RESOLVED KERO Vyoo vya Shule ya Msingi Miembeni iliyopo Manispaa ya Songea (Ruvuma) ni hatari kwa Wanafunzi

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2025-05-25 at 17.41.01_7afc48ca.jpg
Muonekano wa Vyoo vya Shule ya Msingi Miembeni iliyoko Kata ya Msamala Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ni wa kusikitisha na unatia hofu kwa afya za Wanafunzi.

Vyoo hivyo ni vichafu kupita maelezo, kila tundu limejaa kinyesi na hali ya usafi ni duni, kwani harufu ni kali sana inayotoka kwenye vyoo hivyo.

Kukosekana kwa matunzo ya vyoo na usimamizi wa usafi kumeifanya shule hiyo kuwa katika hatari ya kukumbwa na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu na minyoo.
WhatsApp Image 2025-05-25 at 17.40.59_032f280d.jpg

WhatsApp Image 2025-05-25 at 17.40.59_4a810274.jpg

WhatsApp Image 2025-05-25 at 17.41.02_d56db5b5.jpg

Pia soma ~ Vyoo vya Shule ya Msingi Miembeni iliyoko Kata ya Msamala Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma vyafanyiwa usafi
 
Vyoo hivyo ni vichafu kupita maelezo, kila tundu limejaa kinyesi na hali ya usafi ni duni, kwani harufu ni kali sana inayotoka kwenye vyoo hivyo.
Tunawaweka hatarini watoto wetu huko mashuleni, ukizingatia hizi mvua vipindupindu ni kugusa tu
 
waliojenga vyoo vya stahili hiyo ndio wakulaumiwa..kwa watoto wa shule ya msingi kulingana na akili zao wangewekewa vyoo vya shimo vyenye tundu dogo..ila hivyo vya hapo pichani vinahitaji usafi wa hali ya juu ikiwemo maji mengi hivyo vinawafaa sana wanafunzi wa secondary kidogo wamekua kiakili..ila kuwawekea vyoo vya sink watoto wa primary wasiojua kujiongeza wamebugi
 
Muonekano wa Vyoo vya Shule ya Msingi Miembeni iliyoko Kata ya Msamala Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ni wa kusikitisha na unatia hofu kwa afya za Wanafunzi.

Vyoo hivyo ni vichafu kupita maelezo, kila tundu limejaa kinyesi na hali ya usafi ni duni, kwani harufu ni kali sana inayotoka kwenye vyoo hivyo.

Kukosekana kwa matunzo ya vyoo na usimamizi wa usafi kumeifanya shule hiyo kuwa katika hatari ya kukumbwa na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu na minyoo.
Inasikitisha sana maana watoto wetu kila wakati wanaugua UTI
 
Back
Top Bottom