kilaza mjanja
JF-Expert Member
- Jun 2, 2016
- 654
- 1,144
Taarifa zilizotufikia punde ni kuwa baadhi ya vyombo vya kimataifa hasa vya nchi za magharibi na mashariki ya mbali vimeanza kuwasili nchini ili kushuhudia tukio kubwa la kitaifa linalotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi unao kuja (Sept 1)
Uchunguzi uliofanywa na mchunguzi wetu unaeleza wazi kuwa vyombo hivyo vya habari vya kimataifa (CNN, BBC, SBBC, CCTV ALJAZERA, RT) vimewasili nchini baada ya taarifa zilizoripotiwa na ubalozi wa Marekani kwa raia wake ambapo imeelezwa kwamba taarifa za kijasusi zinasema kunaweza kutokea maandamano makubwa yanayoweza kupelekea mapigano na uvunjifu wa amani.
Pia wapo wachunguzi wengine wanasema maandamano haya yanasukumwa na baadhi ya mataifa yenye nguvu za ushawishi duniani.
Ikumbukwe kwamba vyama vya upinzani nchini vimeandaa maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika Sept 1 kama yalivyopangwa huku kukiwa na mivutano mikubwa na serikali ambapo madai ya wapinzani yanahusisha serikali kukiuka katiba.
Source: Afisa uhamiaji (uwanja wa ndege JKNIA)
MY TAKE
Kwa mjibu wa nyaraka za MOSSAD, CIA, RAW na FSB juu ya elimu ihusuyo "kiwango cha hali ya hatari katika eneo la kiraia" ambacho hupimwa kwa kipimo kiitwacho Def Cond, inasema, "Pale majadiliano ya meza yanaposhindwa kuleta jibu chanya, wanamjadala hususia meza, ambapo katika kipimo husomeka Def Cond 0001".
Ikitokea kuwa hata huko walikoamua wanamjadala hao kupeleka hisia zao nako kukazuiwa, hasira ya wanamjadala hao huongezeka na kuwa Def Cond 0002. Hatua ya mwisho ya wanamjadala hawa huwa ni kwenda kwenye mahakama ya umma, hapa kipimo husomeka Def Cond 0003.
Hiki ni kipimo kikubwa katika medani ya kiusalama kwa mambo ya ndani, ambapo matokeo yake shughuli katika jamii husimama, serikali hushindwa kutawala wala kuongoza. Katika lugha nyingine huitwa mgogoro wa ndani,kisiasa,kikatiba nk...
Zingatia hali hii haizai vita, kwani ili vita kamili ya ndani izaliwe lazima hali ya hatari isomeki Def Cond 0006. Na ili vita kamili izaliwe katika ya taifa na taifa lazima hali ya hatari isomeke Def Cond 0008.
Ulimi ndio silaha izaayo vita, na ulimi ndio silaha imalizayo vita... Hakuna silaha kubwa duniani kama Ulimi wa binadamu.