Vyombo vya Usalama vinaweza kufuatilia mawasiliano kwa kibali halali

Tigo Sasa waseme walimpanani taarifa za mteja wao Lissu.
Pia tujue walitoa taarifa zake kwakuwa alikuwa gaidi ama Kwa grounds zipi?
Baada ya kugundua mteja wao anayefuatiliwa kapigwa risasi na wasiojulikana wao hatua gani walichukuwa kusaidiwa polisi kwani walitoa taarifa zake mahali na wanajua.
Nawe ni watigo? Maana tigo ni matigo kweli na lazima waliwe hawa tigo.
 
Hii ndiyo nini...?

Fafanua ili tukuelewe. Kwanini unaokoteza vijitaarifa nusunusu kisha una copy na ku - paste tu bila maelezo....?

Au wewe ndiye Cyprian Musiba aliyeshindwa kutetea hoja hii akiwa kwenye live TV camera kama unavyohangaika wewe?

Eleza, huyo "Home Scretary Sir John Simon alitoa order hiyo kwa kutumia parameters zipi? Katika misingi ya kisheria au kienyeji tu kama Magufuli kwa Lissu 2017?

Fafanua ili tukusaidie kukujengea ufahamu wa mambo hayo utoke kwenye ujinga uwe mwerevu...
 
Tukikuacha unaona unajua sana - please leave your ego at the door
 
Kwa hiyo haki ya faragha (Privacy) haipo tena kwa mtu siku hizi ?
 
Yaani as long as hizi pillars tatu hazipo balanced 😔 hili jambo litaendelea kuwasumbua sana watu wenye mawazo tofauti na CCM!
Mahakama na Bunge vyote vinamtazama Rais wasije kupishana.
 
Toa precedent mkuu. Kesi ya Boniface ndo ulinganishe na tuhuma za kushirikiana na magaidi, ama kufanya espionage, ama uhujumu uchumi???.... Tupe precedent ya mambo unayosema
 
Toa precedent mkuu. Kesi ya Boniface ndo ulinganishe na tuhuma za kushirikiana na magaidi, ama kufanya espionage, ama uhujumu uchumi???.... Tupe precedent ya mambo unayosema

..wewe huna uelewa wa kutosha ktk mada uliyoiwasilisha.

..na inaelekea hauko tayari kupokea elimu hiyo toka kwa wachangiaji waliyonayo.
 
Tukikuacha unaona unajua sana - please leave your ego at the door
Sikiliza ndugu comte, mimi ninajua, nina ufahamu na uelewa kutokana shule niliyonayo, sina "negative ego" ndani yangu. Kama umeiona, basi ni "positive ego...."

Wewe ndiye hasa "empty set" kichwani. Unachofanya ni ulaghai wa ki-maarifa. Unasambaza uongo wako, ufahamu wako fake just to fool people..

We can't be fooled by a person like you...
 
KWANZA; Pole sana kwa kuwa umejitwisha mzigo mzito mwenyewe bila sababu huku ukijua kabisa huuwezi kuubeba matokeo yake umekulemea na unataka kukuvunja mgongo.....

PILI; Umepewa kazi ngumu (au umejipa mwenyewe) kufanya propaganda ya kisiasa kutetea uovu na mauaji. Bahati mbaya sana kwako ni kuwa umechagua eneo usiloliweza kufanyia propaganda zako hizo kwa sababu huna ufahamu nalo hata kwa 20% tu ndiyo maana unayumba na kujikanyaga kanyaga hovyo usielewe ujibu nini....
Toa precedent mkuu..
Unataka precedent wakati sheria iko wazi na unaweza kuisoma na kuielewa? Au na hilo ni tatizo kwako? Ipi iko juu "precedent" au "sheria ya makosa ya jinai yenyewe" + "katiba ya nchi...?"
Kesi ya Boniface ndo ulinganishe na tuhuma za kushirikiana na magaidi, ama kufanya espionage, ama uhujumu uchumi???....
Unam - refer nani hapa? Nani ana kesi ya ugaidi, espionage na uhujumu uchumi? Unaelewa maana ya neno "ugaidi" na "gaidi?"

I think this is another proof that, najadiluana na mtu very ignorant wa mambo haya lakini yeye anafikiri anajua...!
Tupe precedent ya mambo unayosema
Mambo gani ninayosema mwanasheria wa UVCCM?

Jaribu kuwa precise & specific ili usaidiwe kupata ufahamu wa bure...!
 
Unataka precedent wakati sheria iko wazi na unaweza kuisoma na kuielewa? Au na hilo ni tatizo kwako? Ipi iko juu "precedent" au "sheria ya makosa ya jinai yenyewe" + "katiba ya nchi...?"
Nimesoma mpaka mwisho sijaona precedent yoyote.. Nafikiri ni safe kusema hauna. Nitakuelewa.
 
Mimi siyo mwanasheria lkn najua unaweza kuliko bunduki na kuitumia kwa kuzingatia taratibu. Hata Sheria ya kunyonga IPO lkn ina vigezo siyo MAELEKEZO yoyote tuu! Okay???
 
Unam - refer nani hapa? Nani ana kesi ya ugaidi, espionage na uhujumu uchumi? Unaelewa maana ya neno "ugaidi" na "gaidi?"

I think this is another proof that, najadiluana na mtu very ignorant wa mambo haya lakini yeye anafikiri anajua...!
Hypothethically, Palm beach anashukiwa kushirikiana na Alshabaab. Inabidi kufuatilia mawasiliano yake. Katika scenario kama hii, na kwa thesis yako, nani ataomba kibali wapi, na kinatolewaje na kikishatolewa kinapaswa kufahamika kwa nani? Kinatangazwa hadharani???
 
Duuh🤔🤔🤔🤔..

Hivi wewe unajua hata unachoandika kweli...?

Ishara zote zaonesha kuwa, umeshasahau hata hoja yako uliyoianzisha mwenyewe...

You're completely off the track dude...!!!!

Mbona kadiri ninavyojaribu kukusogeza kufungua ufahamu wako, ndivyo unavyozidi kukimbia na kutokomea na kuwa mjinga zaidi na zaidi tu...??

What's your problem brother...?
 
Naomba majibu... Acha janjajanja. Toa jibu hapo tuone
 
Kwa hiyo ukifahamu kama mtu anawasiliana na alishabab ( tuchukulie mfano lisu alikuwa anawasiliana na alshabab).
Kwa hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu zetu ikigundulika kama mtu anawasiliana na alshabab serikali inaamua ina tuma watu wampige risasi?
Kuna watu mna very poor reasoning and argumentation
 
Hoja ni kufuatilia mawasiliano 'survailance' . Hayo mengine mnaongeza wenyewe kwa mapenzi yenu. Siyo hoja yangu
 
Lissu alilijibu SWALI hilo kwa kumwambia ni mpaka hati ya mahakama ipatikane ndipo mawasiliano yanaweza kuchunguzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…