Vyuo vya Kisabato na degree ya sheria

Vyuo vya Kisabato na degree ya sheria

Mkuu unataka uletewe katekism?

Mwishowe utaambiwa we Jesuits!
Hahahahahah, mkuu haukuona kule alivyotupangia decree ya Artashasta, lakini sheria za Wamedi na Waajemi isiyobadilika yupo fit...
 
Unajua mimi sikujua kuna vita baridi humu, watu wanaleta udini na huwa sipendi kabisa kukashifu, kuongea na kudharau kile anachoamini mwenzangu..!
Sijui Eiyer alikusudia nini lakini ikiwa ni kwa ajili ya kukashifu, atakuwa amepungukiwa sana..

Sio kukashifu...Na wala Eiyer hajaleta mjadala kwania ya kukashifu...mimi nimefunguka kwa jinsi nilivyosoma source mbalimbali...Huu ni mjada huru ...mwengine anaweza kusema ni kwanini Wasabato hawasomi LL.B....Mimi nimeeleza kwa upande wangu..
 
Ndio maana mnaambiwa, kama hujui uliza, kama hutaki kuuliza basi kaa kimya. Ukiongea hivyo unaonekana wa ajabu.
heela, m'bwange ukundie masa wee, una makombere sana avae, haya sema wewe basi.
 
Wakuu,

Jana nilijuwa na jamaa zangu na niliwauliza kuhusu chuo kizuri cha sheria kwakuwa kuna jamaa yangu anahitaji

Katika mazungumzo hayo kuna jamaa alitaja chuo kumoja cha kisabato ndipo jamaa yetu akasema kuwa vyuo vya kisabato havitoi degree hiyo kwasababu ya kidini,nilishangaa

Bahati mbaya pale hakukuwa na mtu mwenye majibu sahihi ya maswali yangu,naombeni mnijuze kama hili lina ukweli na kama ni kweli ni kwanini

Karibuni Ntuzu Ishmael Mkuu wa chuo charminglady Basluma Original Otorong'ong'o Nkwesa Makambo Lisa Valentine na wengine ...

Naombeni Wasabato mchimbe ni kwann mlikuwa hamsomi(Ila sijui kama hata leo vyuo vyenu mnasoma Law)kama kuna watu Wasabato wameamua kusoma Law ni kwa mapenzi yao ila Kikanisa ni kosa na nikama Umeamua kufanya kazi siku ya Jumamosi...

kumbuka huwa hamvai pete kwa wanandoa kisa eti ni utamaduni wa Kikatoliki na Rumi...Lol....Trend ni hiyo hiyo hata katika LL.B

Mleta mada nafikiri unajua majukumu ya mwanasheria. Sheria za duniani na hukumu zake kwa mungu hazikubaliki, nikupe mfano mdogo katika biblia kuna sheria 'usiue' ikaishia hapo, na ukiua umetenda dhambi. Tukija kidunia nayo pia hii sheria ipo lakini inawezatokea mtu akapitikan hana hatia eti ameua bila kukuksudia mtu huyu akawa huru kitu ambacho sio sahihi mbele za mungu. Mtu akikusaea saba mara sabini samehe, mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na lakulia kwa mantiki hiyo huyo mtu anaye ua na kuonekana hakukusudia ameua kwa ruhusa ya nani? watu wanatakiwa kupendana na kuheshimiana pia kuzitii amri za Mungu mtu akikosea mwenye kutoa hukumu ni Mungu sio mwanadamu.
kifupi kuwa mwanasheria unakaribisha dhambi maana hutaweza kutenda haki kwakiwango anchotaka Mungu, mashahidi wenyewe ni waongo, rushwa imetawala na haki ya mtu inanunuliwa kwa pesa. Kazi sio sheria tu zipo nyingine tena za kumpendeza MUNGU.
 
Endelea kuchunguza maandiko ili upate maarifa na sio kupotosha umma.

Nichunguze kwa mujibu na muongozo wa nani...??? Usije ukaniambie nichunguze kwa mujibu wa LESSOn na manuscript za Hellena White, please...
 
Good.....Yap yap hapa sasa ndo patamu...Licha ya hayo yote ishu nzima ni hapo kwenye CANON LAW....
Ntuzu alikuwa haamini...Haya sasa..



Niwapi nimesema naamini au siamini? Mbona wewe unapenda sn kusema uongo???? Unajua ni kwanini sijaendelea kutoa maoni yangu juu ya hili swala?

Acha ujinga weye..... Huna hoja ile unayoweza kuoffer Zaidi ya lugha chafu na uongo km hue...!
 
Last edited by a moderator:
hakuna kitu kinanikwaza niwapo church kuona ada za UoA kuwa ni za juu kupita maelezo.... yaani hiki chuo hata sielewi mtoto wa maskini wanamsaidiaje?????? huwa naumia sana. samahani sana kutoka nje ya maada
 
wasabato hawawezi kuwa na idea ya kuwa na chuo kiuu,wao wanajua tu biblia na kubishana kuhusu hiyo biblia


Punguza jaziba kidogo basi hata kama wasabato hukubaliani nao. Vinginevyo utaonekana wa ajabu. Kwanini kutoa hitimisho pasipo kutafiti kwanza?
 
Nichunguze kwa mujibu na muongozo wa nani...??? Usije ukaniambie nichunguze kwa mujibu wa LESSOn na manuscript za Hellena White, please...

Ujue haki inavopatikana kidunia na pia kwa Mungu, sheria za dunia zinavyotofautiana na za Mungu.
 
hakuna kitu kinanikwaza niwapo church kuona ada za UoA kuwa ni za juu kupita maelezo.... yaani hiki chuo hata sielewi mtoto wa maskini wanamsaidiaje?????? huwa naumia sana. samahani sana kutoka nje ya maada

Hujui ukiwa hapo unapata extra education ya kiroho kulinganisha na vyuo vingine? product ya hapo sio mafisadi ukilinganisha na vyuo vingine.
 
Ok mkuu...

Lkn hebu tuangalie haya malengo km yanafaa mbele ya Bwana....! Yesu alipokua hapa duniani ktk huduma zake alikua akifundisha kuokoa roho na kuponya mwili...
Sasa km malengo ya vyuo vya kisabato ni kumpatia mtu maarifa ambao ndio mwili na kuponya roho ambapo atajifunza neno la Mungu, kuna ubaya gani mkuu? Na tujiulize sheria km sheria ina nafasi gani ktk ulimwengu wa kiroho wakati katiba au sheria kuu neno la Mungu tunalo tayari?

Haya ni maoni yangu na Mimi nafatilia kujua kwanini hawatoi sheria ktk vyuo.

Ukishamwingiza Yesu tu utaharibu thread. Ngoja funza wa Mwamedi waje..
 
Ok mkuu...

Lkn hebu tuangalie haya malengo km yanafaa mbele ya Bwana....! Yesu alipokua hapa duniani ktk huduma zake alikua akifundisha kuokoa roho na kuponya mwili... .

Ukishamwingiza Yesu tu utaharibu thread. Ngoja funza wa Mwamedi waje..
 
Kama Kuna ukweli, Kuna sehemu wameteleza kwa sababu
1. Waumini Wao wanasoma sheria, wengi nawafahamu, mfano mzuri Kuna baadhi walifukuzwa SAUT kwa kutofanya mtihani siku ya jmosi.
2. Tunaishi katika dunia ambayo Kuna imani mbalimbali tena zisizofanana, Na wakati huohuo tunashirikiana vitu mbalimbali, je Ni kitu gani ambacho kitaleti uniformity Kama siyo sheria?.
3. Sheria za Mungu (amri 10) naamini hakina dini wala imani inayozipinga, tena zimewekwa katika sheria za nchi kwa namna nyingine (has been accommodated)
4. Hizo sheria wanazozikataa je wanakataa kwakuwa Ni mbaya au?, je Ni sheria gani inayokinzana Na maagizo ya Mungu, (wasabato waje Ku justify hapa)
5. Je, msabato akiwa na tatizo haendi mahakamani kwa ajili ya kupata msaada?
6. Vipi kuhusu kada zingine za elimu, mfano sayansi ambayo ukiofuatilia kwa karibu ndo utakuta inapinga imani zetu, Kama vile historia ya mwanadamu n.k. Je hawafundishi nazo?

Binafsi nahisi kutoweka sheria Kama somo kwenye vtuo vyao its just a coincidence and not a plan, so ipo siku wataweka.
 
Mbona vyuo vya kukatoliki vinalazimisha watu kufanya mitihani jmosi na wakikataa hufukuzwa? Hili mbona hawalihoji mbali na kwamba linakiuka haki za binadamu? Si bure ipo namna

Mkuu, kwanza Chuo hakikulazimishi wewe usome kitu flani ndani ya siku flani, ningependa uufute kabisa huo mtazamo wako kwanza,
Fahamu kwanza utaratibu WA Chuo umewekwa kabla hata ya mwanafunzi kwenda hapo chuoni, Na hata kwenye sekta nyingine Ni vivyo hivyo, Na hauwezi kubadilishwa Na kitu kimoja kikaathiri wengi kwa sababu ya interest zako, kwa ifupi Chuo kinapopanga ratiba fulani huwa hawaangalii Ni nani muislam au mkristu kwa sababu like siyo suala la dini, kinachoangaliwa pale Ni itifaki ya Chuo husika ambayo mwanafunzi lazima aitambue kabla ya kufanya maamuzi ya kujiunga Na Chuo hicho (hapa nazungumzia kile kipindi TCU haijakuwa Na mandate ya kudahili wanafunzi)
...sasa Kama wewe Ni muislam alaf unaenda Chuo cha kinachomilikiwa Na mfumo kristu, ujue Kuna mambo lazma yatabase kwenye ukristu Na Ni lazma uyafuate Kama ukitaka, Na huwezi sema umenyimwa haki.

PIA ifahamike kuwa hata mitihani ya taasisi za elimu zinazomilikiwa Na serikali, huwa Kuna note inawekwa kuwa ratiba haitabadilishwa endapo tarehe ya mtihani itaangukia kwenye sikukuu za kitaifa n.k. (Christmas Na Eid nazo Ni sikukuu za kitaifa) Na hili nimeshalishuhudia Mkwawa University kipindi nipo chini ya UDSM, watu walifanya mtihani siku ya Christmas Na mwaka mpya. So usiwalaumu SAUT maana najua Wao ndo waliwafukuza wanafunzi wa kisabato walipogoma kufanya mtihani siku ya jumamosi.

Na sijui Ni haki gani SAUT waliyoikiuka, je, unaweza itaja? Na ukiitaja ueleze na mipaka ya haki za binaadamu, maana najua haki za binaadamu zina mipaka (check limitations of human rights)

Mfano mzuri Ni shule za kiislam, Kama Thaqaafa pale mwanza Na nyingine uzijuazo, (mdogo wangu Ni mkistu 100% Na kasoma pale, Na Mimi ndo nlikuwa ninampeleka so najua protocal zao hata kabla) hiyo shule wasichana Ni lazima wavae hijab, ambalo nna uhakika Ni vazi la kiislam Na lugha inayotumika Ni English au Arabic, so Na mdogo wangu alivaa na hakuna aliyelalamika. Kwasababu yeye ndiye aliyechagua wakati alikuwa Na options za kwenda shule nyingine tena za kikristu.

Sasa unataka kundi flani la watu wanaoabudu j5 Na Wao jumatano iwe siku ya mapumziko?, Kama Ni hivyo mbona waislam wanafanya mitihani ijumaa Na hawalalamiki?, hilo la wasabato limetoka wapi?, au Wao ndo wana haki zaidi, ukitaka kujibu anza kunijibu kuhusu ijumaa Na waislam kuhusu kufanya kazi Na kwenda mashuleni, then uendelee.

Tafakari.
 
Mkuu, kwanza Chuo hakikulazimishi wewe usome kitu flani ndani ya siku flani, ningependa uufute kabisa huo mtazamo wako kwanza,
Fahamu kwanza utaratibu WA Chuo umewekwa kabla hata ya mwanafunzi kwenda hapo chuoni, Na hats kwenye sekta nyingine Ni vivyo hivyo, Na hauwezi kubadilishwa Na kitu kimoja kikaathiri wengi, kwa ifupi Chuo kinapopanga ratiba fulani huwa hawaangalii Ni nani muislam au mkristu kwa sababu like siyo suala la dini, kinachoangaliwa pale Ni itifaki ya Chuo husika ambayo mwanafunzi lazima aitambue kabla ya kufanya maamuzi ya kujiunga Na Chuo hicho (hapa nazungumzia kile kipindi TCU haijakuwa Na mandate ya kudahili wanafunzi)
...sasa Kama wewe Ni muislam alaf unaenda Chuo cha kinachomilikiwa Na mfumo kristu, ujue Kuna mambo lazma yatabase kwenye ukristu Na Ni lazma uyafuate Kama ukitaka, Na huwezi sema umenyimwa haki.

Mfano mzuri Ni shule za kiislam, Kama Thaqaafa pale mwanza Na nyingine uzijuazo, (mdogo wangu Ni mkistu 100% Na kasoma pale, Na Mimi ndo nlikuwa ninampeleka so najua protocal zao hata kabla) hiyo shule wasichana Ni lazima wavae hijab, Na lugha inayotumika Ni English au Arabic, so Na mdogo wangu alivaa na hakuna aliyelalamika. Kwasababu yeye ndiye aliyechagua wakati alikuwa Na options za kwenda shule nyingine tena za kikristu.

Sasa unataka kundi flani la watu wanaoabudu j5 Na Wao jumatano iwe siku ya mapumziko?, Kama Ni hivyo mbona waislam wanafanya mitihani ijumaa Na hawalalamiki?, hilo la wasabato limetoka wapi?, au Wao ndo wana haki zaidi, ukitaka kujibu anza kunijibu kuhusu ijumaa Na waislam kuhusu kufanya kazi Na kwenda mashuleni, then uendelee.

Tafakari.

huu utetezi wako ni wa kike unangozwa na mihemko zaidi
 
Back
Top Bottom