Vyombo vya Habari Tanzania imarisheni 'Maslahi' kwa Waandishi wenu ili wasiwe wanang'ang'ania ziara za Wakubwa zinazowauwa kwa ajili ya Posho

Vyombo vya Habari Tanzania imarisheni 'Maslahi' kwa Waandishi wenu ili wasiwe wanang'ang'ania ziara za Wakubwa zinazowauwa kwa ajili ya Posho

Mkuu nayajua yote haya na hata na mengineyo kwani nimeshapita huko ( humo ) miaka ya nyuma na ndiyo maana leo nimeamua niwaambie ( niwachane ) huu Ukweli ili tubadilike ( wabadilike )
Bahati mbaya kumekuwa na vifo kadhaa kwa mfululizo vya waandishi wa habari kwenye hii misafara sielewi kwa nini 🤷
 
Bahati mbaya kumekuwa na vifo kadhaa kwa mfululizo vya waandishi wa habari kwenye hii misafara sielewi kwa nini 🤷
Waganga wa Kienyeji huwapenda na Kafara za kutafuta Mafanikio ( ya Uongozi, Mamlaka na Utajiri ) zikielekezwa Kwao huwa na Matokeo Chanya kwa Wahusika.
 
Nakuunga mkono mkuu,hatuongei kwa ubaya..
Nilikuwa nafanya kazi kama fundi wa kituo fulani cha redio kinachomilikiwa na chuo kikuu fulani hapa mkoani kwetu..

Asee njaa mbaya, ikitokea kuna ugeni wa kiongozi fulani au professor fulani anapresent thesis yake ambapo waandishi wa habari inabidi waripoti ndipo majanga yanapoanza, majungu, kujipendekeza sometimes mpaka kushikana mashati.

Imagine hyo ni ndani ya taasisi kubwa tena ya wasomi, vipi huku changanyikeni!!!!!.
Unayoyaongea ni kweli tupu, inafika hatua hadi wanajidhalilisha. Malipo nayo yamekuwa kidogo hivyo wanaona bora kuhombania bahasha
 
Back
Top Bottom