Vyuo vya private na migpa mikubwa kwa nini?

1. Naungana nawe kushangaa tabia ya ajabu ya watu wanaojiita wamesoma kujisifia vyuo walivyosoma badala ya uwezo binafsi. Mwisho wa siku (generally speaking) hutaheshimika kwa jina la chuo chako isipokuwa quality ya unachokifanya/sema. Vinginevyo, labda utembee na label itakayokutambulisha ulikotoka (which is nonesense).

2. Je, ni kweli mfumo wa elimu unapendelea shule za serikali? Swali hili lina pande nyingi za shilingi. Hivi tunaposema serikali inapendelea shule zake tunaaminisha nini? Selection? Au mazingira ya ufundishaji na hamasa ya walimu kufanya kazi?
Kuhusu selection, mambo yamebadilika siku hizi. Zamani, ukienda shule za binafsi ilionekana huna uwezo kwa sababu mazingira ya shule za umma yalikuwa bora na hivyo watu walikimbilia mazingira bora. Siku hizi, kwa sababu ya ubovu wa shule za umma (sijui kama ndio kupendelewa?) mambo yamebadilika. Wazazi wengi wenye uwezo wa fedha wanawapeleka watoto wao shule binafsi. Ushahidi wa hili ni kwamba shule nyingi nzuri za binafsi hufanya selection kabla ya shule za serikali. The best brains (wengi) wenye uwezo kifedha wanaenda shule za binafsi, waliobaki (wasio na uwezo au kwa sababu za kiuchumi) wanaenda shule zetu za kata kusubiri kufeli.
Hivyo utaona kuwa upendeleo unaosemekana kufanywa na serikali kwa shule zake kwa maana ya selection ni nadharia tu. Wengi "wanaopendelewa" kwenda kwenye shule za umma, na wenywe nafasi kiuchumi, hawaendi labda wakipangwa shule zenye nafuu kama zile za serikali (za zamani) kwa imani kwamba kule kuna walimu na wnaafundisha.

3. Kwa nini shule za binafsi zinafanya vizuri?
Well, sababu ni nyingi. Moja, nyingi (hasa zile zenye majina) zinawalipa walimu wake vizuri na zina mifumo inayowabana wafundishe kwa ufanisi. Kwa mfano wakati mwalimu mpya mwenye Shahada anaweza kulipwa 400K serikalini, mwenzake anaweza kulipwa mpaka 1,500K kwenye shule binafsi. Wakati mwalimu wa serikalini hana morali ya kufundisha na hajawekewa mfumo wa kumdhibiti kufundisha, mwenzake wa shule binafsi ana morali na anadhibitiwa afundishe.

4. Hali ikoje vyuo vikuu (private v/s public)?.

Ili tuone kama yanayoendelea sekondari ndiyo yanayoendelea Vyuo Vikuu, ni vyema kujiuliza ubora wa elimu unategemea nini? Ubora wa elimu ya juu unategemea mambo mengi. Lakini kwa uchache kuna mambo manne makubwa.

Moja, ni mitaala/curriculum bora inayotafsiriwa kwa ufanisi kazini. Mtaala bora ni ule unaomnoa mwanafunzi wa elimu ya juu kumwelezesha kuboresha maisha ya jamii katika eneo alilosomea kwa ufanisi.

Pili, ubora wa members of the Faculty/wanataaluma waliobobea kwenye maeneo yao. Kuanzia ngazi ya chini kabisa ya TA mpaka juu, ni lazima Chuo Kikuu kihakikishe kina watu wenye uwezo kitaaluma kwa maana ya ufundishaji makini na kufanya tafiti zenye kuchangia katika body of knowledge kwa maeneo yao. Ndio maana kigezo cha kupanda madaraja kwa Walimu/Academicians wa vyuo vikuu si muda kazini bali idadi na kiwango cha tafiti walizofanya.

Tatu, ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Hapa tuna maana ya vifaa, vitabu, machapisho, maabara zenye viwango, mfumo mzuri wa kuwezesha wanafunzi kujenga tabia ya kutafiti na kadhalika.

Nne, ni ubora wa wanafunzi wanaochaguliwa. Hatuzungumzii matokeo/grades (ambazo nyingi zinaleta maswali mengi kuliko majibu) bali uwezo halisi wa wanafunzi (thinking, reasoning, originality, imagination, talents na kadhalika). Mtu anaweza kuwa na Division III kwenye mazingira mabovu lakini kichwa kimetulia kuliko mwenzake mwenye Division I ya kukaririshwa na mwalimu.

Baada ya kuangalia vigezo hivyo, sasa tuvigeukie vyuo vyetu kwa swali la jumla: Je, vinakidhi vigezo vya kutoa elimu bora? Je, vina teaching staff wenye sifa? Je, vina mitaala bora? Je, vina mazingira bora ya ufundishaji na kujifunzia? Je, ni kweli kuwa Vyuo vya Umma ni bora kuliko vile vya Binafsi?

Huenda tukatofautiana mitizamo (na mara nyingi watu hutetea vyuo walivyosoma/biases). Lakini kwa mtazamo wangu, huwezi kuchora mstari ulio wazi(clear) wa ubora kati ya vyuo vya serikali na vile vya umma. Nitajieleza.

Nchi hii kwa sasa ina vyuo vikuu ishirini na sita (26) ukiacha vile vishiriki. Katika hivyo 26, ni tisa (9) tu ndivyo vilivyo vya serikali na vilivyobaki vyote ni vya binafsi kwa maana ya kumilikiwa na mashirika ya kidini, wafanyabiashara binafsi.

Pamoja na ukweli wa mambo kuwa ni vyuo vichache sana vya umma vyenye advantage ya umri/ukongwe (Mlimani, Muhimbili SUA etc) vilivyoanza siku nyingi, vyuo vyetu vingi vya binafsi vinakabiliwa na changamoto ya uchanga kwani vingi vilianza miaka ya 2005 na vichache vikianza miaka ya 1997/8.

Kwa hiyo ni kweli kuwa Mlimani wana advantage kubwa. Kwa mujibu wa Mkandala (VC), chuo hicho kina zaidi ya Walimu/Faculty Members 600 wenye PhD (waliobaki ni au wanasoma au wanatarajia kusoma), na wanafanya sana tafiti zinazopatikana mtandaoni. Kwa upande wa ufundishaji, kwa kweli waliosoma pale mtakubaliana nami kuwa inategemea na Shule/College/Faculty. Lakini kimsingi ufundishaji sio kivile ingawa kina advantage ya resource nyingi za kumwezesha mwanafunzi kuelimika. Nenda East Africana pale Library unakutana na kila takataka inayoitwa desa kuanzia thesis za tangu miaka na miaka, vitabu, machapisho na kadhalika. Hali hii haipo kwenye vyuo vingi vigeni. Na advantage nyingine ni aina ya wanafunzi wanaochaguliwa, wengi wao wana uwezo wa kujisimamia na kusoma. The same to Muhimbili/SUA.

Lakini vyuo vingine vilivyobaki, hali ni tofauti kidogo. Kwa upande wa faculty members (moja wapo ya kigezo cha ubora) unaweza kukuta kuna chuo kina hadi watu watano wenye PhD (na wote ni maadministrators mfano SMMUCo, MUM, TEKU nk) na waliobaki ni ndugu zangu wenye shahada za mtaji. Tena unaweza kushangaa hata mwenye Bachelor ndio Dean wa Faculty (nenda TEKU, SMMUCo, UoA, MUCCOBs etc). Kwa upande wa mazingira ya kufundishia unaweza kukuta Chuo kina kajengo kamoja (UoA) na mambo yanaenda.

Kwa hiyo tukizungumzia ubora, tutakuwa tunakurupuka kudai kuwa vyuo hivi vinatoa elimu inayotegemewa. Ingawa naelewa vyuo hivi vingi vinatumia wahadhiri wa vyuo vikongwe kufundisha wanafunzi wao, lakini bado kuna walakini wa ufanisi. Mfano wanafunzi wa Masters Makumira wanafundishwa kozi nyingi na wahadhiri wa Mlimani (ambao huenda pale kwa muda mfupi) na wanafundisha kwa bidii kuliko wanavyofundisha kwenye ajira zao (lakini muda wa wiki mbili kufundisha kozi ya ya units 4-6 ni sawa?).

Hata hivyo huwezi kusema ni vyuo vya serikali peke yake. Constituent colleges za Mlimani na SUA nk zilizofumuka miaka ya majuzi nazo zinakabiliwa na hali hiyo hiyo. Nenda MUCE, MUCCOBS utakutana na yale yale unayokutana nayo TEKU, MWUCE, Mount Meru na kadhalika. Kwamba vigezo halisi vya kutoa elimu shindanishi havipo (havina wahadhiri wa kudumu wenye sifa, vinafundisha kwa mtindo wa zima moto, vina shida za utawala/ukabila/udini na matatizo mengine).

Hitimisho langu ni kwamba, huwezi kuja na sweeping statement ya "vyuo binafsi ni hovyo" kwa kuzingatia ushahidi nilioutoa hapo juu. Hata hivyo changamoto hizi tunazoziona katika vyuo vyetu vichanga (vya umma na binafsi) zinaweza kukabiliwa kadri muda unavyokwenda. Kama ushahidi wa manufaa ya umri, leo ukienda SAUT (kilichoanza mwaka 2003) utashangaa kinavyojitahidi kwenye ubora na kamwe huwezi kukibeza (na hadhi yake ni kubwa kuliko Mzumbe). Kina wahadhiri wengi seniours na waliobaki wanasoma, na kinajitahidi kwa resources. Nenda Kariuki (private) utaona kinavyojitahidi. Lakini kwa upande wa pili, vyuo vyote vichanga (UDOM, SJUT pamoja na colleges kama Ushirika nk) utakuta yale yale iwe ni public au private.

REFERENCES (Kwa wasio na allege ya kusoma):

Makulilo, V. B. (2012). The proliferation of private universities in Tanzania: Quality compromised?: University of Bayreuth, Germany: Wudpecker Journal of Educational Research Vol. 1(4), pp. 51 - 66, October 2012

Sifuna, D. N. & Sawamura, N. (2010). Challenges of Quality Education in Sub-Saharan African Countries: New York, Nova Science Publishers, Inc.,

Mosha, H. J. (2000). Conceptualizing Quality of Education. In Galabawa, J.C.J, et al. The Quality of Education in Tanzania: Issues and Experiences: Institute of Kiswahili Research, University of Dar es Salaam.
huwa napenda mijadala ya hoja namna hii, ikibidi nakubali kuwa hapa ama pale sikuwa sahihi ama kama pia hauko sahihi nitakuonyesha kiaje unapima pia, lakini wengi hawawezi kujadili kwa hoja namna hii,hata hivyo sitajibu hoja kwa hoja haya maelezo yote japo kuna maeneo nakubaliana nayo,lakini pia si kweli kuwa every private school or college is the best,hilo nalitambua sana,lakini kwa kiasi kikubwa private struggle to make their institution the best.

umechambua vizuri,ngoja kwanza nisome hayo makablasha uliyoyaweka hapo nione kilichomo ndani. lakini hata nikisoma si lazima nikubaliane na kila kitu ila naamini nitaongeza uelewa kwenye hili. thanks once more
 
Kama kweli wewe ulikua na akili darasani kwa nini ukose nafasi ya kuchaguliwa SPECIAL SCHOOLS! mbona sisi tulichaguliwa SPECIAL SCHOOLS? maana yake ulikuwa na marks za chini ukakosa hata shule za Govt za kawaida kama PUGU,TOSAMAGANGA,BAGAMOYO,MIRAMBO,MINAKI,GALANOS,MOSHTECH,MALANGALI ,n.k
 
,Mshinga mimi nimesomea TABORA SPECIAL SCHOOL(TABORABOYS)! ngoja nikuulize swali umesomea shule gani O-LEVEL,A-LEVEL ,Umesoma chuo gani na mwaka gani? nikukamate vizuri uabike humu jamvini!

wakati naitaja tabora boys nilikuwa najua umesoma pale maana nishaona umeandika hivyo, kwa kifupi sana,mimi sijawahi kusema nimesoma wapi, iwe O level ama A level ama chuo, zaidi nishaweka wazi shule yangu ya msingi,kwa nini sijwahi kuweka wazi? nina sababu zangu binafisi kama nilivyo sikuweka jina langu, ama ulivyo hukuweka jina lako.

ila huwezi kuniabisha kwa namna yoyote ile hata ukimpata mtu anaenijua physically and biographically, na sipo hapa kuweka profile yangu, labda ningekuwa public figure as a leader ikibidi ningefanya hivyo kama kuna demand.

ila niliyokueleza habari ndio hiyo,japo tabora boys ndio walikuwa washindani wetu kwenye kanda kipindi kile na kama umesoma tabora boys kweli utakuwa unajua shule zilizokuwa na ushindani western zone miaka ya 2000s.
 
bado hujajibu swali langu! mbona mimi nimesoma MZUMBE SEC Then TABORA BOYS siogopi kusema! hahahahah unaogopa kwa sababu ulichoandika ni uongo mtupu! kama unajiamini taja shule ulizosoma?
 
Kama kweli wewe ulikua na akili darasani kwa nini ukose nafasi ya kuchaguliwa SPECIAL SCHOOLS! mbona sisi tulichaguliwa SPECIAL SCHOOLS? maana yake ulikuwa na marks za chini ukakosa hata shule za Govt za kawaida kama PUGU,TOSAMAGANGA,BAGAMOYO,MIRAMBO,MINAKI,GALANOS,MOSHTECH,MALANGALI ,n.k
wapi iliwahi kuandikwa kila mwenye akili za darasani ataenda special schools? ama hizo shule ulizozitaja. kuwa na marks za chini kwa darasa la saba kiasi cha kukosa nafasi kwenda government schools siwezi kukataa,lakini hilo peke yake halitoshi kusema nilikuwa na uwezo mdogo kulinganisha wengine.

unatakiwa kujua kuwa si kila aliyefika hizo shule alistahili,wengine waliziba nafasi yangu na hawakustahili kama kigezo pekee kilikuwa marks, najua na hata sasa walimu wanawafanyia baadhi ya wanafunzi mitihani, na kati ya hao wengine wanachaguliwa hizo shule lakini mimi toka darasa la kwanza sikuwahi kufanyiwa mtihani wala kuiba mtihani.

pia unatakiwa kujua mazingira ya shule niliyosoma shule ya msingi na stahili ya marks nilizosoma. nilisoma shule ya kawaida sana ambayo kwa kumbukumbu zangu ni mara moja tu iliwahi kufaulisha wanafunzi tena kwenda shule ya wazazi na hakuna tena shule iliyowahi kufanya hivyo kwenye kata hiyo. kifupi ni kwamba elimu ilikuwa chini sana maeneo yale ila si kwamba wanafunzi ndio hawakuwa na uwezo.

mpaka sasa nenda kwenye website ya wizara ya elimu,utakuta shule zote za msingi zilizowekewa na ufaulu wa juu hakuna hata shule moja ya serikali kati ya maelefu ya shule. na hizo special schools zinaangalia wingi tu wa marks kwa kiasi kikubwa lakini kuna mikoa mingine elimu iko chini sana mpaka sasa, unapaswa kujua haya.

lakini nisingekuwa na uwezo kabisa naamini hata baada ya kusoma private singefeli,lakini hilo halikutokea tena. na wewe unasemaje inapotokea mwanafunzi yupo hizo special schools na anafeli?utasema alikuwa special kuliko yule aliyefaulu katika shule nyingine isiyo special hata kama hakuchaguliwa special?
 
bado hujajibu swali langu! mbona mimi nimesoma MZUMBE SEC Then TABORA BOYS siogopi kusema! hahahahah unaogopa kwa sababu ulichoandika ni uongo mtupu! kama unajiamini taja shule ulizosoma?

hata nikitaja shule bado utahitaji maelezo yangu kunifahamu mimi,na kila kitu kinachonihusu mimi, ama unataka kulinganisha shule nilizosoma?
 
Ninachotaka nikukukamata uabike humu jamvini (jf) eti "sijawahi kufeli" nipo TABORA nafanya FIELD nitakuabisha kabisa ukitaja shule ulizosomea ! najua ushakiri kwamba uwezo wako darasani kiakili ni mdogo ndio maana hukuchaguliwa Govt SCHOOLS! ,
 
sasa kama unataka matokeo yangu si uniambie nikupe matokeo,kwani shule niliyosoma itakupa matokeo?ama nikitaja tu shule utakuwa umejua matokeo yangu. kweli akili zako ni fupi sana, kama hawa ndio special students i dare to say nothing special in them kama nilivyosema,nilikuwa nikiwazidi matokeo lundo la hao special kwenye hiyo mitihani yote ya NECTA.

nilishasema pia hakuna mtoto wangu atakaesoma government schools, unless nife leo. hakuna shule hata moja kwa sasa yenye hali nzuri ikiwa na mazingira stahiki kwa mwanafunzi. endelea kuamini sina akili huku umeshindwa kabisa kufurukuta kwenye kujadili mada.

sishangai sana maana hata tunao wasomi wa kukariri kama wewe wasio na uelewa kabisa.
 
sasa kama unataka matokeo yangu si uniambie nikupe matokeo,kwani shule niliyosoma itakupa matokeo?ama nikitaja tu shule utakuwa umejua matokeo yangu. kweli akili zako ni fupi sana, kama hawa ndio special students i dare to say nothing special in them kama nilivyosema,nilikuwa nikiwazidi matokeo lundo la hao special kwenye hiyo mitihani yote ya NECTA.

Taja umepata one ya ngapi(NECTA) na shule uliyosoma ,ili tukaprove kama ni kweli maana unaweza ukasema umepata one ya 7 kumbe kwenye shule yako hamna mwenye matokeo hayo ,,haya nijibu swali hilo
 
kila ogani ya mwili iliumbwa kwa kazi maalumu, ili kuruhusu mfumo mzima wa mwili kufanya kazi sawasawa, sasa kwa mfano, ukichanganya kazi ya kichwa ifanyike na makalio, shida yake lazima uione.. Nadhani vijana hapo juu wameelewa.
 
Taja umepata one ya ngapi(NECTA) na shule uliyosoma ,ili tukaprove kama ni kweli maana unaweza ukasema umepata one ya 7 kumbe kwenye shule yako hamna mwenye matokeo hayo ,,haya nijibu swali hilo
kwa nini unakimbilia one ya saba? kwa nini usifikirie nitaje hata four ya 30 ya wakati huo?
 
Hahahahah unamatatizo ya akili wewe! umesema umewahi kufanya vizuri kwenye mitihani ya WESTERZONE,na NECTA! utaongozaje na iv.30? kwa taarifa yako sasa kanda magharibi huwezi kuongoza kama hauna one ya 7-10 form 4 na Kwa ADVANCE huwezi kuongoza kama hauna one ya 3-mpaka 5! ,tayari nishakuona ni muongo na mbabaishaji ! na tayari nishakukamata
 
utakuwa unamatatizo ya macho kama huna makengeza mana nahisi kuna mahali umeruka kusoma,rudi tena ukasome sawasawa nilichoandika kama kinaendana na haya maelezo yako. ama ndio mwendelezo wa kushindwa kuelewa mantiki ya unachojibu.
 
kwa nini unakimbilia one ya saba? kwa nini usifikirie nitaje hata four ya 30 ya wakati huo?

kaka achana nae huyo bado ana ulimbukeni wa first year, akifika semister ya 4 second year ataheshimu wakubwa zake baada ya kupata supp za kutokosha na hapo ndipo atajitambua!
 
IV.30 alafu uongoze WESTERN ZONE? nimekimbilia one ya 7 kwa sababu huwezi kuongoza kanda ya magharibi bila ya kuwa na 7-10, mpaka hapa umeonekana ni dhaifu,muoga,huna akili darasani,kichwa ngumu
 
kaka achana nae huyo bado ana ulimbukeni wa first year, akifika semister ya 4 second year ataheshimu wakubwa zake baada ya kupata supp za kutokosha na hapo ndipo atajitambua!

nashangaa sana mtu mwenyewe kashindwa kabisa hata kuonyesha uwezo kidogo wa kujenga hoja,alafu anataka matokeo yangu ambayo hayana msaada wowote kwenye mada inayojadiliwa na muasisi ni yeye huku ameshindwa kujibu za msingi za wadau ama hata kuzikosoa na ameshindwa kuwa na displine katika mada kwa kurukia mambo nje ya mada.

naelewa sana misingi ya mijadala ndio mana niliamua kwenda nae hivyo hivyo kwa akili yake. lakini hatambui kuwa hapa hata nikiweka wazi matokeo yangu anaweza kunyamaza ama akatafuta kasababu kengine hata kama hakana msingi, natambua kuwa matokeo yoyote yaliyo yangu hayawezi kujibu hoja za mada hii ila majibu ya mada hii nimeyatoa ambapo hajajibu hata hoja moja kati ya nyingi nilizoeleza.

pia yeye hajui kuwa matokeo binafisi si kigezo cha mjadala hapa,mfano wapo wanajadili hapa pengine wameishia form four lakini wanweza kuwa na michango mizuri kuliko yeye aliyepita hiyo 4,pia wapo hapa wenye masters na PHD na maprofesa, je watu wasijadili kisa wao si wenye elimu kubwa? akikua ataacha.

ngoja niachane nae niangalia vitu vya msingi vya kujadili na watu waelewa.
 
maelezo mazuri.. nadhani wataelewa kinagaubaga..

1. Naungana nawe kushangaa tabia ya ajabu ya watu wanaojiita wamesoma kujisifia vyuo walivyosoma badala ya uwezo binafsi. Mwisho wa siku (generally speaking) hutaheshimika kwa jina la chuo chako isipokuwa quality ya unachokifanya/sema. Vinginevyo, labda utembee na label itakayokutambulisha ulikotoka (which is nonesense).

2. Je, ni kweli mfumo wa elimu unapendelea shule za serikali? Swali hili lina pande nyingi za shilingi. Hivi tunaposema serikali inapendelea shule zake tunaaminisha nini? Selection? Au mazingira ya ufundishaji na hamasa ya walimu kufanya kazi?
Kuhusu selection, mambo yamebadilika siku hizi. Zamani, ukienda shule za binafsi ilionekana huna uwezo kwa sababu mazingira ya shule za umma yalikuwa bora na hivyo watu walikimbilia mazingira bora. Siku hizi, kwa sababu ya ubovu wa shule za umma (sijui kama ndio kupendelewa?) mambo yamebadilika. Wazazi wengi wenye uwezo wa fedha wanawapeleka watoto wao shule binafsi. Ushahidi wa hili ni kwamba shule nyingi nzuri za binafsi hufanya selection kabla ya shule za serikali. The best brains (wengi) wenye uwezo kifedha wanaenda shule za binafsi, waliobaki (wasio na uwezo au kwa sababu za kiuchumi) wanaenda shule zetu za kata kusubiri kufeli.
Hivyo utaona kuwa upendeleo unaosemekana kufanywa na serikali kwa shule zake kwa maana ya selection ni nadharia tu. Wengi "wanaopendelewa" kwenda kwenye shule za umma, na wenywe nafasi kiuchumi, hawaendi labda wakipangwa shule zenye nafuu kama zile za serikali (za zamani) kwa imani kwamba kule kuna walimu na wnaafundisha.

3. Kwa nini shule za binafsi zinafanya vizuri?
Well, sababu ni nyingi. Moja, nyingi (hasa zile zenye majina) zinawalipa walimu wake vizuri na zina mifumo inayowabana wafundishe kwa ufanisi. Kwa mfano wakati mwalimu mpya mwenye Shahada anaweza kulipwa 400K serikalini, mwenzake anaweza kulipwa mpaka 1,500K kwenye shule binafsi. Wakati mwalimu wa serikalini hana morali ya kufundisha na hajawekewa mfumo wa kumdhibiti kufundisha, mwenzake wa shule binafsi ana morali na anadhibitiwa afundishe.

4. Hali ikoje vyuo vikuu (private v/s public)?.

Ili tuone kama yanayoendelea sekondari ndiyo yanayoendelea Vyuo Vikuu, ni vyema kujiuliza ubora wa elimu unategemea nini? Ubora wa elimu ya juu unategemea mambo mengi. Lakini kwa uchache kuna mambo manne makubwa.

Moja, ni mitaala/curriculum bora inayotafsiriwa kwa ufanisi kazini. Mtaala bora ni ule unaomnoa mwanafunzi wa elimu ya juu kumwelezesha kuboresha maisha ya jamii katika eneo alilosomea kwa ufanisi.

Pili, ubora wa members of the Faculty/wanataaluma waliobobea kwenye maeneo yao. Kuanzia ngazi ya chini kabisa ya TA mpaka juu, ni lazima Chuo Kikuu kihakikishe kina watu wenye uwezo kitaaluma kwa maana ya ufundishaji makini na kufanya tafiti zenye kuchangia katika body of knowledge kwa maeneo yao. Ndio maana kigezo cha kupanda madaraja kwa Walimu/Academicians wa vyuo vikuu si muda kazini bali idadi na kiwango cha tafiti walizofanya.

Tatu, ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Hapa tuna maana ya vifaa, vitabu, machapisho, maabara zenye viwango, mfumo mzuri wa kuwezesha wanafunzi kujenga tabia ya kutafiti na kadhalika.

Nne, ni ubora wa wanafunzi wanaochaguliwa. Hatuzungumzii matokeo/grades (ambazo nyingi zinaleta maswali mengi kuliko majibu) bali uwezo halisi wa wanafunzi (thinking, reasoning, originality, imagination, talents na kadhalika). Mtu anaweza kuwa na Division III kwenye mazingira mabovu lakini kichwa kimetulia kuliko mwenzake mwenye Division I ya kukaririshwa na mwalimu.

Baada ya kuangalia vigezo hivyo, sasa tuvigeukie vyuo vyetu kwa swali la jumla: Je, vinakidhi vigezo vya kutoa elimu bora? Je, vina teaching staff wenye sifa? Je, vina mitaala bora? Je, vina mazingira bora ya ufundishaji na kujifunzia? Je, ni kweli kuwa Vyuo vya Umma ni bora kuliko vile vya Binafsi?

Huenda tukatofautiana mitizamo (na mara nyingi watu hutetea vyuo walivyosoma/biases). Lakini kwa mtazamo wangu, huwezi kuchora mstari ulio wazi(clear) wa ubora kati ya vyuo vya serikali na vile vya umma. Nitajieleza.

Nchi hii kwa sasa ina vyuo vikuu ishirini na sita (26) ukiacha vile vishiriki. Katika hivyo 26, ni tisa (9) tu ndivyo vilivyo vya serikali na vilivyobaki vyote ni vya binafsi kwa maana ya kumilikiwa na mashirika ya kidini, wafanyabiashara binafsi.

Pamoja na ukweli wa mambo kuwa ni vyuo vichache sana vya umma vyenye advantage ya umri/ukongwe (Mlimani, Muhimbili SUA etc) vilivyoanza siku nyingi, vyuo vyetu vingi vya binafsi vinakabiliwa na changamoto ya uchanga kwani vingi vilianza miaka ya 2005 na vichache vikianza miaka ya 1997/8.

Kwa hiyo ni kweli kuwa Mlimani wana advantage kubwa. Kwa mujibu wa Mkandala (VC), chuo hicho kina zaidi ya Walimu/Faculty Members 600 wenye PhD (waliobaki ni au wanasoma au wanatarajia kusoma), na wanafanya sana tafiti zinazopatikana mtandaoni. Kwa upande wa ufundishaji, kwa kweli waliosoma pale mtakubaliana nami kuwa inategemea na Shule/College/Faculty. Lakini kimsingi ufundishaji sio kivile ingawa kina advantage ya resource nyingi za kumwezesha mwanafunzi kuelimika. Nenda East Africana pale Library unakutana na kila takataka inayoitwa desa kuanzia thesis za tangu miaka na miaka, vitabu, machapisho na kadhalika. Hali hii haipo kwenye vyuo vingi vigeni. Na advantage nyingine ni aina ya wanafunzi wanaochaguliwa, wengi wao wana uwezo wa kujisimamia na kusoma. The same to Muhimbili/SUA.

Lakini vyuo vingine vilivyobaki, hali ni tofauti kidogo. Kwa upande wa faculty members (moja wapo ya kigezo cha ubora) unaweza kukuta kuna chuo kina hadi watu watano wenye PhD (na wote ni maadministrators mfano SMMUCo, MUM, TEKU nk) na waliobaki ni ndugu zangu wenye shahada za mtaji. Tena unaweza kushangaa hata mwenye Bachelor ndio Dean wa Faculty (nenda TEKU, SMMUCo, UoA, MUCCOBs etc). Kwa upande wa mazingira ya kufundishia unaweza kukuta Chuo kina kajengo kamoja (UoA) na mambo yanaenda.

Kwa hiyo tukizungumzia ubora, tutakuwa tunakurupuka kudai kuwa vyuo hivi vinatoa elimu inayotegemewa. Ingawa naelewa vyuo hivi vingi vinatumia wahadhiri wa vyuo vikongwe kufundisha wanafunzi wao, lakini bado kuna walakini wa ufanisi. Mfano wanafunzi wa Masters Makumira wanafundishwa kozi nyingi na wahadhiri wa Mlimani (ambao huenda pale kwa muda mfupi) na wanafundisha kwa bidii kuliko wanavyofundisha kwenye ajira zao (lakini muda wa wiki mbili kufundisha kozi ya ya units 4-6 ni sawa?).

Hata hivyo huwezi kusema ni vyuo vya serikali peke yake. Constituent colleges za Mlimani na SUA nk zilizofumuka miaka ya majuzi nazo zinakabiliwa na hali hiyo hiyo. Nenda MUCE, MUCCOBS utakutana na yale yale unayokutana nayo TEKU, MWUCE, Mount Meru na kadhalika. Kwamba vigezo halisi vya kutoa elimu shindanishi havipo (havina wahadhiri wa kudumu wenye sifa, vinafundisha kwa mtindo wa zima moto, vina shida za utawala/ukabila/udini na matatizo mengine).

Hitimisho langu ni kwamba, huwezi kuja na sweeping statement ya "vyuo binafsi ni hovyo" kwa kuzingatia ushahidi nilioutoa hapo juu. Hata hivyo changamoto hizi tunazoziona katika vyuo vyetu vichanga (vya umma na binafsi) zinaweza kukabiliwa kadri muda unavyokwenda. Kama ushahidi wa manufaa ya umri, leo ukienda SAUT (kilichoanza mwaka 2003) utashangaa kinavyojitahidi kwenye ubora na kamwe huwezi kukibeza (na hadhi yake ni kubwa kuliko Mzumbe). Kina wahadhiri wengi seniours na waliobaki wanasoma, na kinajitahidi kwa resources. Nenda Kariuki (private) utaona kinavyojitahidi. Lakini kwa upande wa pili, vyuo vyote vichanga (UDOM, SJUT pamoja na colleges kama Ushirika nk) utakuta yale yale iwe ni public au private.

REFERENCES (Kwa wasio na allege ya kusoma):

Makulilo, V. B. (2012). The proliferation of private universities in Tanzania: Quality compromised?: University of Bayreuth, Germany: Wudpecker Journal of Educational Research Vol. 1(4), pp. 51 - 66, October 2012

Sifuna, D. N. & Sawamura, N. (2010). Challenges of Quality Education in Sub-Saharan African Countries: New York, Nova Science Publishers, Inc.,

Mosha, H. J. (2000). Conceptualizing Quality of Education. In Galabawa, J.C.J, et al. The Quality of Education in Tanzania: Issues and Experiences: Institute of Kiswahili Research, University of Dar es Salaam.
 
nashangaa sana mtu mwenyewe kashindwa kabisa hata kuonyesha uwezo kidogo wa kujenga hoja,alafu anataka matokeo yangu ambayo hayana msaada wowote kwenye mada inayojadiliwa na muasisi ni yeye huku ameshindwa kujibu za msingi za wadau ama hata kuzikosoa na ameshindwa kuwa na displine katika mada kwa kurukia mambo nje ya mada.

naelewa sana misingi ya mijadala ndio mana niliamua kwenda nae hivyo hivyo kwa akili yake. lakini hatambui kuwa hapa hata nikiweka wazi matokeo yangu anaweza kunyamaza ama akatafuta kasababu kengine hata kama hakana msingi, natambua kuwa matokeo yoyote yaliyo yangu hayawezi kujibu hoja za mada hii ila majibu ya mada hii nimeyatoa ambapo hajajibu hata hoja moja kati ya nyingi nilizoeleza.

pia yeye hajui kuwa matokeo binafisi si kigezo cha mjadala hapa,mfano wapo wanajadili hapa pengine wameishia form four lakini wanweza kuwa na michango mizuri kuliko yeye aliyepita hiyo 4,pia wapo hapa wenye masters na PHD na maprofesa, je watu wasijadili kisa wao si wenye elimu kubwa? akikua ataacha.

ngoja niachane nae niangalia vitu vya msingi vya kujadili na watu waelewa.

Humu wapo watu wa aina nyingi sana. Wakati mwingine unajaribu kujitahidi kujadiliana na mtu hata mwenye uelewa mfupi kama huyu anayejiita mpigamsuli na ID nyingine anazotumia kutukana. Lakini kwa kweli unapokuta mtu wa namna hii, ambaye mbali na kutokuwa na hoja yoyote ya maana, amejaa matusi ya hovyo hovyo, maoni ya jumla jumla yasiyo na utafiti wowote, uamuzi mzuri ni kumpuuza na kumwacha akajadiliane na wanaofanana nao.
 
Hapa ndo tunaona nani mkorofi! siwezi kukubaliana na mawazo yako hata kidogo kwa sababu nilichoandika kwenye thread yangu kipo wazi kabisa nani hajui vyuo vya PRIVATE wanagraduate na G.P.A Kubwa? Nani anayebisha kwamba vyuo vya PRIVATE vinachukua division three nyingi na mbovu? Nilichoandika ni ukweli na nitaupigania kwa nguvu zote halaaa
 
Back
Top Bottom