chapishwa na vyombo vya habari hayakidhi viwango, na yanakiuka taratibu zilizo ainishwa na Sheria ya vyombo vya habari Tanzania. Hi inasababishwa na kuwepo na waandishi wa habari wasio kidhi viwango na kukosa elimu juu ya maswala ya uandishi na taratibu zake.

Sheria imetengenezwa ili kuongoza vyombo vya habari na kulinda ukiukwaji wa taratibu zilizoainishwa kwenye sheria. Pia kulinda haki na usalama wa wananchi pamoja na waandishi wa habari.

Endapo mtu au watu wataumizwa kwa nanna yeyote na maudhi yaliyo chapishwa juu yake anayo Haki ya kwenda kushtaki mahali panapostahiki. Na Sheria zinaelezea juu ya makosa yatayo fanywa na muandishi au chombo Cha habari ikiwemo udhalilishaji kwa njia ya mitandao au michoro au kumtaja muhusika kwa jina, kuchapisha takwimu zisizo na uhakika na kuondoa amani kwa wananchi kupita machapisho yao, kuwa ni kosa kisheria na watawajibishwa kwa makosa yao.

Hivyo basi ni muhimu kwa waandishi na wahusika wa vyombo vya habari mbalimbali, kuwa na elimu juu ya taaluma yao, kusajili vyombo vyao vya habari kama inayohitajika kisheria, kuhakikisha kuwa maudhui yanayo chapishwa kukidhi viwango husika.
Ni muhimu kuzingatia pia ufanyaji kazi wao kuwa na uhuru bila kuingiliwa na kuwekewa vikwazo vitavyo wazuia wao kufanya kazi kwa ufasaha.

Vyombo vya habari hutumika kama daraja la kusambaza na kufikisha habari kwa wananchi, hivyo basi wafanyaji kazi wa tasnia hii hutizamwa zaidi na jamii. Ni muhimu kuhakikisha kuto kukiuka maadili ya jamii husika kwani kwakufanya hivyo hutengeneza taswaira isiyofaa katika jamii, na kuleta mtazomo hasi juu ya kazi zinazo husiana na tasnia ya habari kama vile kuonekana kama kazi isiyofaa na kuchukuliwa kama sio kazi ya muhimu.

Baraza la habari Tanzania(MCT), ni chombo kinachosimamia maadili ya wanahabari hapa nchini. Vile vile sheria zinalinda taswira ya chombo hiki kwa kuweka vifungu vya adhabu kwa watu ambao watakwenda kinyume na taratibu zilizopo kwenye mamlaka husika.

Hivyo basi ni muhimu sana kwa jamii iliopo kwenye tasnia ya habari hapa Tanzania kupata elimu zaidi juu ya kazi zao. Kwani vyombo vya habari vina cheza nafasi kubwa sana hapa duniani, vina nguvu ya kuchochea Amani,kusambaza habari..n.k.

Na kwaupande wa sheria ni muhimu kuhakikisha kuwa haki za wanahabari na Tasnia kwa ujumla zina lindwa na kusimamiwa inavyostahiki, kwakufanya hivyo inatengeneza mahusiano bora kati ya Tasnia ya habari na wasimamizi wa sheria.

AHSANTE SANA
 

Attachments

Upvote 0
Back
Top Bottom