Vyuo vya Kisabato na degree ya sheria

Vyuo vya Kisabato na degree ya sheria

Last edited by a moderator:
Watu wengi huwa wanakubali chochote tu hata kama hajui....ila kwa mwenye busara angekujibu 'sijui' ili apate muda wa kutaka kujua. Ukweli ni kuwa vyuo vya Kisabato vinafundisha masomo ya sheria tena hata kwenye level za Doctorate...

Kuna msemo....''information is power''

Mkuu,hii program imeanza lini?
 
Wewe ni Msabato?!
Umewahi kupitia kwenye department ya elimu ya kanisa? Vyuo vya kisababato vinatoa degree ya law na legal studies(major)

Chukua muda wako kusoma hapa SDA majors and programs | Adventist Colleges and Universities
Ndio mimi msabato, lakini haimaanishi kuwa nikiwa msababto basi nijue education system ya kanisa coz kuna uwezekana sijawa na interest hiyo au labda fani hiyo haina uelekeo na fani/kazi za kila siku za maisha yangu.

Nilijaribu kuangalia university of arusha jana kweli sikuona hiyo course, na mimi nikaona well, kumbe kweli hatuifundishi kwenye vyuo vyetu...nimesomea sekondari ya kisabato lakini baada ya hapo sijaihusisha na vyuo vyetu tena..!
 
Ila inaonekana wameanza karibuni tu maana kwa wale waliosoma miaka mitano nyuma hawajui hii kitu ....

Kwahiyo inawezekana waligundua wameingizwa chaka na sasa wamejirekebisha ..!!

Mi sioni km hii ni issue sn mpk tufikie kusema kwamba walikua wameingizwa Chaka..... Maana sijawahi kusikia au kuona tukifundishwa Kua kusoma sheria au Kua mwanasheria ni dhambi...!
 
Kuna mwenzako alikubali hapo juu,sijui hao ni wasabato au vipi!
Eiyer, kuna mambo ili uyafahamu ni lazima ujihusishe directly au indirectly, vinginevyo uwe na hobby. Sasa kwa swala la kutoa masomo ya sheria inategemea na interest ya mtu kufahamu mambo ya elimu yatolewayo na wasabato. I bet kuna mengi pia hujui kwenye dhehebu lako coz labda huna interest nayo, au sio fani yako...!
 
Last edited by a moderator:
Kwa walea ambao tumebahatika kusoma vitabu vya huyu Mama ni mibaraka kwa kweli, kila aliye Mwadventista Msabato na asiyemwadventista hakika vinatubariki sana. Ninajivunia kuwa Mwadventista Msabato.

Ellen G. white haruhusu sheria za kidunia.
 
Mi sioni km hii ni issue sn mpk tufikie kusema kwamba walikua wameingizwa Chaka..... Maana sijawahi kusikia au kuona tukifundishwa Kua kusoma sheria au Kua mwanasheria ni dhambi...!

Kitendo cha kuacha kufundisha ni ishara ya walakini kwasababu ni somo ambalo ni uhimu sana kwenye maisha ya kila kisu

Na pia inaonekana hakukuwa na hiyo kozi kwenye vyuo vyenu mkuu,kwanini?

Na je ile sababu ambayo iliwafanya msiweke hiyo kozi imeondokaje?
 
Eiyer, kuna mambo ili uyafahamu ni lazima ujihusishe directly au indirectly, vinginevyo uwe na hobby. Sasa kwa swala la kutoa masomo ya sheria inategemea na interest ya mtu kufahamu mambo ya elimu yatolewayo na wasabato. I bet kuna mengi pia hujui kwenye dhehebu lako coz labda huna interest nayo, au sio fani yako...!

Nimekusoma mkuu ....!
 
Mimi ni mdau wa Chuo kikuu cha Arusha, ni kwamba mtaala wa kozi ya sheria kuanzia ngazi ya cheti umechelewa kukamilika tu lakini shahada hio itaanza kutolewa mwaka wa masomo
 
Mi sioni km hii ni issue sn mpk tufikie kusema kwamba walikua wameingizwa Chaka..... Maana sijawahi kusikia au kuona tukifundishwa Kua kusoma sheria au Kua mwanasheria ni dhambi...!
Na hapo ndo utaamini kuwa hivi vitu vinaletwa kwa makusudi tu ili mradi watu wapate pa kuanzia hayo ya walikuwa wameingizwa chaka yametoka wapi. Hivi ni Hiyo kozi ya sheria ni lazima sana kutolewa katika vyuo vyote duniani. Wapi imeandikwa msabato akipata kesi basi ni lazima atetewe na msabato mwenzie. Kuna vitu watu wanaanzisha just ku take your attention. Maake mada za wasabato ulikuwa umepita muda bila kujadiliwa naona watu waneona waanze tena. ulitaka kujua why wasabato hawafundishi law umepewa vyuo vinavyofundisha law then your assumption is wrong sababu vyuo vipo.
 
Mkuu, kwanza Chuo hakikulazimishi wewe usome kitu flani ndani ya siku flani, ningependa uufute kabisa huo mtazamo wako kwanza,
Fahamu kwanza utaratibu WA Chuo umewekwa kabla hata ya mwanafunzi kwenda hapo chuoni, Na hata kwenye sekta nyingine Ni vivyo hivyo, Na hauwezi kubadilishwa Na kitu kimoja kikaathiri wengi kwa sababu ya interest zako, kwa ifupi Chuo kinapopanga ratiba fulani huwa hawaangalii Ni nani muislam au mkristu kwa sababu like siyo suala la dini, kinachoangaliwa pale Ni itifaki ya Chuo husika ambayo mwanafunzi lazima aitambue kabla ya kufanya maamuzi ya kujiunga Na Chuo hicho (hapa nazungumzia kile kipindi TCU haijakuwa Na mandate ya kudahili wanafunzi)
...sasa Kama wewe Ni muislam alaf unaenda Chuo cha kinachomilikiwa Na mfumo kristu, ujue Kuna mambo lazma yatabase kwenye ukristu Na Ni lazma uyafuate Kama ukitaka, Na huwezi sema umenyimwa haki.

PIA ifahamike kuwa hata mitihani ya taasisi za elimu zinazomilikiwa Na serikali, huwa Kuna note inawekwa kuwa ratiba haitabadilishwa endapo tarehe ya mtihani itaangukia kwenye sikukuu za kitaifa n.k. (Christmas Na Eid nazo Ni sikukuu za kitaifa) Na hili nimeshalishuhudia Mkwawa University kipindi nipo chini ya UDSM, watu walifanya mtihani siku ya Christmas Na mwaka mpya. So usiwalaumu SAUT maana najua Wao ndo waliwafukuza wanafunzi wa kisabato walipogoma kufanya mtihani siku ya jumamosi.

Na sijui Ni haki gani SAUT waliyoikiuka, je, unaweza itaja? Na ukiitaja ueleze na mipaka ya haki za binaadamu, maana najua haki za binaadamu zina mipaka (check limitations of human rights)

Mfano mzuri Ni shule za kiislam, Kama Thaqaafa pale mwanza Na nyingine uzijuazo, (mdogo wangu Ni mkistu 100% Na kasoma pale, Na Mimi ndo nlikuwa ninampeleka so najua protocal zao hata kabla) hiyo shule wasichana Ni lazima wavae hijab, ambalo nna uhakika Ni vazi la kiislam Na lugha inayotumika Ni English au Arabic, so Na mdogo wangu alivaa na hakuna aliyelalamika. Kwasababu yeye ndiye aliyechagua wakati alikuwa Na options za kwenda shule nyingine tena za kikristu.

Sasa unataka kundi flani la watu wanaoabudu j5 Na Wao jumatano iwe siku ya mapumziko?, Kama Ni hivyo mbona waislam wanafanya mitihani ijumaa Na hawalalamiki?, hilo la wasabato limetoka wapi?, au Wao ndo wana haki zaidi, ukitaka kujibu anza kunijibu kuhusu ijumaa Na waislam kuhusu kufanya kazi Na kwenda mashuleni, then uendelee.

Tafakari.

Kama unaelewa hili basis hata huu uzi hauna mantik. Vyuo vya wasabato navyo ni taasisi ya kujiamulia vile watakavyo so isifanywe big deal.
 
Na hapo ndo utaamini kuwa hivi vitu vinaletwa kwa makusudi tu ili mradi watu wapate pa kuanzia hayo ya walikuwa wameingizwa chaka yametoka wapi. Hivi ni Hiyo kozi ya sheria ni lazima sana kutolewa katika vyuo vyote duniani. Wapi imeandikwa msabato akipata kesi basi ni lazima atetewe na msabato mwenzie. Kuna vitu watu wanaanzisha just ku take your attention. Maake mada za wasabato ulikuwa umepita muda bila kujadiliwa naona watu waneona waanze tena. ulitaka kujua why wasabato hawafundishi law umepewa vyuo vinavyofundisha law then your assumption is wrong sababu vyuo vipo.
Hata mimi naamini kuna vita ya baridi dhidi ya usabato..!
..Hata hivyo,vyuo vya wasabato kama zilivyo taasisi zingine, zina sheria zake na mipaka ayake kutokana na kanuni zilizowekwa. Kwa nini kunazuka maswali ya ajabu? Bahati mtu amejibiwa, lakini bado hataki kuelewa, anataka jibu alilojiwekea kichwani..!
 
ila haina shida ngoja watusaidie kututangazia kanisa letu the more they shout the more people wants to know how the adventist church is?haijalishi iwe positive or negative wanavyo taja taja watu watakuwa interested kuchimba na kuutafuta ukweli. infact wanatusaidia katika kutoa madodoso ya kuokoa roho za watu kazi inakuwa nyepesi. Alisema hata msipo piga kelele ninyi basi mawe yataongea. Naona mawe mwaka huu yanaongea sana kwa kweli na hiini dalili ya kuwa tumenyamaza sana
 
Kitendo cha kuacha kufundisha ni ishara ya walakini kwasababu ni somo ambalo ni uhimu sana kwenye maisha ya kila kisu

Na pia inaonekana hakukuwa na hiyo kozi kwenye vyuo vyenu mkuu,kwanini?

Na je ile sababu ambayo iliwafanya msiweke hiyo kozi imeondokaje?

Mkuu elimu ya sheria naona unaipa kipaombele kuliko elimu ya mwili na roho wakati wewe pia unakuja kuhukumiwa siku ya mwisho! ni ajabu sana. Kujua sheria za duniani is nothing to God, Mungu anacho himiza ni wewe mwanadamu kuishi apendavyo yeye yaani ufuate amri zake 10.
Swala la msingi ni wewe KUOKOA NAFSI YAKO USIINGAMIZE.
 
Kuna mambo ya Mungu na kuna mambo ya duniani

Huwezi kupuuza ya Mungu kwasababu unkwenda kwake
Huwezi kupuuza ya duniani kwakuwa uko duniani

Yesu aliagiza kuwa tunapokuwa hapa duniani tunatakiwa tujue kuwa tunahitajika tujue kuwa kuna serikali na tuipe yale ambayo ni halali kwayo NA NDIO MAANA ALISEMA TUMPE YA kAISARU YALE AMBAYO YANAMFAA NA YA mUNGU TUMPE PIA

Unapokuwa duniani halafu ukapuuza ya hapa duniani unakuwa unakosea sana,serikali inatambulika na Mungu na ndio maana ametuagiza tuiheshimu,unaposema tuzingatie tu ya kiroho unakuwa unamkosea Mungu pia

Kwa mantiki hiyo sasa,ndipo swali linakuja,ni kwanini kwenye vyo vya kisabato kulikuwa hakuna hili somo?

Nadhani utakuwa umeelewa!
 
Back
Top Bottom