Vyombo vya Habari Tanzania acheni upendeleo kwa chama tawala, Mtaligawa taifa? Hivi hamuelewi?

Vyombo vya Habari Tanzania acheni upendeleo kwa chama tawala, Mtaligawa taifa? Hivi hamuelewi?

tusha, unfollow, dogo kiazi sana yule, bora tuhamie jf tu ndio kuko huru
Mimi wanafiki wote sitaki hata kuwasikia. Hadi kufikia mwaka jana nilikuwa mfuatiliaji na msikilizaji mzuri wa WAPO radio na mahubiri ya Askofu Gamanywa. Baada ya kuuelewa Unafiki wake siisikilizi tena hiyo radio wala Magazeti ya Msemakweli sitaki hata kuyaona kwenye macho yangu
 
siku za MILLARD AYO zinahesabika, huyu dogo wa pale akheri meru , haya kampeni ya ku-unfollow kwenye youtube, insta na fb ianze mara moja

Mbona Membe alioneshwa na aliongea na hakuna shida?
 
[SUP]Naunga mkono mengi uliyo sema ila nimeduwaa kusikia unasema BBC, CNN na DW wako balanced. Hivyo vyombo vya habari ni vya hovyo sijapata kuona. Nashangaa Sana hata upinzani kutangazwa sana na hizo media. Maana halisi ya vyombo vya habari vilivyo biased Ni hivyo. Ongeza hapo MSNBC, NBC, RT ABC na vingine vingi.[/SUP]
 
Kalipieni pesa za air time acheni ubahili Vyombo vya habari kuviendesha
 
Niliwahi kuwaambia siku zilizo pita kuwa kwa Lissu kuwa Presidential Candidate na vile lopolopo bila kujali implications za lopolopo zake mpaka uchaguzi unaisha chadema itakuwa imepigika sana. Vyombo vya habari havitaki vitumike kama speaker zinazotumiwa na Lissu kumtukana Mkulu, na hata vikifanya hivyo Lissu ama Chadema hawata wasaidia kuwalipa faini au gharama kufungiwa. Kwa hali hiyo vyombo vya habari vinachukua tahadhali kubwa kurusha live habari za chama cha Mbowe.
 
Nimejaribu kufuatilia jinsi coverage unavyofanywa na hizi local media zetu kuhusu matukio mbali mbali yanayofanywa na chama tawala CCM, hakika inasikitisha. Hakuna balance kabisa kwenye matukio ya kisiasa kati ya chama tawala na Upinzani.

Hivi vyombo vimeamua kua upande wa Chama Tawala hata kwenye urushaji habari na matangazo ya live, hili liko wazi na kila mmoja analijua. Mnataka mpaka mualikwe kwani kazi yenu si kutafuta matukio? Hii kwangu aiona kama ni aibu kubwa.

Hivi taaluma za waandishi wa habari wanazozisema ziko wapi? Tulizoea ITV ilikuwa balanced kwenye taarifa zake lakini kwa sasa ninashangaa sana kwa yanayoendelea. Haya ambayo miaka yote mmekuwa mkiyaripoti leo hii imekua ni uchochezi?

AZAM media na MillardAyo mnalalamikiwa sana na umma kuwa mmefuta taarifa za Mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu wakati akichukua form toka NEC kwenye mitandao yenu kwa sababu gani?

Toeni notifications kwa Umma ni kwanini mmefanya hivyo kwa wakati mmoja kama ni kweli?

Vyombo vya habari ni muhimu mwingine muhimu sana wa taifa, sasa mkiendelea hivi mtakosa credibility ya kuaminiwa na jamii. Iangalie ni CNN na BBC au DW kunapokuwa na matukio ya kisiasa nchini mwao wanavyokua balanced.
hawajaripoti habari gani kwani?
 
Back
Top Bottom