Vyuo vyetu vya Kilimo ni kupoteza muda tu, there is no learning taking place with regard to Kilimo na ufugaji

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Vijana wanamaliza hivi vyuo wakiwa hawajui lolote kwa miaka mitatu ya certifcate na diploma.

Nimemhoji kijana amemaliza certificate kutoka MATI Mtwara, Mtoto amesoma certificate in Kilimo na Mifugo, unamuuliza ECF ni nini hajui! Kupiga sindano ng'ombe hajui! Hakuna ugonjwa wowote wa mimea anaoujua.

Ndio wahitimu, lk si kosa lao. Mfano MTwara Agricultural Trainig Institute wanachowafanya watoto ni kulima tu mashamba ya korosho etc. Ni kama manamba, wako pale as a source of labour and not to learn agricultural and animal science be fit to be employed or self-employed.

Hawawezi kuajiliwa popote au kujiajiri maana unamuuliza kuku wanafugwaje hajui..., magonjwa ya kuku ni yapi, hajui. Watafute mkawaulize

( Nisi generalise, lkn for MATI Mtwara is a waste of time for our kids!
 
Mi nadhani hii iko kwenye kila taaluma hapa tz, nenda hata chuo kikuu utakutana na wanachuo wengi wanjua wanachokisoma lakini ukiwauliza wanaweza kufanya nn kwa taaluma yao hawana clear picture,

Pia unaweza ukawa umekutana na yule mtu wa mwisho darasani, umehoji wangapi na kuthibitisha utafiti wako juu y vyuo hivyo?
 
Nitangulie kwanza kukusifu kwa maneno yako ya mwishoni kabla ya kukukosoa, kuwa usigeneralize.Ni hivi Ndugu yangu research yako umeifanya kwa mtu mmoja ambaye inawezekana hakuwa na interest na Kilimo zaidi ya kulazimishwa tu na Wazazi/walezi kusoma Kilimo, Hivyo inawezekana alikuwa mtoro.
 
Kwa tanzania km umezaliwa kijijini sioni umuhimu wa kwenda chuo cha kilimo kwani tayari unakuwa ntaalam
Ulichokisema ni sawa na kusema "mtu ukizaliwa Tanzania hakuna haja ya kufundishwa kiswahili shuleni"

Je, huko kijijini wanalima kitaalamu au kwa mazoea? Wanafahamu magonjwa ya mimea na tiba zake? Wanafanya tafiti za mbinu mpya za kilimo na kilimo-biashara..???
 
Umeona eenhh??!!.
 
Ana interest Sana, Tena GPA ya over 4. Highly determined to have a degree in agriculture ndiyo maana alikazana kupata GPA kubwa isije mletea kikwazo
 
Ana GPA kubwa ,over 4
 
Labda wamebobea kwenye umanamba. Wape majembe, mapanga, shoka halafu uone

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Kilimo ni wito, kama mtu hana wito hata asome vipi hawezi kuchukulia umuhimu. Pamoja na hilo bado nchi yetu haijaweka mkazo sana kwenye kilimo nafikiri kwasababu ya kukosekana kwa viwanda vya kutosha hivyo kudababisha ukosefu wa masoko ya uhakika wa kuuza malighafi zitokanazo na kilimo
 
Hivyo ni vitu minor atajufunzia kwa komgamano au semina
 
Ana interest Sana, Tena GPA ya over 4. Highly determined to have a degree in agriculture ndiyo maana alikazana kupata GPA kubwa isije mletea kikwazo
Sawa,lkn bahati mbaya sana wanafunzi wanaopata GP kubwa huwa sio wazuri Sana kujieleza.
 
Mi siamini.

Yaani na kufaulu kafaulu ila hajui hata gonjwa moja? Sasa mitihani ilikua ina maswali gani?
 
Mleta mada naona watu wengi wanachangia kimzaha mzaha, lakini unachoongea kina ukweli mkubwa na hii ni matokeo ya kuingiza siasa na kutafuta ulaji na maslahi binafsi kwenye maeneo yanayohitaji weledi zaidi.

Ukilinganisha wazee waliosoma diploma miaka hiyo ambao wengi wamestaafu na hawa wa kizazi kipya utagundua tofauti kubwa sana kwenye uelewa wao wa mambo na namna ya kufanya mambo in a practical way. Anyway, tuendelee kukusanya tozo kwa ajili ya mafuta ya ma viieite, ndege na kufanya shooting ya vivutio vya utalii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…